TBA Ukandarasi unawatokea puani!

TBA Ukandarasi unawatokea puani!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,511
Reaction score
30,666
Pamoja na kupingwa sana uamuzi wa Serikali kuwapa kazi zote za serikali TBA, sasa madudu ya kutisha yanajitokeza.

Tukumbuke kuwa TBA Tanzania Buildings Agency, ni wakala wa nyumba za serikali.
Uanzishwaji wake huko nyuma ilikuwa ku manage matumizi ya nyumba za serikali chini ya Wizara ya Ujenzi.
Sitaongelea sakata la uuzwaji wa nyumba za serikali maana hilo ni dudu tosha.

Baada ya nyumba nyingi kuuzwa TBA sasa wakapewa jukumu la kujenga nyingine kwa watumishi na ofisi za serikali..

Leo , TBA wamegeuka kuwa kandarasi, na kupewa kazi nchi nzima.

Ukandarasi ni biashara nyeti ya kitaalam, na msukumo wa wanaoifanya biashara hiyo ni faida na ukamilishaji kazi vizuri na kujenga jina, ili siku nyingine wapewe kazi .

Siyo siri TBA hawana management capacity ya kuendesha miradi mingi, mikubwa tena kwa mpigo.

-Sasa tumemsikia waziri Ndalichako akiwalalamikia TBA, mradi wa bilioni13 Mlonganzila, Chuo Kikuu Muhimbili,

-Waziri Mkuu alilalamikia mradi wa bilioni 3, Ofisi za Halmasphauri Butiama, kiSi cha kufikia TAKUKURU wamshughulikie meneja wa TBA.

-Chuo Kikuu cha DSM, na "expansion joints" zake sinahaja ya kurudia hayo madudu.

-Mradi wa bilioni 10 nyumba za Magereza Ukonga unasuasua.

Mifano ni mingi sana.

Unapomgeuza wakala TBA kuwa mkandarasi, hivi tulitegemea nini?

Makandarasi wa serikali kama MECCO na SUMA JKT, wameshindwa kwa vile uanzishwaji wao hauko kibiashara.

Tunakumbuka machinjio ya Ruvu na mradi wa barabara Msata Bagamoyo(TAKOPA) vilivyoishia hewani.
MECCO ndio ilikufa na kuuzwa kabisa.

Serikali ya Rais Magufuli iutazame upya uamuzi wa kuifanya wakala TBA kuwa mkandarasi, anasivyo hasara juu ya hasara hazikwepeki.
Na kuwaweka ndani watumishi wa TBA si suluhisho la nyumba kujengwa kwa weledi. Viongozi wetu hapa sana sana wanaficha aibu zao kwa kuwa walifanya maamuzi yasiyo na tija katika sekta ya ujenzi, kwa kugeuza wakala TBA kuwa mkandarasi.
 
Hata mtoto wako unayempendelea sana kuzidi watoto wengine ujue tu unamharibu maana atafika mahali ataanza jeuri, kiburi na madharau, hiyo ni kanuni ya asili ndiyo maana wenzetu waliweka taratibu za tenda kwenye manunuzi, sasa mwenzetu huyu yeye kaamua kuanza upya tafiti ili kuprove kama wako sahihi, kwa hiyo tutegemee hasara nyingi sana siku za usoni
 
Pamoja na kupingwa sana uamuzi wa Serikali kuwapa kazi zote za serikali TBA, sasa madudu ya kutisha yanajitokeza.

Tukumbuke kuwa TBA Tanzania Buildings Agency, ni wakala wa nyumba za serikali.
Uanzishwaji wake huko nyuma ilikuwa ku manage matumizi ya nyumba za serikali chini ya Wizara ya Ujenzi.
Sitaongelea sakata la uuzwaji wa nyumba za serikali maana hilo ni dudu tosha.

Baada ya nyumba nyingi kuuzwa TBA sasa wakapewa jukumu la kujenga nyingine kwa watumishi na ofisi za serikali..

Leo , TBA wamegeuka kuwa kandarasi, na kupewa kazi nchi nzima.

