habari wana jm f,nadhani Watanzania wengi sasa wanafatilia Bunge la Katiba, na kwa sasa ni TBC pekee ambao wanarusha matangazo ya bunge hili moja kwa moja (sijui kwa nini TV zingine hazirushi matangazo ya bunge hili live) ila ,kwa kitendo walichofanya jana cha kutukatia matangazo nadhani kwa watu makini hakikubaliki na si tu hakikubaliki bali hakivumiliki na si cha kukifumbia macho hata kidogo. Haiwezekani kituo ambacho kinajinasibu kuwa ni cha taifa kikawa kinafanya mambo ambao tunayaona kabisa yanamlengo tofauti, si kazi yake chombo hiki kuwafanya watanzania wamsikilize nani na nani wasimsikilize ,si kazi yake kuwachagulia watanzania kitu cha kusikiliza na si kazi yake kufanya siasa,kama ambavyo hakipaswi kuonekana kinaunga mkono chama au kikundi chochote hasa katika swala la kutunga katiba ya nchi. Cha kushangaza chombo hiki cha TBC moja kwa moja kinaonekana kuwa upande wa CCM kwa kila jambo,na kimefikia hatua ya kukata matangazo pale tu watu wanaotoa hoja zinazopingana na CCm wanapowakilisha hoja zao,hii inaonyesha kuwa mchezo huu si huru kama unavyopaswa kuwa.
TUKUMBUKE KUWA WALIMFUKUZA TIDO MHANDO KWA SABABU TU ALIENDELEA NA MPANGO WA KUENDESHA KIPINDI CHA MCHAKATO MAJIMBONI-kwake haikuwa rahisi kukisitisha kwa kuwa walishahafikiana na shirika la BBC ambao waliwezesha kipinde kile kiwe hewani lakini kwa kuwa watu wa chama flani waliona hakina masirahi kwao wakamkataza kukirusha japo kwa kuwa yeye ni msafi alikirusha na yaliyomkuta wote tunajua.
SASA WAKATI WA KULALAMA NADHANI UMEPITA..Watanzania ambao kodi zetu zinaendesaha kituo hiki tunapaswa kuchukua hatua stahiki ili waelewe kwa vitendo kuwa tumechoka na vitendo vyao vya KIZANDIKI,KISHENZI,KIJUHA NA MANENO YOTE MABAYA WANAYOLANDANA NAO. TUELEWE KUWA WANAJUA KUWA HATUPENDI, ILA WANAFANYA KWA KIBURI KUWA TUTAFANYA NINI ,SASA TUWAONYESHE KUWA TUNAWEZA FANYA KITU JUU YAO.
NINATOA WAZO HILI HILI KWA MTU ANAYEWEZA KUTUPA USHAURI NA ITAKUWA VIZURI KAMA UKIWA WA KISHERIA NA KAMA HAKUNA JAPO TUAMBIANE NINI CHA KUFANYA ..BINAFSI NAWAZA KUANDAMANA PAKA OFISI ZA tbc NA MABANGO YENYE JUMBE MBALIMBALI JUU YA KERO HII..HII ITASAIDIA KWA KUWA WAANDISHI WA TV MAKINI KAMA itv, star tv,na waandishi wa magazeti kama ----- na MwanaNchi na wengineo watarusha habari hii na hii itakuwa aibu kubwa kwao.
kisha maandamano hayo yataelekea vituo vya ITV na STAR TV kuwalaumu kwa nini wanatuacha watanzania katika kutupa habari za bunge la katiba wakati wao ndio tegemeo letu na wao ndio tunaowategemea kama vituo vya TAIFA.
Kama tunaweza kuwasiliana na vyombo vingine kama watu wa HAKI ZA BINADAMU katika kupigania hili kwani habari ni moja ya haki zetu za msingi.
JAMANI HAYA NI MAWAZO YANGU NAOMBA MICHANGO YA KUFANIKISHA HILI. NA KAMA KUNA MTU ANAWEZA NIPA NAMBA YA MTU NAYEWEZA KUWASILIANA NAE KATIKA KULIWEZESHA HILI TAFADHARI NAOMBA.
na kama una kitu muhimu juu la hili na ungependa hiwe siri basi ni PM
nawakilisha wana jamii f.
bajar musica gratis