Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,775
Salaam wana jamvi
Jana tarehe 23/03/2020 katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Kituo chetu pendwa cha TBC kilirusha taarifa nyingi kama ilivyo kawaida na ikafikia kwenye habari ya Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika matembezi ya jioni ndani ya Ikulu, jijini Dodoma.
Isivyo bahati ni kwamba, Rais alikua hakimbii na hata kama angekua anakimbia, mbona ulaya tunaona mashindano ya Formula One kwa njia ya video.
Lahaula Ya-rabb na roho yangu picha inatetemeka balaa na ubora wake haifanani na hata na iliyochukuliwa na mwanafunzi wa cheti anayesomea Video graphics.
Nimetatizwa na Kuanzia mhariri hadi mtu wa technical kuruhusu picha mbaya kiasi kile kurushwa hewani.
Mhe. Magufuli ameteua watu wenye elimu kubwa sana kuanzia maprofesa, Daktari wa shahada tatu, Wahandisi na madaktari wa shahada moja, bahati nzuri chombo hiki kinaongozwa na Daktari wa shahada tatu Ndugu Ayubu Riyoba, inatakiwa tuamini kwamba uwezo wake wa kuajiri watu wenye weledi ndio umeishia hapo?
Daktari Riyoba unakwama wapi kaka, huna hata mtu anayeweza kuchukua still picture na video vizuri?
Sent using Jamii Forums mobile app