TB Joshua....Emmanuel TV

Asante kaka Pius. Vipi wakati Ayubu anateseka kama tunavyosoma biblia...watoto wake...mifugo yake..wake zake...do u think kipindi chote hicho hakua na imani??..na kwamba alikua hamwombi Mungu??.....Kiufupi najitahidi kusali..namwamini Mungu sana...na ninajua bila yeye mimi si kitu. Kuna vitu vingi vigumu nimepitia but bila yeye nisingeandika hata hii thread. Naweza kusema Muda tu haujafika. Hata Ayubu muda wake ulivyofika...alipewa na Mungu vitu vingi vizuri zaidi ya alivyokuanavyo awali. God's time is the best.
 
Nikiwa na pesa hua natoa kaka. Sasa sina pesa..nitatoa nini??......
 
Ukiangalia Emmanuel TV. .utashangaa kuona wachungaji wengi wanavyoconfess kwa kuwarubuni watu. Wengi wanatumia nguvu za giza. Kikubwa ni kuangalia sehemu ambapo Mungu yupo. Hata Yesu alifuatwa na watu kokote aendako...na wengine walidiriki kumfuata hata sehemu ya mbali kwasababu walisikia miujiza na matendo makuu ya ajabu aliyokua akifanya...na enzi hizo hakukua na TV..u can imagine. Ili imani ikue zaidi matendo pia yanahusika. Nashindwa nikupe mfano gani....anyways..Nimekuelewa.
 
Umeokoka?au unamtania mungu? Je uko kwenye njia sahihi inayompendeza yeye usije kuwa unatenda dhambi halafu unategemea kuona mkono wa mungu biblia inasema chakula cha watoto hawezi kuwapa mbwaaa je wewe ni mtoto au mbwa ?tafakari chukutua hatua
 
Nashukuru kwa ushauri. But Generally...sijaandika kumkebehi Mungu..tafadhali. Na narudia kusema mnisamehe kwa hilo. Ningefurahi zaidi usome kitu kizima na kukitafakari ndipo unatoa komenti. Sio kuchukua baadhi ya lines na kuhisi kwamba am joking God. Nisamehe bure na Mungu pia anisamehe kwa kukupa hisia hizo.
 
Pole sana ..nadhan kwa sasa usishike tena tv ili Mungu akuonekanie. Nadhan ni muda muafaka wa Kushika NENO la Mungu ili ufanikiwe. Yaish maneno ya Mungu yeye ni mwaminifu mambo yakuwa safi.
 
Nimeshashika sana screen ya TV wakati anaomba ili nipate kazi lakini wapi??..yerewiiiii....majanga mbona majanga mwenzenu. Wanasema God's time is the best. Nataka niende pale kwa Reinard Bonke nikajaribu kuombewa but nasikia mastory yake tena mara ooh..alishawahi kukamatwa anaingiza sembe bongo...mara ooh..sijui eti eti hana upako sana...yan mpaka nachanganikiwa...yan full mastory. .mavimavi tu. Sio kwamba simwamini Mungu but sasa ivi kuna wachungaji wengi sana wanatumiwa na ibilisi. ...so yatupasa kua makini sana. Nani hapa anamjua Bonke vizuri......anikomvinc kupitia miujiza yake...

Kuna shuhuda moja nilibandika hapa kwenye uzi wako ili ujifunze jinsi ya kuomba.Kupitia hilo bandiko lilinifungua sana pia binafsi.Ni refu kiasi lakini litakupa kitu.
 
Mkuu kb52 inawezekana ulishalisoma mahali lakini rudia tena kupitia!!