Ukandarasi ni biashara nyeti ya kitaalam, na msukumo wa wanaoifanya biashara hiyo ni faida na ukamilishaji kazi vizuri na kujenga jina, ili siku nyingine wapewe kazi .

Siyo siri TBA hawana management capacity ya kuendesha miradi mingi, mikubwa tena kwa mpigo.

-Sasa tumemsikia waziri Ndalichako akiwalalamikia TBA, mradi wa bilioni13 Mlonganzila, Chuo Kikuu Muhimbili,

-Waziri Mkuu alilalamikia mradi wa bilioni 3, Ofisi za Halmasphauri Butiama, kiSi cha kufikia TAKUKURU wamshughulikie meneja wa TBA.

-Chuo Kikuu cha DSM, na "expansion joints" zake sinahaja ya kurudia hayo madudu.

-Mradi wa bilioni 10 nyumba za Magereza Ukonga unasuasua.

Mifano ni mingi sana.

Unapomgeuza wakala TBA kuwa mkandarasi, hivi tulitegemea nini?

Makandarasi wa serikali kama MECCO na SUMA JKT, wameshindwa kwa vile uanzishwaji wao hauko kibiashara.

Tunakumbuka machinjio ya Ruvu na mradi wa barabara Msata Bagamoyo(TAKOPA) vilivyoishia hewani.
MECCO ndio ilikufa na kuuzwa kabisa.

Serikali ya Rais Magufuli iutazame upya uamuzi wa kuifanya wakala TBA kuwa mkandarasi, anasivyo hasara juu ya hasara hazikwepeki.
Na kuwaweka ndani watumishi wa TBA si suluhisho la nyumba kujengwa kwa weledi. Viongozi wetu hapa sana sana wanaficha aibu zao kwa kuwa walifanya maamuzi yasiyo na tija katika sekta ya ujenzi, kwa kugeuza wakala TBA kuwa mkandarasi.
Kwapa wakala biashara ngumu ya ukandarasi is trying to re-invent the wheel!
Kweli MECCO walishindwa na kuuzwa, kuna mashirika vile vile ya kiserikali katika sekta ya ujenzi kama NEDCO hata NHC , yote tumena performance zao zikiishia.
Tujifunze!
 
Sina hakika kama shirika la nyumba walikuwa wanajenga wenyewe niliwahi kutembelea ujenzi wa nyumba za kigamboni enzi hizo,kuna jamaa walikuwa wamepewa tenda,NHC yeye ni kama msimamizi tuu
 
Hata mimi siungi Mkono Serikali kujiendesha kijamaa kwa kujipa kandarasi za Ujenzi lakin kuwalaumu moja kwa moja kwa ucheleweshaji wa ujenzi sio sahihi kwa kuwa nimesoma hoja za Mtendaji Mkuu wa TBA kwenye Mwananchi ya leo nimemuelewa.

kwenye ujenzi wa chini ya kiwango kama Hostel za UDSM kwa kweli sina cha kuwatetea ni kweli walivurunda lakin wanasiasa kuficha madhaifu yao kwa kuwalaumu TBA kwa ucheleweshaji ni kujikosha kisiasa.

Mtendaji Mkuu yule anamshangaa Waziri Mkuu kwa kuamuru kukamatwa kwa Meneja wa TBA kule Mara kwa ucheleweshaji wa Mradi, anasema kwenye Mkataba walioingia kuna kipengele kinazungumzia nini cha kufanya ikiwa huridhishwi na mwenza wako wa mradi, na kipengele hicho hakijasema Msimamizi wa Mradi akamatwe na TAKUKURU, anasema mradi wa 3 Billion zimepelekwa 600 Million pekee na wamekamilisha kazi ya 400 million kweli hapo kuna ucheleweshaji?

