TBC ifutwe, ni ufisadi mtupu

TBC ifutwe, ni ufisadi mtupu

binafsi siangalii tena TBC these days, uzuri hata familia yangu nao wamebaini inbalancing of story hawaipendi. kilichobaki sasa ni kwa vile wanaendeshwa kwa kodi yangu jinsi gani kudhibiti hilo, kodi yangui isitumike kwa manufaa ya ccm
 
tbc mbona ilishakwisha fariki, siamini kama bado ipo. tido alipoondoka yenyewe haikuchukua raundi
 
Hivi kweli nyie wapenda Tanzania na walilia maendeleo na wazalendo wa Tanzania mlitegemea TBC waseme nini mbele ya CCM ? TBC hawana hata miiko ya habari kuna waandishi ambao utadhani hawajasoma wanalishwa ujinga nao wanaitikia ni aibu sana . Dawa ni kuachana nao na kupiga kelele kodi zetu zisiende huko hakuna njia zaidi . Huwezi kuwaamini TBC ni CCM kwisha kazi
 
Ingekua ya mtu binafsi, simply ningesema nimeacha kuangalia vipindi vyake, ila inaniuma sana kuona kituo cha habari cha taifa kinatetea uovu wa serikali wanaoufanya dhidi ya wananchi, wakati wao wanalipwa na kodi zetu, hii INAUMA SANA.
 
Hakuna haja ya kuendelea kuangalia TBC hata kama unalipia kodi, kwani kufanya hivyo utakuwa unautesa moyo wako, njoo jamvini utahabarishwa na wanahabari wetu waliopo humu jamvini.
 
Tafuta Gazeti la RAI pamoja na kwamba linamilikiwa na fisadi, lakini wiki mbili zilizopita kulikuwa na makala inayoeleza kuwa watanzania TBC sio mali yetu bali ni mali ya serikali na kwamba kuna tofauti kati ya Public media na State Media. Sasa Tanzania tunatakiwa kuwa na Public media sio hii TBC ambayo ni State Media. Ukilipata hilo gazeti utaelewa zaidi tofauti ya makundi haya mawili ya media. Aibu TBC
 
Watanzania tusiisikilize,ni TV ya wahuni na ya MAFISADI
 
TBC imekuwa kama magazeti ya uhuru na mzalendo ambayo hayasomeki, leo nilikuwa na mfanyakazi mmoja wa TBC hotelini sasa wakati wa taarifa ya habari ameona mwenyewe maana tulihamia ITV akasema Tido tutamkumbuka daima. Amekiri mwenyewe kuwa yule mama wa sasa hivi wa ccm (I mean mtumwaji) hamna lolote kabisaaaaaa. Huyo alikuwa ni mfanyakazi wa TBC tena ni maarufu aliyasema hayo, na bado anafanya TBC for the sake of mshahara tu. otherwise wakipata kazi wataondoka.
 
Katika tukio la mauaji yaliyotokea Tarime (North Mara Mine) shirika la utangazaji la taifa limeonyesha mapungufu makubwa na kupoteza kabisa umuhimu wa kuwepo kwake, kwa siku mbili mfululizo wametoa kwenye taarifa zao za habari (prime time) za saa mbili kuhusu tukio hili lakini cha ajabu hakuna hata sehemu moja ambapo wamewapa fursa waathirika kueleza upande wao wa habari, kwa siku zote wamemnukuu Kagasheki na Kamanda wa polisi lakini hakuna sehemu yoyote ambapo wamewanukuu wanaotuhumiwa kuvamia mgodi ili nao watupe upande wao lakini hilo halijatokea.<br />
<br />
Kwa mtazamo wangu TBC imegeuka kuwa chombo cha wanasiasa walioko madarakani (CCM) na si cha watanzania kama ambavyo sababu za kuundwa kwake zinaeleza, kwa hiyo uendeshaji wa chombo hiki kuendelea kugharimiwa na watanzania wote ni <font color="red"><b>UFISADI</b></font>, ni bora basi CCM wakakichukua na kulipia uendeshaji wake kwa sababu kinaendeshwa kwa matakwa ya CCM siyo watanzania wote!
<br />
<br />
 
sasa unauhakika gan kama reporter alichukua matukio yote ambayo ww ungependa yaonyeshwe? Hali ya usalama nyamungo inatisha,hauwez kuwa huru ktk kufanya kitu chochote kwa ajili ya kuhofia usalama wako,ni vizuri mambo kama haya ukachangia kama una waled wa kutosha ktk jambo husika.
 
Hata habari za upinzani hawaandiki, wamepangua utaratibu wote wa alio uacha bwana Tido kisa hakuipa shavu ccm wakati wa uchaguzi. Mambo yote yataenda safi ikiwa wananchi tutakua na nguvu ya pamoja. Na muda huo hauko mbali.

Unafiki mtupu. Nyie ndiyo mliotaka kumpiga Marine Hassan Marine pale Jangwani na mkamshutumu sana Tido alipokatiza matangazo ya mkutano wa CDM mkidai anatumika na CCM. Leo Tido amegeuka kuwa malaika. Halafu aliyewaambia kwamba ni lazimi kila tukio lirushwe nani? Hivi ikiwa kila tukio litaripotiwa na hasa hii mizunguko ya CDM inayofanana na wakimbiza mwenge, basi watu watachoka maana hiyo ndo kazi ya chama hiki kwa miaka yote hii mpaka 2015 au mpaka pale watakapokuwa wametakasa mafisadi kiasi cha kuwafanya wameremete na kunukia.
 
sasa unauhakika gan kama reporter alichukua matukio yote ambayo ww ungependa yaonyeshwe? Hali ya usalama nyamungo inatisha,hauwez kuwa huru ktk kufanya kitu chochote kwa ajili ya kuhofia usalama wako,ni vizuri mambo kama haya ukachangia kama una waled wa kutosha ktk jambo husika.

Ndugu yangu unadhani wanaelewa hilo? Tuanapata nao shida hasa hawa jamaa!
 
Kama wanasoma humu salam ziwafikie kuwa watanzania hawapendi kuona mali zao zinachezewa na kikundi cha watu wachache.Ccm ni kikundi kidogo ktk jamii,wajue kwamba TBC ni chombo cha raia Million zaidi ya 40 wa tanzania ,wengine hawana vyama ,tumeshaanza kuikimbia kitakachofuata ni kudai Kodi zetu
 
Kama wanasoma humu salam ziwafikie kuwa watanzania hawapendi kuona mali zao zinachezewa na kikundi cha watu wachache.Ccm ni kikundi kidogo ktk jamii,wajue kwamba TBC ni chombo cha raia Million zaidi ya 40 wa tanzania ,wengine hawana vyama ,tumeshaanza kuikimbia kitakachofuata ni kudai Kodi zetu

Matumizi mazuri ni kufanya coverage mikutano na maandamano ya CDM? A big joke!
 
mi naipa Big up ITV kwani hata taarifa ya habari za kitaifa inachukua zaidi ya dakika 30 lakini ya TBC inachukua muda mchache sana kwa makusudi ili kutoa habari chache, sasa hii nchi ni kubwa na kama Tv ya taifa haitawataarif watu matukio yanayojiri wanategemea nani aripoti,TBC inakera sana hata vipindi vya live hawathubutu kuweka na kodi hawalipi wanang'ang'ania matangazo ya biashara tu, kumbe sirikali nayo inafanya biashara? Mi naona kwa vile Ze Comedy wanafadhiliwa na yule fisadi...... Na TBC nadhani wanafadhiliwa nae sio kodi zetu
 
Back
Top Bottom