TBC ifutwe, ni ufisadi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC ifutwe, ni ufisadi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, May 20, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika tukio la mauaji yaliyotokea Tarime (North Mara Mine) shirika la utangazaji la taifa limeonyesha mapungufu makubwa na kupoteza kabisa umuhimu wa kuwepo kwake, kwa siku mbili mfululizo wametoa kwenye taarifa zao za habari (prime time) za saa mbili kuhusu tukio hili lakini cha ajabu hakuna hata sehemu moja ambapo wamewapa fursa waathirika kueleza upande wao wa habari, kwa siku zote wamemnukuu Kagasheki na Kamanda wa polisi lakini hakuna sehemu yoyote ambapo wamewanukuu wanaotuhumiwa kuvamia mgodi ili nao watupe upande wao lakini hilo halijatokea.

  Kwa mtazamo wangu TBC imegeuka kuwa chombo cha wanasiasa walioko madarakani (CCM) na si cha watanzania kama ambavyo sababu za kuundwa kwake zinaeleza, kwa hiyo uendeshaji wa chombo hiki kuendelea kugharimiwa na watanzania wote ni UFISADI, ni bora basi CCM wakakichukua na kulipia uendeshaji wake kwa sababu kinaendeshwa kwa matakwa ya CCM siyo watanzania wote!
   
 2. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  haisee ni kweli hawa tbc wanaboa sana na wamesababisha watu wengi kuwa na chuki dhidi yao angalieni nyie tbc siku si nyingi mtajwa piga mawe
   
 3. I

  Isekuu Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata habari za upinzani hawaandiki, wamepangua utaratibu wote wa alio uacha bwana Tido kisa hakuipa shavu ccm wakati wa uchaguzi. Mambo yote yataenda safi ikiwa wananchi tutakua na nguvu ya pamoja. Na muda huo hauko mbali.
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Kama taarifa ya jana kwa kweli ilibore na kwa mtu aliyeangalia taarifa ya jana unajua kwa kweli kuna kitu gani TBC wanaficha maana ilinunukuu kabisa kuwa kuna mbunge wa chama cha upinzani ambaye alisababisha tafrani hiyo.Hawajaonyesha kabisa wala kuwahoji waathirika ni nini kilisababisha mpaka hayo yatokee.Wangewahoji wangeweza kupata taarifa ya nini kilisababisha ila taarifa wanazotumia ni za upande mmoja tuu wa Serikali kusema wale walikuwa wahalifu
   
 5. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TBC ni ya ccm si ya serikali ndiyo maana wanachakachua habari zote zinazohusu matokio yanayoweza kuwaadhiri.


   
 6. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nina hasira naoooo...
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Baada ya Tido TBC imekuwa inaboa kupita kiasi,sijui huyu Mshana kama atakuwa na jipya,kodi zetu zinapotea bure kabisa.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  SIoni umuhimu wa hiki kituo hasa ukichukulia kinaendeshwa na kodi za wa Tanzania
   
 9. h

  hans79 JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wapo kwenye kuandaa kumbukumbu za kitchen party,toka lin tv ya taifa na mambo hayo.wao jukumu lilitakiwa n taarifa za habar tu za sehemu mbalmbal,tatizo la nch n mfumo yaan polis,magereza,jwtz wote wauza mayai je?kaz za jesh watazifanya wakat gan?vijana tuamuke kuweka mfumo wa kaz za kila sekta.
   
 10. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  wao si wanafanya kazi kwa intersest za ccm,wanaripoti taarifa ya kagasheki ambaye hata huko hajafika,Lema ndio kaenda huko kuona halisi kama waziri kivuli mambo ya ndani kutoka kambi ya upinzani,wanatumia kodi zetu kufanya kazi za chama cha mapindunzi haki ya kupata habari ni ya kila mtanzania
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Siku zote unapotoa habari hakikisha unaweka usawa ili wananchi wajue kilichojiri na wawe waamuzi wazuri.Sasa TBC kazi yao ni kupendelea upande mmoja(kwa kutoa habari zinazoibeba Serikali ya ccm ambayo kila siku utendaji wake unashuka(mmbovu mno)Sikumbuki vizuri Ila yupo kiongozi mmoja wa Serikali alipohojiwa alisema kipo chama cha upinzani ndicho kilichochea vurugu zile ila hakukitaja(me nnaona wanaweweseka).Hivi kweli chama na viongozi wake kinaweza kuchochea wananchi wakavamie mgodi kweli?Kama sio mikataba mibovu iliyoingia Serikali na Wawekezaji ndio chanzo cha yote hayo ikiwa ni pamoja na Serikali kuziba masikio juu ya malalamiko ya wananchi wake.HAKUNA ASIEJUA CCM INAKUFA sasa kama ccm mnakufa kisiasa nnaomba msife na vyama vingine sbb nyinyi wenyewe ndio mmelikoroga(kushindwa uongozi bora),tuachieni Tanzania yetu
   
