TBA Ukandarasi unawatokea puani!

TBA Ukandarasi unawatokea puani!

“Huu ni ufisadi, Meneja huna kazi” -Waziri Ndalichako via YouTube

Huyu Prof sijui taaluma yake ni ipi?

Kafika Mloganzila anaanza kujifanya Mjuaji analaumu kuwa Vibarua 40 ni wachache hawatoshi waongezwe kazi iende haraka, hajui kuwa wale wanalipwa na labor charges yao ni sehemu ya Budget

ukiongoza vibarua kwa maelekezo ya Waziri nani atalipia extra cost?
 
Pamoja na kupingwa sana uamuzi wa Serikali kuwapa kazi zote za serikali TBA, sasa madudu ya kutisha yanajitokeza.

Tukumbuke kuwa TBA Tanzania Buildings Agency, ni wakala wa nyumba za serikali.
Uanzishwaji wake huko nyuma ilikuwa ku manage matumizi ya nyumba za serikali chini ya Wizara ya Ujenzi.
Sitaongelea sakata la uuzwaji wa nyumba za serikali maana hilo ni dudu tosha.

Baada ya nyumba nyingi kuuzwa TBA sasa wakapewa jukumu la kujenga nyingine kwa watumishi na ofisi za serikali..

Leo , TBA wamegeuka kuwa kandarasi, na kupewa kazi nchi nzima.

Ukandarasi ni biashara nyeti ya kitaalam, na msukumo wa wanaoifanya biashara hiyo ni faida na ukamilishaji kazi vizuri na kujenga jina, ili siku nyingine wapewe kazi .

Siyo siri TBA hawana management capacity ya kuendesha miradi mingi, mikubwa tena kwa mpigo.

-Sasa tumemsikia waziri Ndalichako akiwalalamikia TBA, mradi wa bilioni13 Mlonganzila, Chuo Kikuu Muhimbili,

-Waziri Mkuu alilalamikia mradi wa bilioni 3, Ofisi za Halmasphauri Butiama, kiSi cha kufikia TAKUKURU wamshughulikie meneja wa TBA.

-Chuo Kikuu cha DSM, na "expansion joints" zake sinahaja ya kurudia hayo madudu.

-Mradi wa bilioni 10 nyumba za Magereza Ukonga unasuasua.

Mifano ni mingi sana.

Unapomgeuza wakala TBA kuwa mkandarasi, hivi tulitegemea nini?

Makandarasi wa serikali kama MECCO na SUMA JKT, wameshindwa kwa vile uanzishwaji wao hauko kibiashara.

Tunakumbuka machinjio ya Ruvu na mradi wa barabara Msata Bagamoyo(TAKOPA) vilivyoishia hewani.
MECCO ndio ilikufa na kuuzwa kabisa.

Serikali ya Rais Magufuli iutazame upya uamuzi wa kuifanya wakala TBA kuwa mkandarasi, anasivyo hasara juu ya hasara hazikwepeki.
Na kuwaweka ndani watumishi wa TBA si suluhisho la nyumba kujengwa kwa weledi. Viongozi wetu hapa sana sana wanaficha aibu zao kwa kuwa walifanya maamuzi yasiyo na tija katika sekta ya ujenzi, kwa kugeuza wakala TBA kuwa mkandarasi.
bado temesa
 
bado temesa

Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency (TEMESA)

What We Do

The functions of the Agency are as follows:

(i) Undertake an effective maintenance of Government Owned Motor vehicles, motor cycles and Plants;

(ii) Undertake an effective maintenance of Electrical, Electronics/ICTs, Air Conditioning and Refrigeration systems in all Government Buildings;

(iii) Operation and maintenance of Traffic Signals and Street Lights;

(iv) Hiring of transport for Government VIPs;

(v) Hiring of Plants and Equipment to Government Institutions and the Public at large;

(vi) Ensure safe operation and maintenance of all Government Owned Ferry Services;

(vii) Provision of quality Technical Advice and Consultancy services in Engineering Works and related services to Government institutions and the Public at large;

(viii) Provision of quality Technical Advice and Consultancy services on new installations related to Engineering Works and Services;

(ix) Design and supervise new installations related to Engineering Works and Services.

Home | TEMESA
Hawa lazima waende na maji pia...wachafu mno...
 
Mkuu hapa tunaongelea TBA, ingawaje kuna mtindo sasa kugeuza Wakala wa serikali kuwa kandarasi.
 