Yafuatayo ni maelezo ya Mchungaji John Mulinde:
Napendanikushirikishe ushuhuda wa kijana mmoja ambaye aliokoka; kijana ambaye alikuwaakimtumikia ibilisi. Na mtu yule alipotoa ushuhuda wake, ulinitia changamotokubwa sana. Sikutaka kuamini. Ilinibidi nifunge kwa muda wa siku kumi mbele zaBwana, huku nikimuuliza, "Bwana, hivi mambo haya ni kweli?" Na ilikuwani katika wakati huo ndipo Bwana alipoanza kunifundisha kile kinachotokeakwenye ulimwengu wa roho pale tunapoomba.Kijana huyu alizaliwabaada ya wazazi wake kuwa wamejiweka wakfu wao wenyewe kwa lusifa. Wakati badoakiwa tumboni, walifanya matambiko mengi na kumweka wakfu awe mtumishi walusifa. Alipozaliwa na kufikisha miaka minne, tayari alianza kutumia nguvu zakeza kiroho. Hata wazazi wake walianza kumwogopa! Akiwa na miaka sita, baba yakealimkabidhi kwa wachawi ili akapatiwe mafunzo. Na akiwa na miaka kumi, alikuwaakifanya mambo makubwa katika ufalme wa ibilisi. Alikuwa akiogopwa hata nawachawi wa kawaida.Alikuwa bado nikijana mdogo, lakini mambo aliyokuwa anafanya yalikuwa ni mabaya mno. Alikuahadi kufikia miaka ya ishirini akiwa na damu nyingi ya watu mikononi mwake.Aliua watu kila alipotaka. Alikuwa na uwezo wa kutoka nje ya mwili wake kupitiataamuli ya kinjozi (transcendental meditation), yaani kitendo cha kutulizamawazo na mwili kama wafanyayo Wahindukatika yoga. Tazama mfano HAPA. Katika hukokutaamuli, angeweza hata kunyanyuka kimwili kutoka ardhini pale alipokaa nakuelea hewani (levitate). Tazama mfano HAPA. Wakati mwinginealiweza kutoka nje ya mwili; akauacha mwili wake na kwenda nje huko na kulekufanya mambo mbalimbali (astro-travelling). Na kijana huyu alitumiwa nashetani kuharibu makanisa mengi; na kuwaharibu wachungaji wengi.Siku moja, alipangiwakwenda kuharibu kanisa moja ambalo lilikuwa na maombi ya kutosha. Kulitokea namigawanyiko mingi kanisani na kuchanganyikiwa kwingi. Alianza kufanya kazikwenye kanisa hili; lakini mchungaji wa kanisa lile aliitisha mfungo wa kanisazima. Kanisa lilipoanza kufunga, watu walitubu sana na kufanya mapatano mengi.Na watu wakawa kitu kimoja, na wakaanza kuomba kwa ajili ya kazi ya Bwanakatikati yao. Na wakaendelea kufanya maombezi na kumlilia Mungu ili awarehemuna kuingilia kati maishani mwao. Na kadiri siku zilivyoendelea, bwana huyualikuwa akija tena na tena akiwa na mapepo kinyume na kanisa hili. Lakinililitoka neno la kinabii likiwaambia Wakristo wasimame pamoja na kufanya vitadhidi ya nguvu za giza ambazo zilikuwa zinashambulia kanisa lile.Siku moja, kijanahuyu aliuacha tena mwili wake chumbani kwake na akatoka nje. Aliongoza jeshi kubwala mapepo moja kwa moja hadi kwenye kanisa lile ili kwenda kufanya vita vyakiroho.Sasa, ufuatao niushuhuda wake.Roho yake ilikuwainapaa hewani juu ya kanisa lile na kujaribu kulishambulia, lakini kulikuwa nakifuniko cha nuru juu ya kanisa hilo. Wakati waliendelea na mapambano, ghafla,kulikuja jeshi la malaika ambalo liliwashambulia na kukawa na mapambano