TBA waingia matatani kwa kutokamilisha miradi Kigoma

abackuk

Senior Member
Jan 6, 2014
193
187

Jafo aagiza watumishi TBA kukamatwa​

SATURDAY JANUARY 16 2021​

Summary

  • Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye kuwakamata na kuwekwa ndani viongozi na wasimamizi wa miradi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) mkoani humo kwa kuchukua fedha za miradi na kushindwa kuitekeleza.
By Happiness Tesha(Mwananchi)

Uvinza. Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye kuwakamata na kuwekwa ndani viongozi na wasimamizi wa miradi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) mkoani humo kwa kuchukua fedha za miradi na kushindwa kuitekeleza.

Jafo ametoa agizo hilo leo Jumamosi Januari 16, 2021 wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati akikagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo nyumba ya mkuu wa Wilaya Uvinza, za watumishi na hospitali ya wilaya hiyo.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kupokea taarifa kuwa TBA imepewa Sh500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya huyo miaka mitano iliyopita lakini hadi leo umejengwa msingi pekee.

Waziri huyo pia alikerwa na kusuasua kwa miaka mitatu kwa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya wilaya hiyo linalogharimu Sh900 milioni.

"Nataka kuorodheshewa miradi yote iliyokwama kwa mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa inatekelezwa na TBA, nielezwe thamani ya kazi iliyofanyika na kiasi cha fedha kilichotolewa na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwangu mara moja ili niweze kuifanyia kazi," amesema Jafo.

Awali, akitoa taarifa kwa Jafo meneja wa miradi ya ujenzi Mkoa wa Kigoma, Masawika Kachenje amesema miradi hiyo ilianza mwaka 2013 na ilipaswa kukamilika 2018

"Utekelezaji umekuwa mgumu kwa sababu fedha zimeenda TBA makao makuu na huku kwenye miradi fedha hazipelekwi na hivyo miradi umekwama, tumeshavunja mikataba yote na tumewaandikia barua tangu mwaka 2019 fedha zirudishwe lakini hadi sasa hakuna utekelezaji uliofanyika," amesema Machenje.

Maendeleo hayana vyama!
 
Na Editha Karlo, Uvinza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI), Seleman Jafo ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani kwa viongozi na wasimamizi wa miradi wa wakala wa majengo nchini (TBA) Mkoa Kigoma kwa kushindwa kukamilisha miradi ya ujenzi waliyopewa huku wakichukua kiasi kikubwa cha pesa.

72a3bcfd-a3a6-4c16-8663-46a437273892-1024x461.jpg

Jengo la Utawala la halmashauri ya wilaya Uvinza ambalo limekwama huku TBA wakiwa wamepokea milioni 900
Jafo ametoa agizo hilo leo Jumamosi Januari 16, kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Kigoma

Akiwa kwenye ziara ya kukagua majengo ya Utawala ya viongozi na watumishi walio chini ya wizara hiyo wilayani Uvinza Jafo amekerwa na taarifa ya ujenzi wa majengo hayo.
Waziri Jafo ameeleza kukerwa na taarifa ya TBA kupewa kiasi cha Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza miaka mitano iliyopita ambapo hadi sasa nyumba hiyo imefikia usawa wa msingi.

Aidha, Jafo ameonyesha kukerwa kutokana na kukwama jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Uvinza ambapo kiasi cha Sh milioni 900 kimetolewa lakini mradi umekwama kwa miaka zaidi ya mitatu na kwa sasa ujenzi upo usawa wa madirisha.

Awali, akitoa taarifa kwa Waziri, Meneja wa miradi ya ujenzi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Masawika Kachenje amesema miradi hiyo ilianza mwaka 2013 na ilipaswa kukamilika mwaka 2018 na waliomba pesa kwenye miradi hiyo kama malipo ya awali.

93735ebf-a1f1-49b2-8bf1-39e96baabbb8-1024x461.jpg

Jengo la nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza ambalo limekwama tangu mwaka 2013 licha ya watekelezaji wa mradi wakala wa majengo (TBA) kupokea milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo

Kachenje amesema pesa kwenye miradi hiyo zimeingizwa kwenye akaunti ya TBA makao makuu lakini taarifa zinaonyesha kuwa pesa hizo hazipelekwi kwenye miradi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amemweleza Waziri Jafo kuwa analazimika kuishi kwenye kontena zilizoachwa na mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami wa Kidahwe hadi Uvinza kutokana na kukwama kwa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa wilaya.

Mrindoko amesema kuwa wamefanya jitihada kuhakikisha TBA wanarejesha fedha lakini hakuna jitihada iliyofanyika.

Kutokana na hali hiyo Jafo ameagiza kuorodheshwa kwa miradi yote iliyokwama kwa mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa inatekelezwa na TBA, kueleza thamani ya kazi iliyofanyika na kiasi cha pesa kilichopelekwa na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwake aweze kuifanyia kazi.
 
