Tb Joshua "Kesheni mkiomba"

Mandela5599

Member
Jul 28, 2020
65
278
Tarehe 5/6/2021 siku 6 kabla ya birthday yake kufikisha miaka 58 Tb Joshua na mtumishi wa Mungu maarufu duniani alitwaliwa na Mungu.

Tb Joshua aliingia kwenye garden ambayo alikua akifundishia na kutoa huduma, aliwasalimu watu na alianza kusema maneno haya "Kuna majira tofauti, majira ya kuja hapa kusali na majira ya kurudi nyumbani baada ya huduma" kwa siku hii hawawekea watu mikono, aliuliza baadhi ya maswali na baada ya hapo aliondoka kwa haraka sana, na baada mfupi alirudi nyumbani kama alivyo sema

Mwaka 2014 aliwaambia waumini wake " siku Mungu akiniambia leo nakuchukua siwezi kuja na kuwaambia moja kwa moja, nitasema kwa mafumbo, wale wanao mwamini baba watatafuta maana ya mafumbo hayo baada ya mimi kutwaliwa."

Lugha za mafumbo nikawaida katika ulimwengu wa roho, "Yesu aliwaambia wayahudi libomoeni hakalu hili nami nitalijenga tena kwa siku tatu" aliposema hekalu walijua alimaanisha jengo lao la kuabudia, kumbe hekalu lilikua na maana ya mwili wake na kujenga siku alimaanisha ufufuko wake baada ya siku tatu. Hizi ni lugha za kiroho

Tangu alipoanza huduma mwaka 1988 mpaka leo, upako na nguvu yake havikuwahi kupungua. Matendo yake, aina ya mafundisho vinatosha kueleza moyo wa kipekee tofauti kabisa na watumishi wengine.

Mungu ampumzishe mahali pema peponi. Ameen
 
Dah.. Huyu mtumishi kafa kifo kizuri sana!

Hajaumwa kabisa!

Mbaya sana mtu unaumwa na kuteseka kitandani miaka kadhaa alafu ndio unafariki!
 
Kwani waumini wake si wamesema jamaa amelala tu, ataamka.
Ila Chalamila kajitakia mwenyewe, eti watu waje na mabango ya matusi kweli!!
 
Halafu mbona kuna usiri sn taarifa za mazishi yake?Kuna nn nyuma ya pazia?
 
Back
Top Bottom