makalipale hewani. Hatimaye, mapepo yalikimbia, lakini yeye alikamatwa na walemalaika.Ndiyo, alikamatwa namalaika! Alijiona akiwa ameshikiliwa na malaika sita. Na wakamleta kwakumpitisha kwenye paa hadi kwenye madhabahu ya kanisa. Akawa yuko pale hukuwatu wanaendelea kuomba. Walikuwa wamezama kwenye maombi, wakifanya vita vyakiroho; wakifunga na kuvunja, na kutupa nje. Mchungaji alikuwa kwenye madhabahuakiongoza maombi hayo na vita. Roho wa Bwana akaongea na mchungaji, akisema, "Niraimevunjika, na mhusika yuko hapa mbele yako. Msaidie kwa kumfungua."Mchungaji alipofunguamacho yake, alimwona yule kijana akiwa ameanguka pale hajitambui. Mwili wakeulikuwa pamoja naye! Kijana yule anasema kuwa haelewi ni kwa vipi mwili wakeuliungana naye; maana alikuwa ameuacha nyumbani. Lakini ndio alikuwa pale;hajui ni kwa vipi aliingia, isipokuwa tu malaika walimpitishia kwenye paa.Sasa, mambo haya nimagumu kuamini, lakini mchungaji alinyamazisha kanisa na kuwaambia kile ambachoBwana alimwambia. Kisha akamwuliza yule kijana, "Wewe ni nani?" Kijanayule alikuwa anatetemeka wakati mapepo yalipoanza kumtoka.Kwa hiyo, waliombakwa ajili ya kufunguliwa kwake, na hatimaye baadaye alianza kusema ushuhudawake. Hivi sasa kijana huyu ameshaingia kwa Bwana na ni mwinjilisti, akihubiriInjili. Anatumiwa sana na Bwana kuwaweka huru watu wengine.Usiku mmoja, mimi(John Mulinde) nilienda kwenye chakula cha usiku mahali fulani. Sababu hasa yakwenda pale ni kwa vile kuna mtu alinieleza habari za huyo kijana; na nilikuwana shauku kubwa sana ya kumwona, na kuona kama kweli hadithi yake ina ukweliwowote. Kwa hiyo, nilipofika, nilikaa mezani. Na jioni ile, kijana huyu alipewanafasi ya kutoa ushuhuda wake. Alizungumza juu ya mambo mengi sana. Maranyingine alilia kutokana na mambo aliyoyafanya. Alipomaliza kusema, alitoaombi.Kulikuwako nawachungaji wengi pale kwenye ukumbi. Alisema, "Ninawaomba ninyi, wachungaji.Tafadhalini, wafundisheni watu namna ya kuomba." Watu ambao hawaombi,wanaweza kuchukuliwa na chochote, katika chochote na ibilisi; na ziko hata njiaza adui za kutumia maisha yao na maombi yao. Adui anajua hata namna ya kutumiakwa faida yake maombi ya watu wasiojua kuomba. "Wafundisheni watu namna yakutumia silaha za kiroho ambazo Mungu amezitoa."Kisha alieleza jinsiambavyo alikuwa akiongoza mapambano kwenye anga. Alikuwa akienda pamoja namaajenti wengine wa shetani na mapepo mengi hadi angani. Ilikuwa kama zamu.Inabidi kwenda kutekeleza zamu yako. Kwa hiyo, ni mara nyingi tu alikuwa namuda wa kwenda kwenye anga ili kufanya vita. Na akasema kuwa kule angani,kwenye ulimwengu wa roho, kama anga limefunikwa na blangeti la giza, blangetihilo linakuwa ni nene sana; na ni kama jiwe. Na linakuwa limefunika eneo lote.Na mapepo haya yanaweza kwenda juu yake na chini yake. Na yakiwa huko, yanawezakuathiri matukio yanayoendelea duniani.Pale mapepo wachafupamoja na maajenti wa shetani wa kibinadamu wanapomaliza zamu yao, wanashukaduniani kwenye