TBC 1 habari hovyo hovyooo

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Clement Msahana ni kama ameshindwa kazi. Nafuatilia habari za TBC leo tarehe 13.03.12 saa mbili usiku, kuna habari ya wakazi wa Kibaha kurejea katika kijiji chao cha asili cHORUMA..lakini habari hiyo imeingiliana na masauti na mahabari mengine kibao..hakuna hata kumradhi wametoa kwa usumbufu huo..
 
hakuna siku imewahi kuwa nzuri
lazima kuwe na hitilafu katika mitambo
 
TBC ilishakufa baada ya Tido kuondoka, huyu Mshana anaizika tu sasa hivi
 
Halafu wananishangaza kwa kutounda vipindi vipya ila ni vupindi vifuatavyo wanavizungusha kuanzia saa nne asubuhi. Vipindi hivyo ni:
1. CASTLES OF CLAY - ni kipindi cha vichuguu na wanyama wanaopenda kuishi kwenye vichuguu.
2. ZIWA BABATI - Mambo ya mazingira kuhusiana na maisha kuzunguka ziwa babat mkoani manyara
3.HUNTERS - kipindi cha wanyama waishio baharini.
3. ZIWA GENDABE - Kipindi kinachohusu uvunaji wa chumvi kwenye ziwa Gendabi lililoko wilayani Hanang
4.GILBERT JOSAMU- Kisa cha bondia wa Zimbabwe aliyekufa kwa HIV.
5.RUAHA MDOGO NA MKUU- Mazingira ya mto Ruaha na pembezoni.

Kila siku lazimaTBC1 walete kimojawapo ya vipindi hapo juu. Usitarajie kipya tbc1 labda kama rais atahutubia taifa!
 
Clement Msahana ni kama ameshindwa kazi. Nafuatilia habari za TBC leo tarehe 13.03.12 saa mbili usiku, kuna habari ya wakazi wa Kibaha kurejea katika kijiji chao cha asili cHORUMA..lakini habari hiyo imeingiliana na masauti na mahabari mengine kibao..hakuna hata kumradhi wametoa kwa usumbufu huo..

Mi wameniuzi waliposhindwa kuonyesha Kombe la mataifa ya Africa, nafikiri Tido angekuwepo yasingetokea yote haya.
 
Tangu mwaka huu uanze kuna thread zaidi ya kumi zikilalamikia hawa TBC. Hii inaonyesha kuna tatizo kubwa pale...
 
Mara wameweka picha kwenye habari isiyohusika ili mradi tafrani tu.Ni aibu kuitwa televisheni ya taifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom