Sasa mtu anaongea live utahariri vipi hapo?!
Unajua maana ya kuhariri?
Tbc haialiki wahuni.
Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na Star tv,mh.Machali amekiponda kituo cha tetevision cha umma cha TBC 1 kuwa kina tabia mbaya ya kualika watu wenye mtizamo wa chama kimoja na hapa alikuwa akimanisha wafuasi wa CCM ndio wanaoalikwa.Mh machali ameongeza kuwa anakatwa kodi kuiendesha TBC na kile ni chomba cha umma.
Wakati huo huo,Machali ameisifu Star tv kwa kualika wageni bila kupendelea upande wowote,ambapo leo amealikwa yeye pamoja na mh.Assupter Mshana kutoka CCM kama wageni kujadili yanayojiri katika bunge la katiba na mada ya leo ikihusu uhakisi wa Tanzania kwenye Hati ya Muungano.
MY TAKE:
TBC kweli wana tabia mbaya.
Kama serikali ya CCM inaonekana kuitumia TBC kwa sababu za kisiasa,je huu si ushahidi wa kimazingira wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya dola(polisi) kwa madhumuni hayo hayo?
Labda CCM ya miaka hii ndiyo imekuwa OGA ya kukimbia midahalo yenye HOJA na KUFIKIRISHA akili. Mbona Nyerere alikuwa anakuja Nkrumah Hall (UDSM) na kutukabiri kwa hoja na sometimes kututoa nock out! Mbona BW Mkapa 1995 alimkabiri Mrema kwenye mdahalo wa wazi wa president candidates na kumpiga nock out Mrema!
Wanajiona kuwa wao ni Wana CCM na kusjisahau kuwa wao ni Watanzania.
Sasa hapo uzushi wangu upo wapi?
Pamoja na ubaya wote wa TBC lakini mtu au taasisi ikikiuka ethics tukae kimya na kutokumueleza?
Kutumia chombo fulani cha habari kukikandia chombo kingine cha habari tena vilivyo katika kada moja sio maadili sahihi na hata sheria inaweza kutumika kushtakiana...
Hivi si unafahamu kuwa kuna Uhariri wa habari?
Toka lini mahijiano ya live yakahaririwa au zile f**k za kule bungeni zilizokuwa tinatemwa na kigwangala zilihaririwa na hao tbccm
kwanzia hii siku niliwaogopa tbccm
Ulitaka kwenye hivyo vipindi vya asubuhi wahojiwe makada wa CHADEMA wasio na staha katika lugha zao? TBC ni chombo cha umma na kinalinda maslahi ya Umma, wengi wanaohojiwa sio tu ni makada wa CCM pia ni viongozi wa serikali. Sioni ubaya hapo!