maeneo ya kimaagano, iwe ni kwenye maji au ardhini, ili kuwezakurejesha upya nguvu zao, maana zinakuwa zimepungua kutokana na kufanya kaziangani wakati wa zamu yao. Na wanarejeshaje nguvu zao? Ni kupitia kafara ambazowatu wanatoa kwenye madhabahu hizi. Kafara zinaweza kuwa ni uchawi wa wazi,damu za aina zote, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba, vita, na utoaji wa kafaraza wanadamu na wanyama. Zinaweza pia kuwa ni kafara za uzinzi, pale ambapo watuwanafanya uzinzi na uashetati wa kila aina. Na matendo haya maovu yanaletanguvu kwenye ulimwengu wa giza. Na ziko aina nyingi za kafara.Kijana huyo alisemakuwa, maajenti wa shetani wanapokuwa juu kwenye anga, na Wakristo wakaanzakuomba hapa duniani, maombi ya Wakristo huonekana kwa namna tatu. Maombi yotehuonekana kama moshi ambao unapaa kuelekea mbinguni.Baadhi ya maombihuonekana kama moshi, na yanaenda juu kiasi na kupotelea hewani. Maombi ya ainahii hutoka kwa watu ambao wana dhambi maishani mwao na hawako tayari kushughulikanazo. Maombi yao ni dhaifu sana, kiasi kwamba yanapeperushwa na kupoteleaangani.nyingine ya maombinayo ni kama moshi ambao unainuka juu hadi unapofikia kwenye ule mwamba, lakinihayana nguvu ya kupenya mwamba huo. Kwa kawaida, hawa ni watu ambao hujaribukujitakasa, lakini hawana imani juu ya kile ambacho wanakifanya palewanapoomba, yaani wanaomba lakini moyoni hawana ujasiri kwamba kilewanachokiomba watakipokea. Mara nyingi huwa wanapuuzia mambo mengine ya muhimuyanayotakiwa wakati mtu anapoomba.Aina ya tatu yamaombi ni kama moshi ambao umejaa moto. Yanapokuwa yanapaa, yanakuwa ni ya motosana kiasi kwamba yanapoufikia ule mwamba, unaanza kuyeyuka kama nta. Yanapenyamwamba huo na kuendelea hadi juu.Mara nyingi watuwanapoanza kuomba, maombi yao huonekana kama aina ya kwanza ya maombi. Lakinikadiri wanavyoendelea kuzama, yanageuka na kuwa ya aina ya pili. Na wakiendeleazaidi, ghafla yanalipuka moto. Na maombi hayo yanakuwa yana nguvu sana kiasikwamba yanapenya kabisa ule mwamba.Mara nyingi maajentiwa uovu hubaini kwamba kuna maombi yanabadilika na kuelekea kwenye kuwa moto.Kisha huwasiliana na viumbe vingine vilivyoko duniani na kuwaambia, "Mvurugienimtu huyo maombi! Mfanyeni aache kuomba! Mwondoeni kwenye maombi!"Mara nyingi Wakristohushindwa na mbinu hizi. Wanakuwa wanaomba kwa nguvu; wanatubu; wanaruhusu Nenokukagua nafsi zao; imani inaanza kujengeka. Maombi yao yanaanza kuwa na shabahazaidi. Kisha ibilisi anaona kuwa maombi yao yanaanza kukusanya nguvu. Ndipovurugu zinaanza ili kuharibu maombi hayo. Mara simu inalia. Wakati mwingine,katikati ya maombi ambapo mtu alikuwa amezama kabisa, , simu inaweza kulia naunawaza kuwa, ngoja niende nikaipokee kisha nitarudi kuendelea na maombi.Mbinu zingine zakuvuruga maombi nazo zinaweza kutumika; hata kama ni kukugusa mwili wako nakuleta maumivu mahali fulani. Hata pia kukufanya ujisikie njaa ambapoutajisikia kwenda jikoni kutengeneza japo chakula kidogo. Ilimradi tu