akizungumzia ucheleweshaji wa ukarabati wa shule kongwe anasema kazi ya kutathmini gharama za Ujenzi walipewa Ardhi University ambao estimate zao zilikuwa unrealistic hivyo ikabidi zirudiwe na wakamjulisha kwa Maandishi Client wao ( Wizara ya elimu) kuhusu jambo hilo na wakakubaliana kwa maandishi extention ya muda wa mradi lakin ghafla Prof Ndalichako anakwenda kuwaropokea wamechelewa

akizungumzia ya Mloganzila anasema waliambiwa wajenge hostel ya ku accomodate wanafunzi elf 10 na walipoanza ujenzi wakaletewa marekebisho iwe wanafunzi elf 1 pekee hivyo ukawabidi waanze upya lakin yote hayo ni ndani ya miezi mitatu ya awali kati ya Miezi 15 ya mradi lakin wanasiasa bado wanwalaumu, so Wanasiasa waache kuwabebesha lawama TBA kwa maamuzi yao mabovu
 
Nimekuelewa.asante
 
Bila kumung'unya maneno, kumpeleka TAKUKURU mtendaji au mjenzi ambaye kazi yake wal haijakamilika ni matumizi mabaya ya madaraka.
 
Ndio maana wanasema usihukumu kwa kusikiliza upande mmoja.

Wanasiasa sio watu wazuri kabisa.
 
Naona huyo Mkurugenzi naye kaamua kujiripua. Hayo alipaswa kwenda kuyaeleza kwa Waziri Mkuu ana kwa ana wala siyo kumweleza kupitia magazeti.
 
Naona huyo Mkurugenzi naye kaamua kujiripua? Hayo alipaswa kwenda kuyaeleza kwa Waziri Mkuu ana kwa ana wala siyo kumweleza kupitia magazeti.
Tatizo hapa ni viongozi wengi kutaka kuendesha mambo wanavyotaka wao viwe.

Sekta ya ujenzi ina miiko yake na taratibu zake.
Watu wengi na hata viongozi wanafikiri ukimpata mkandarasi basi jengo limesimama.

Hawaelewi kuwa katika ujenzi kuna tarstibu muhimu sana za upembuzi, usanifu, ukadiriaji gharama, utafutaji wa mkandarasi mwenye vigezo, na mwisho ujenzi na usimamizi.

Napata shida kuamini kama TBA wanazo sifa za kutekeleza miradi ya mabilioni, uzoefu huo hawana.
Kumweka ndani mtumishi ni kujiondoa toka uhalisia wa tatizo.

Tujifunze tulipokosea.
 
Naona huyo Mkurugenzi naye kaamua kujiripua. Hayo alipaswa kwenda kuyaeleza kwa Waziri Mkuu ana kwa ana wala siyo kumweleza kupitia magazeti.
Waziri mkuu angeelezwa haya ana kwa ana angepingana na ukweli na kutafuta namna ya kujisafisha mbele ya kadamnasi, bora kaeleza kwa uwazi na uzuri kasema kabisa taarifa walitoa tena kwa maandishi.
Ni vema wanasiasa wakapunguza mihemko na kuacha kutoa maamuzi as if wamekurupushwa. Ethics za uongozi hakuna tena ni maonesho ya kipumbavu, kijuha, kizwazwa na kishenzi ndo yametawala. Tunachotaka kuona ni miradi imesimama mengine yote wasolve ndani ya ofisi sio kwenye vyombo vya habari.
 
Sina hakika kama shirika la nyumba walikuwa wanajenga wenyewe niliwahi kutembelea ujenzi wa nyumba za kigamboni enzi hizo,kuna jamaa walikuwa wamepewa tenda,NHC yeye ni kama msimamizi tuu
Pengine we bado ni kijana mdogo.
1965 nyumba zote za pale Keko, mtaa wa Majimaji pamoja na maghorofa yake(upande mwingine wanakaa wanajeshi), nyumba nyingi Wailesi, Magomeni na Mwanayamala , Kinondoni-zilijengwa na NHC, National Housing na Kampuni yake ya TACONA(Tanzania Conrete Articles).
TACONA ilikufa, NHC ilikuwa inaelekea kufa mpaka uongozi mwingine ulivyoingia miaka michache iliyopita na kuligeuza kwa kukopa fedha nyingi mabenkini..
 
