TBA wabania ujenzi wa chuo Mbeya

TBA wabania ujenzi wa chuo Mbeya

Ozzie

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Posts
3,217
Reaction score
1,274
Kuna taarifa kuwa mkuu wa Tanzania Building Agency mkoani Mbeya, hataki kutoa kibali cha ujenzi mkubwa wa chuo cha madaktari wasaidizi jijini Mbeya.
Taarifa zaidi zinadai kuwa mwanzoni chuo hiki kilitakiwa kupanuliwa na wizara ya afya kwa kutumia pesa toka Global Fund. Ujenzi huu ungehusisha pia manunuzi ya thamani. Bahati mbaya, pesa toka Global Fund zikatafunwa na wajanja wa wizara hivyo Global Fund wakaamua kujitoa.
Center for Disease Control and Prevention (CDC), Marekani, ikaamua kuufadhili mradi wa ujenzi uliotaka kufadhiliwa na Global Fund kwa sharti la kutonunua thamani na pia kufanya consultancy zote zihusianazo na ujenzi wao wenyewe. Wizara ya Afya haikuwa na kipingamizi.
Awali wizara ya afya ilipoomba kibali cha kutumia eneo la serikali kufanya upanuzi huu mkubwa kwa kutumia pesa za CDC, TBA Mbeya ilikubali kwa sharti kuwa wao watafanya consultancy. TBA ilipojua CDC itatumia consultants wake, ikaamua kuwaandikia wizara ya afya kwamba serikali ina matumizi mengine na hicho kiwanja. Taarifa zinadai viongozi wa wizara ya afya hadi katibu mkuu wameshindwa kukubaliana na TBA. Kwa sasa waziri wa afya na wa ujenzi ndio wanategemewa kuokoa jahazi.
 
Back
Top Bottom