wakiwezakukufanya utoke mahali pale, wanakuwa wameshakushinda. Wachungaji, ni lazimamuwafundishe watu jinsi ya kuomba. Tengeni muda, si tu kwa ajili ya maombi yajuujuu. Mara moja kwa siku, Wakristo wanatakiwa kuwa na muda wa kujielekeza kwamoyo wote kwa Mungu, bila kuwapo kwa kitu chochote cha kuwaharibia umakini wao.Na kama watuwaking'ang'ana kabisa kwa njia hii ya maombi na kuruhusu kupata mwongozo wakiroho, kisha wakawa wanaendelea na kuendelea, lazima kitu kitatokea rohoni.Moto utalipuka na kugusa ule mwamba na kuuyeyusha! Kuyeyuka kunapoanza, ni motosana kiasi kwamba hakuna pepo ambaye anaweza kustahimili. Wala hakuna roho yamwanadamu inayoweza kustahimili pia. Wote wanakimbia.Kama mtu atajitoakuomba kwa bidii na kwa kumaanisha namna hiyo, hatimaye kutafuata kufunguka kwaulimwengu wa roho. Na mara hili linapotokea, matatizo yote haya katika maombiyanafikia mwisho! [Yaani ule ugumu na ule uzito unakwishilia mbali!] Yuleambaye anakuwa anaomba duniani anakuwa sasa anajisikia kuwa maombi ni kitukilaini kabisa, cha kuburudisha, na chenye nguvu.Na nimegundua kuwawakati huo, huwa tunapoteza kabisa hisia za muda na mambo mengine. Si kwambatunakosa mpangilio; la hasha! Mungu anakuwa anashughulika na muda wetu. Lakiniinakuwa ni kama unaachilia kila kitu, na unaunganishwa moja kwa moja na Mungu.Maombi yako yanapopenya, kunakuwa hakuna kizuizi tena kuanzia hapo; na mtuanayeomba anaweza kuendelea kwa muda mrefu kama apendavyo. Hakuna kabisakizuizi.Na mara anapomalizakuomba, lile tundu linabakia wazi.Kijana huyu piaalisema kuwa, watu wa namna hii wanapomaliza kuomba na kuondoka mahali hapo,lile tundu linakuwa linaondoka pamoja nao. Wanakuwa hawaenendi tena chini yalile blangeti la jiwe. Wanakuwa wanaenenda chini ya mbingu zilizo wazi. Naakasema kwamba, katika hali hiyo, ibilisi hawezi kufanya kile anachokitakakwao. Na uwepo wa Mungu unakuwa kama nguzo kutoka mbinguni ikiwa iko juu yamaisha yao. Wanalindwa; na kunakuwa na nguvu kubwa sana ndani ya hiyo nguzokiasi kwamba kadiri wanavyotembea huku na kule, uwepo huo unakuwa unagusa hatawatu wengine. Nguzo hiyo inakuwa inatambua kile ambacho adui amefanya kwa watuwengine. Na pale watakatifu hao wanapozungumza na watu wengine, na wale watuwakawa wamesimama nao, wanaingia ndani ya nguzo hiyo. Na mradi tu wakiwa ndaniya ile nguzo, vifungo vyote vya adui vinadhoofika.Kwa hiyo, watu hawawenye mpenyo huu wa kiroho wanapowashuhudia wenye dhambi habari za Yesu Kristo,upinzani wa wenye dhambi unakuwa wa chini. Ni rahisi kuwaleta wenye dhambi kwaKristo. Wanapoomba kwa ajili ya wagonjwa, au kwa ajili ya mambo mengine, maombiyao yanakuwa na nguvu sana.Na kama kuna sehemuambako maombi ya namna hii huombwa mara kwa mara, uwepo wa Mungu unakuja mahalipale na hauondoki. Hivyo, hata watu wasiomjua Mungu wanapokuja kwenye sehemukama hizo, ghafla vifungo vyao vinakatika.Na kama atatokea mtuwa kusema nao kwa uvumilivu na kwa upendo, wanaweza kugeuka haraka sana; si kwanguvu au