Waziri mkuu angeelezwa haya ana kwa ana angepingana na ukweli na kutafuta namna ya kujisafisha mbele ya kadamnasi, bora kaeleza kwa uwazi na uzuri kasema kabisa taarifa walitoa tena kwa maandishi.
Ni vema wanasiasa wakapunguza mihemko na kuacha kutoa maamuzi as if wamekurupushwa. Ethics za uongozi hakuna tena ni maonesho ya kipumbavu, kijuha, kizwazwa na kishenzi ndo yametawala. Tunachotaka kuona ni miradi imesimama mengine yote wasolve ndani ya ofisi sio kwenye vyombo vya habari.
Ajiandae kupigwa kofi na wajakazi na kuulizwa "unamjibu hivyo waziri mkuu?" Kwa maneno mengine ajiandae kutumbuliwa.
 
Waziri mkuu angeelezwa haya ana kwa ana angepingana na ukweli na kutafuta namna ya kujisafisha mbele ya kadamnasi, bora kaeleza kwa uwazi na uzuri kasema kabisa taarifa walitoa tena kwa maandishi.
Ni vema wanasiasa wakapunguza mihemko na kuacha kutoa maamuzi as if wamekurupushwa. Ethics za uongozi hakuna tena ni maonesho ya kipumbavu, kijuha, kizwazwa na kishenzi ndo yametawala. Tunachotaka kuona ni miradi imesimama mengine yote wasolve ndani ya ofisi sio kwenye vyombo vya habari.
Ni kweli, inawezekana Waziri Mkuu kaingizwa chaka na maneno ya kuambiwa.
Lakini hii haiondoi ukweli kuwa TBA wamebambikwa miradi mini ya gharama kubwa wakati uwezo wao ni mdogo.
Na taratibu za kumpata mkandarasi huyo TBA haikidhi matakwa ya mradi husika.
Hapa funzo ni wamba huwezi ukamwamrisha TBA kuwa kesho nataka jingo A liwe limekamilika, na likakamilika.
Ujenzi una taratibu zake, zege yenyewe huchukua siku 28 kukomaa, ukiamrisha nataka iwe imekamilika siku 10, utaishia hasara.
 
Mkurugenzi wa TBA ni washkaji sana na bwana
Yule.....

Ova
 
Tatizo kubwa la TBA ni lack of professionalism. Wataalamu wanasema kabisa jengo litagharimu bilioni 40, TBA huko watokako wanatuhakikishia kuwa watajenga kwa bilioni 10. Of course tenda wanapewa, ukweli ukidhihirika mbele ya safari visingizio vinaanza. Hawa mameneja kwenye site wanajua ukweli. Gharama za kukarabati majengo ni kubwa sana. Meneja akiomba bilioni 4 anaambiwa bilioni 1 inatosha halafu anapewa milioni 400 za mwanzo. Zitatosha nini kwenye ukarabati wa shule za zamani kama Malangali nk.?
 
Pamoja na kwamba walikuwa mawakala na kugeuzwa kuwa wakandarasi, bado sielewi kwanini TBA wanashindwa kupiga kazi! Mtaani kuna ma-engineers na wajenzi lukuki wanatafuta kazi, tatizo letu bado lile lile, kufanya kazi kwa mazoea, kufikiria wizi na ufisadi katika kila tenders...
Ukiweka watu wa uhakika pale, TBA inaweza kufanya kazi hizi zote kwa umahiri, maarifa na utaalamu...
Inaonekana bado ina ile mizuzu inayopenda kukaa ofisi badala field, kunywa chai na mandazi ya mamilioni!
Yaani unapewa tenders lukuki unashindwa hivi hivi kweli?! Nguvu kazi zipo, hela zinatolewa in advance!
Bure kabisa hawa TBA, fukuza safisha, anza na watu wanaojielewa, TBA bado yaweza kupiga kazi zote hizi..
 
Hata kama wewe ni mhandisi nafikiri ukandarasi unausikiaga tu!
 
Bure, aghali. Tuwape muda. Sheria ya karma....ifanye kazi.
 
Back
Top Bottom