 12. m

  mafutamingi JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Mimi niliishaacha kutazama TBC muda mrefu. Nilikuwa mpenzi sana wa TBC enzi za Tido Mhando lakini tangu aondoke nilianza kuona mabadiliko katika vipindi vyake ambavyo sasa taarifa zake za habari siyo balanced. Fuateni nyayo zangu. Achana na TBC!
   
 13. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,978
  Likes Received: 20,359
  Trophy Points: 280
  Nafasi yao sasa inachukuliwa tena na ITV, balance yao ya habari anagalau unaweza kuivumilia na sio hawa TBC1, yaani ukiwaangalia mipesa wanayolipwa kwa mishahara unaweza ukadhani akili zao wanazitumia kwa faida ya wanaowalipa na haki kwao binafsi.
  Wao wanadhani ccm ndo wanaowalipa na ndiyo maana hata katibu wa ccm akicheka nayo inawekwa katika habari saa mbili nyambafu wakubwa hawa
   
 14. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wakubwa hii tbc si ya kuangalia kabisa,wanakwenda kwenye mikutano ya wakubwa na kuwanukuu bila kuhoji chochote hawana tofauti na uhuru fm siwapendi au nao tuwaite uhuru tv.jamani tuwapongeze itv kwani wameonesha live wakati mbunge anafika,anafukuzwa,unapigwa mawe msafara na pia wakawahoji wananchi.je hii ni tv ya kichaga?naomba waheshimiwa viongozi wa chadema mnijibu ni lini mtakuwa na vyombo vyenu vya habari,kama magazeti,redio na tv?tunapata shida kujua habari.big up.
   
 15. Tympa

  Tympa Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  TUANDAE MAANDAMANO YA KUPINGA UCHAKACHUAJI UNAOENDELEA TBC(vilevile tutake huyu mkurugenzi mpya ajiuzuru). IKISHINDIKANA KWA MAANDAMANO, TUTAANZA KUPIGA MAWE WAANDISHI WA TBC KILA WATAKAPOONEKANA.
   
 16. k

  kamimbi Senior Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole kaka kama ulikuwa hujui kama TBC ni ya ccm, kinachosikitisha ni pale inaendeshwa kwa pesa ya watz wavuja jasho, hiyo ndo Tz yetu bana au vp, but their days are numberd, time soon will tell.
   
 17. Josephine

  Josephine Verified User

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inayotoa vibari sasa ni CCM subiri ikifa tu vibari vya Chadema kupata vyombo vya habari vitapatikana.
   
 18. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  huyo ndo new CEO.Clemence Mgonja.
  mh! Tanzania jamani.........!
   
 19. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu mapendekezo yako yamejaa hekima: HAKI HUTAFUTWA, haiji kama mvua au hewa tunayopumua. Lazima tuwalazimishe kuwa chombo chetu, mimi binafsi nalipa zaidi ya milioni 15 (hapa sijajumlisha kodi zilizofichwa kama vile VAT na kodi zingine zilizofichwa) kwa mwaka kuchangia shughuli za serikali na ningependa kupata zaidi ... barabara mbovu, umeme haupatikani, hospitali hakuna dawa, hata habari sahihi nisipewe? I SAY NO!
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  TBC! wanapaswa kushitakiwa the Hague,TV ya taifa inachochea hasira za wananchi,unadhani wananchi wanafurahi kuitwa majambazi,au kuambiwa wamechochewa na Chadema au na Mbunge wa Arusha,au kwamba wanastaili kufa kwa sababu kudai kwao haki kulitokana na msukumo wa kisiasa haya ni matusi makubwa nadhani wanasheria na wataangalia uwezekano wa kuishitaki TBC! kwa kuchochea hasira za wananchi walio kwenye majonzi

  Bravo Channel Ten waliweza kuwaunganisha wananchi,serikali na wanasiasa kuweza kuelezea ukweli na wananchi tukapata ukweli
   
Loading...