kwa uwezo, bali ni kwa Roho wa Mungu, ambaye anakuwa yuko pale. Nakama hakuna mtu atakayewajali watu hawa, wanakuja kwenye uwepo wake nakujisikia hatia, wanaanza kujadili kama wakubali au la. Pale watakapoondoka,vifungo vinakuwa na nguvu zaidi kwao. Na ibilisi anajihadi kwa kila njiakutowaruhusu kurudi tena kwenye sehemu kama hizo.Je, shetani anakaa kimya tu baada ya mtu kupata mpenyo?Kijana huyu alisemakuwa, ibilisi anawachukia sana watu wa namna hiyo, yaani wale waliopata mpenyowa maombi.Sasa unaweza kupigapicha, sote tulikuwa tumekaa chini tunamwangalia kijana huyu akieleza ushuhudawake. Alikuwa anatueleza mambo ambayo yeye mwenyewe alikuwa akiyafanya naaliyoyashuhudia kwa macho yake. Alitueleza kile ambacho walifanya kwa watuambao walipata mpenyo katika maombi. Alisema kuwa waliwaweka akilini sana watukama hao. Kisha waliwafuatilia sana na kujifunza kuhusu wao ili kuwajua vizuri.Walitafuta kila kitu kuwahusu. Hivyo, walifahamu udhaifu wao wote, na ikitokeamtu akawashinda kwenye maombi na kupenya, wanawasiliana na wengine kwenyeulimwengu wa giza na kusema, "Mumlenge mtu huyu kwenye eneo hili na hili.Udhaifu wake uko hapa na hapa."Kwa kuwa mtu wa ainahii anapotoka nje ya kifuniko cha maombi, roho ya maombi inakuwa juu yake,uwepo wa Mungu upo juu yake, roho yake inakuwa iko juu, na furaha ya Bwanandiyo nguvu zake; anapokuwa anaenda, adui anajaribu kila njia kuleta yale mamboambayo yatamvuruga ili asielekeze macho yake kwa Bwana.Kama, kwa mfano,imeshajulikana kuwa udhaifu wake uko kwenye eneo la hasira, basi aduiatasababisha watu watende mambo ambayo yatamfanya akasirike. Na kama hayukomakini kumsikiliza Roho Mtakatifu, na akaingiwa na hasira, basi ataondoa machoyake kwa Bwana. Na anapokuwa na hasira hivyo, ghadhabu zinamjaa. Baadayeanapokuja kujirudi, anakuwa anataka kutupilia mbali hali hiyo na kuendelea nafuraha ya Bwana, lakini anajikuta hajisikii tena ile furaha kama mwanzo.Anajitahidi kujisikia vizuri tena; lakini haiwezekani tena. Kwa nini?Alipojiachilia kwenye kishawishi cha hasira, mapepo walifanya bidii zote katikamuda huo kufunga lile tundu kule juu. Na mara waliporudishia lile jiwe, uwepowa Bwana unakuwa umekatika, yaani ile nguzo iliyokuwa inatokea mbinguni nakumfunika inakuwa haimfikii tena!Mtu huyo hataachakuwa mwana wa Mungu. Lakini ule upako wa ziada uliokuwa unaandamana nayemaishani; ule uwepo uliokuwa ukitenda mambo bila yeye kutumia nguvu zozote,unakuwa umekatika! Maana pepo wachafu wanatafuta uliko udhaifu wako.Kama udhaifu wa mtuni kwenye masuala ya mapenzi, adui ataandaa watu, matukio, na mambo ambayoyatainua hisia za mtu huyo za tamaa ya kimapenzi. Na kama mtu huyo atazikubaliahizo tamaa na kufungua akili yake kuyapokea mambo hayo, na kuyalea nafsinimwake, pale anapomaliza kila kitu na kutaka kurejea tena kwenye hali ya upakoili asonge mbele, anakuta kwamba ule uwepo haupo tena. Labda unasema, "Hii sivizuri kabisa." Kumbuka tu Biblia inasemaje, " Tena ipokeeni chapeo ya