Dar_Millionaire
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 227
- 89
Sasa hivi katika majumuisho ya bajeti ya wizara ya ujenzi Mh. Aden Rage ameuliza, "Jana nilisikia TBC kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku kuwa makandarasi wa barabara mkoani Tabora wamegoma kwa sababu ya kucheleweshewa malipo. Namuomba mheshimiwa waziri au naibu waziri [wa ujenzi] atoe kauli kuhusu hilo"
Naibu waziri akaeleza kuwa hata yeye aliona taarifa hiyo kwenye TV ya TBC jana usiku. Hata hivyo alishangaa kuona Meneja wa Mkoa wa Tabora wa TANROADS akinukuliwa laivu kwenye hiyo taarifa ilhali meneja huyo yupo Dodoma na amekuwepo hapo Dodoma kwenye kikao cha Bunge kwa wiki mbili zilizopita.
Baada ya kuwasiliana na meneja wake huyo, ndipo ikabainika kuwa hiyo video ya kauli ya meneja ni ya miezi mitano iliyopita, TBC wame-cut na kupaste ili kutengeneza habari.
Waziri akamalizia kwa kutoa onyo kwa TBC waache ubabaishaji na kuipaka tope serikali.