Mkuu hapa tunaongelea TBA, ingawaje kuna mtindo sasa kugeuza Wakala wa serikali kuwa kandarasi.
Kuna Siku Tanroads watajenga barabara na Rahco wanaanza kuchomeka mataluma ya reli na Ewura wataanza kuendesha petrol station
 
Wale wanafunzi wa yale mabweni lazima watakaa kwa wasiwasi sana maana ukweli umejulikana. Ilikuwa swala la muda tu, hakuna cha expansion joints wala nn, dude bovu ikitokea earthquake wajiandae kisaikolojia
 
Naona huyo Mkurugenzi naye kaamua kujiripua. Hayo alipaswa kwenda kuyaeleza kwa Waziri Mkuu ana kwa ana wala siyo kumweleza kupitia magazeti.
Kama mbwai na iwe mbwai tu kwani nini Bwana watu tumechoka kuonewa.
 
Tatizo kubwa la TBA ni lack of professionalism. Wataalamu wanasema kabisa jengo litagharimu bilioni 40, TBA huko watokako wanatuhakikishia kuwa watajenga kwa bilioni 10. Of course tenda wanapewa, ukweli ukidhihirika mbele ya safari visingizio vinaanza. Hawa mameneja kwenye site wanajua ukweli. Gharama za kukarabati majengo ni kubwa sana. Meneja akiomba bilioni 4 anaambiwa bilioni 1 inatosha halafu anapewa milioni 400 za mwanzo. Zitatosha nini kwenye ukarabati wa shule za zamani kama Malangali nk.?
Mkuu hapo Malangali umenikumbusha mengi sana aisee! Nimebukua hapo miaka mingi iliyopita.
 
Serikali ya CCM hua haijifunzi kutokana na makosa. Wangesema wanatoa upendeleo kwa makandarasi wazawa wenye uwezo ningewaelewa, lakini kutoa upendeleo kwa TBA ni mawazo ya kijima kabisa
 
Kuna Siku Tanroads watajenga barabara na Rahco wanaanza kuchomeka mataluma ya reli na Ewura wataanza kuendesha petrol station
Exactly, that's my point mkuu!
Badala ya ku think through a project, sasa TBA wanafanya wenyewe, wakati hawako equipped managerially, na hata kwa set up kuwa kampuni ya kikandarasi.
Wameokoa fedha kama pale Hostel za Mlimani hatukatai, lakini si tumeziona "expansion joints" za kutisha?
Maintainance costs lazima zitakuwa kubwa mno!
 
Hata mimi siungi Mkono Serikali kujiendesha kijamaa kwa kujipa kandarasi za Ujenzi lakin kuwalaumu moja kwa moja kwa ucheleweshaji wa ujenzi sio sahihi kwa kuwa nimesoma hoja za Mtendaji Mkuu wa TBA kwenye Mwananchi ya leo nimemuelewa.

kwenye ujenzi wa chini ya kiwango kama Hostel za UDSM kwa kweli sina cha kuwatetea ni kweli walivurunda lakin wanasiasa kuficha madhaifu yao kwa kuwalaumu TBA kwa ucheleweshaji ni kujikosha kisiasa.

Mtendaji Mkuu yule anamshangaa Waziri Mkuu kwa kuamuru kukamatwa kwa Meneja wa TBA kule Mara kwa ucheleweshaji wa Mradi, anasema kwenye Mkataba walioingia kuna kipengele kinazungumzia nini cha kufanya ikiwa huridhishwi na mwenza wako wa mradi, na kipengele hicho hakijasema Msimamizi wa Mradi akamatwe na TAKUKURU, anasema mradi wa 3 Billion zimepelekwa 600 Million pekee na wamekamilisha kazi ya 400 million kweli hapo kuna ucheleweshaji?

akizungumzia ucheleweshaji wa ukarabati wa shule kongwe anasema kazi ya kutathmini gharama za Ujenzi walipewa Ardhi University ambao estimate zao zilikuwa unrealistic hivyo ikabidi zirudiwe na wakamjulisha kwa Maandishi Client wao ( Wizara ya elimu) kuhusu jambo hilo na wakakubaliana kwa maandishi extention ya muda wa mradi lakin ghafla Prof Ndalichako anakwenda kuwaropokea wamechelewa

akizungumzia ya Mloganzila anasema waliambiwa wajenge hostel ya ku accomodate wanafunzi elf 10 na walipoanza ujenzi wakaletewa marekebisho iwe wanafunzi elf 1 pekee hivyo ukawabidi waanze upya lakin yote hayo ni ndani ya miezi mitatu ya awali kati ya Miezi 15 ya mradi lakin wanasiasa bado wanwalaumu, so Wanasiasa waache kuwabebesha lawama TBA kwa maamuzi yao mabovu
Kama kaongea hivyo kaamua kujilipua! Lakini kafanya vizuri kwani tumejua upande wa pili wa story
 
Mecco iliisha kwa kushauriwa vibaya raisi aliyekuwepo madarakani wakati huo sababu mkurugenzi mkuu alikataa kutoa fedha kugharimia mtoto wa mjumbe wa bodi kwenda ulaya ikaua shirika zima
 
Back
Top Bottom