wokovu.Vaeni dirii ya haki." Mara nyingi hatuoni haja ya silaha hizi za kivita. Lakinikumbuka Yesu alivyotuambia juu ya namna ya kuomba "Usitutie majaribuni, lakiniutuokoe na yule mwovu."Kila mara unapopatampenyo katika maombi, unapofika mwisho, kumbuka kuwa wewe bado ni kiumbemwanadamu aliye dhaifu. Kumbuka kuwa haujakamilishwa bado. Mwombe Bwana, useme,"Bwana, nimefurahia wasaa huu wa maombi, lakini nitakapotoka nje kwenye dunia,usiniongoze kwenye majaribu. Usiruhusu niangukie kwenye mtego wa ibilisi. Najuakuwa adui anatega mitego kule nje. Sijui ni mitego ya namna gani. Na ninajuakuwa bado mimi ni dhaifu katika baadhi ya maeneo. Kama nikiingia kwenye halifulanifulani, nitaanguka. Unilinde, Bwana. Unapoona ninaelekea kule ambako kunamitego niliyotegewa, nifanye nielekee upande mwingine. Uingilie kati, Ee,Bwana. Usiche niende tu kwa nguvu zangu na uwezo wangu. Niokoe na yule mwovu."Mungu anaweza kufanyahivyo. Lakini, kama kuna kitu kibaya kitatokea, ambacho kitakufanya uondoemacho yako kwa Kristo, wewe sema tu, "Asante Yesu." Ndiyo sababu Mtume Pauloaliandika, "Mshukuruni Mungu kwa kila jambo." Baadhi ya mambo si mazuri.Yanaumiza, na tunashangaa kwa nini Mungu anayaruhusu yatufikie. Lakini kama tutungejua kwa njia hiyo anatuokoa na mambo yapi, tungemshukuru. Tukijifunzakumwamini Bwana, tutamshukuru kwa kila jambo.Yule kijanaaliendelea kusema kuwa, unapopata mpenyo katika maombi, majibu yako ni lazima yatakuja. Alisema kuwa jibumara zote huja, lakini mara nyingi, huwa halifiki kwa mtu aliyeliomba. Kwanini? Ni kwa sababu ya mapambano yaliyoko kwenye anga. Pia, majibu yanawezakuzuiliwa iwapo viumbe waovu wa rohoni watafanikiwa kurejesha ule mwamba nakuziba tundu ambalo mwombaji alifanikiwa kulitoboa kwa njia ya maombi yake.Kisha aliongea jamboambalo kwa kweli lilitikisa imani yangu. Binafsi ilinibidi niingie kwenyemfungo wa siku kumi, ili kumwuliza Bwana kama hilo alilosema lilikuwa na ukweliwowote. Basi sikiliza haya: Kijana huyu alisema kuwa, kila Mkristo anayemalaika ambaye anamtumikia Mkristo huyo. Nasi tunafahamu kuwa Biblia inasemakuwa malaika ni roho wanaotutumikia. (Waebrania 1:14). Alisema kuwa watuwanapoomba, majibu huletwa kwa mikono ya malaika. Malaika huleta majibu, kama ambavyotunasoma kwenye kitabu cha Danieli. Kisha alisema jambo ambalo ni gumu sana.Alisema kwamba, kama yule anayeomba anafahamu silaha za kiroho na amejivikasilaha hizo, majibu nayo huja kwa kupitia malaika ambaye, naye amejivikakikamilifu kwa silaha hizohizo.Lakini, kamaanayeomba hajali silaha za kiroho, basi malaika nao wanakuja bila silaha hizo.Wakristo ambao hawajali kile ambacho kinaingia mawazoni mwao; hawashindanikuangusha mawazo yasiyofaa; malaika wao huja bila chapeo. Silaha zozoteutakazoacha kuzitilia maanani duniani, malaika anayekutumikia naye anakuwahanazo. Kwa maneno mengine, silaha zetu za kiroho hazitulindi miili yetu, balizinalinda vitu vile vya kiroho tunavyofanikiwa kuvipata kutoka kwa Bwana.Malaika anapokuwaanakuja, mapepo wanamtazama na kumkagua na kubaini maeneo ambayo hajajifunika;na hayo ndiyo maeneo ambayo watashambulia. Kama hana chapeo kichwani, basiwatashambulia kichwani. Kama hana dirii, watashambulia kifuani. Kama hanaviatu, watajaribu kutengeneza moto ili kumwunguza miguuni.Sasa, najua kuwa hilini gumu kuamini; mimi narudia tu kile ambacho kijana huyu alisema. Kishatulimwuliza, "Je, malaika wanaweza kuungua moto?" Na unajua alisema nini?Kumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa roho. Hizi ni roho kwa roho zinapambana. Mapambanoni makali sana, na pale wanapomshinda malaika wa Mungu, jambo la kwanzawanalokimbilia ni lile jibu alilobeba; na wanalichukua hilo. Na hizi zinakuwani zawadi ambazo hutolewa kwa watu kupitia imani za siri, au uchawi.Kumbuka kile ambachoBiblia inasema kupitia kitabu cha Yakobo. Vipawa vyote vyema hutoka kwa Mungu(Yakobo 1:17). Kwa hiyo, shetani anapata wapi vitu vizuri anavyowapatia watu?Baadhi ya watu ambao hawawezi kupata watoto, huenda kwa wachawi na waabudushetani, na wanapata mimba! Mtoto anakuwa ametoka wapi? Je, shetani nimuumbaji? HAPANA! Anaiba kutoka kwa watu ambao hawaombi maombi yao hadi mwisho.Katika Biblia, Yesualisema, "Ombeni bila kukoma." Pia alisema, "atakapokuja Mwana wa Adamu, je!Ataiona imani duniani? " Je, Yesu atakukuta bado unangojea? Au utakata tamaa nakumwacha adui aibe kile ambacho umekuwa ukikiombea?Na hawaridhiki tu nakuiba jibu la maombi. Wanataka pia kumweka malaika kifungoni. Na wanaanzakupambana naye. Wakati mwingine wanafanikiwa kumkamata na kumfunga malaika.Inapotokea hivyo, Mkristo anakuwa kama chakula chao duniani. Wanaweza kumfanyiachochote maana hana ulinzi tena kwenye ulimwengu wa roho.Nilimwuliza kijanahuyo, "Una maana kuwa malaika anaweza kushikiliwa katika ulimwengu wa giza?"Sasa alikuwa anaeleza uzoefu wake, na akasema, hawatamshikilia malaika kwa mudamrefu kwa sababu ya Wakristo wengine ambao wanaomba mahali pengine. Jeshi laziada litatumwa, na malaika atakuwa huru. Na kama yule Mkristo anayehusikahajaomba hadi kwenye mpenyo, basi atabakia mateka. Ndipo shetani atatumamalaika wake na malaika wa nuru kwa mtu huyu, na hapo ndipo uongo naudanganyifu unapotokea; maono ya uongo na unabii wa uongo. Uongozi wa uongo, nakufanya kila aina ya maamuzi mabaya. Na mara nyingi, mtu wa namna hii anawezakupata mashambulizi na vifungo vya kila aina.Niliondoka kwenyekile chakula cha jioni huku na mawazo mengi sana. Nikasema, "Bwana, sitaki hatakujaribu kuamini jambo hili." Linaondoa ujasiri na usalama wangu wote!Nilipoenda kumlingana Bwana, ilikuwa ni kwa siku kumi; na Bwana alifanya mambomawili. Kwanza, si tu kwamba alithibitisha mambo hayo niliyoyasikia kutoka kwayule kijana, bali pia alifungua akili zangu zaidi ili kuona mambo mengine mengizaidi ya yale ambayo niliyasikia. Pili, aliniongoza kuona kile ambachotunatakiwa kukifanya wakati mambo haya yanapotokea ili tuweze kuwa washindi.Alinipa mambo matatu:