Inasikitisha kwa Kiongozi wa nchi kuishi katika kontena.
Inakatisha tamaa hata utendaji ukiachia mbali utu.

Wacha Serikali mjihukumu wenyewe maana ni wakaidi kuelewa misingi ya ujenzi.
Mara TBA watajenga, mara JKT SUMA, mara Force Account.
Makandarasi wanawatazama tu mkijikoroga.
Mtajiju.
 
Serikali imara ni ile yenye viongozi walio tayari kuona makosa yao na ya watendaji wao na kuwajibika
Pongezi kwa mheshimiwa Jafo💥
Viva Rais John Pombe Magufuli 👍
 
Na Editha Karlo, Uvinza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI), Seleman Jafo ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani kwa viongozi na wasimamizi wa miradi wa wakala wa majengo nchini (TBA) Mkoa Kigoma kwa kushindwa kukamilisha miradi ya ujenzi waliyopewa huku wakichukua kiasi kikubwa cha pesa.

72a3bcfd-a3a6-4c16-8663-46a437273892-1024x461.jpg

Jengo la Utawala la halmashauri ya wilaya Uvinza ambalo limekwama huku TBA wakiwa wamepokea milioni 900
Jafo ametoa agizo hilo leo Jumamosi Januari 16, kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Kigoma

Akiwa kwenye ziara ya kukagua majengo ya Utawala ya viongozi na watumishi walio chini ya wizara hiyo wilayani Uvinza Jafo amekerwa na taarifa ya ujenzi wa majengo hayo.
Waziri Jafo ameeleza kukerwa na taarifa ya TBA kupewa kiasi cha Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza miaka mitano iliyopita ambapo hadi sasa nyumba hiyo imefikia usawa wa msingi.

Aidha, Jafo ameonyesha kukerwa kutokana na kukwama jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Uvinza ambapo kiasi cha Sh milioni 900 kimetolewa lakini mradi umekwama kwa miaka zaidi ya mitatu na kwa sasa ujenzi upo usawa wa madirisha.

Awali, akitoa taarifa kwa Waziri, Meneja wa miradi ya ujenzi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Masawika Kachenje amesema miradi hiyo ilianza mwaka 2013 na ilipaswa kukamilika mwaka 2018 na waliomba pesa kwenye miradi hiyo kama malipo ya awali.

93735ebf-a1f1-49b2-8bf1-39e96baabbb8-1024x461.jpg

Jengo la nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza ambalo limekwama tangu mwaka 2013 licha ya watekelezaji wa mradi wakala wa majengo (TBA) kupokea milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo

Kachenje amesema pesa kwenye miradi hiyo zimeingizwa kwenye akaunti ya TBA makao makuu lakini taarifa zinaonyesha kuwa pesa hizo hazipelekwi kwenye miradi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amemweleza Waziri Jafo kuwa analazimika kuishi kwenye kontena zilizoachwa na mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami wa Kidahwe hadi Uvinza kutokana na kukwama kwa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa wilaya.

Mrindoko amesema kuwa wamefanya jitihada kuhakikisha TBA wanarejesha fedha lakini hakuna jitihada iliyofanyika.

Kutokana na hali hiyo Jafo ameagiza kuorodheshwa kwa miradi yote iliyokwama kwa mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa inatekelezwa na TBA, kueleza thamani ya kazi iliyofanyika na kiasi cha pesa kilichopelekwa na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwake aweze kuifanyia kazi.
TBA wanapewa chakula kingi mno kiasi wanashindwa kumudu kutafuna na kumeza. Kuna ubaya haya mambo ya ujenzi km huo waka outsource wakapewa watu wenye uwezo na nafasi kuliko kuwarundikia TBA kazi nyingi ili hali hawana uwezo wa kuzimudu zote ipasavyo?
 
TBA na SUMA JKT wamepewa miradi mingi ya ujenzi na mingi wanashindwa kuikamilisha.

Wapeni sekta binafsi hiyo miradi.
Kwa kifupi TBA na SUMA JKT wamezidiwa au hawana uwezo ku implement miradi waliyo contract.

In 10 years to come zitaibuka kesi nyingi kwa TBA na SUMA JKT wasipojipanga na kukamilisha miradi sawa na contract walizoingia.
 
"milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza miaka mitano iliyopita"

Nataka nipate kazi huko TBA na mimi nile mema ya nchi.
Mitadi mingi TBA anafanya consultancy, lkn ndo anapigwa mijihela hiyo.

TBA ni kichaka fulani na nahisi kuna jambo hidden lipo kwa consultancy hizo.... ni kamrija fulani kwa watu fulani nasema tu lkn!!!
 
Jamani hivi nyumba ya mtumishi wa umma kugharimu milioni 500 ni jambo la kawaida hili?

Hii inamaanisha vijana tusitarajie kujenga au?
 
Back
Top Bottom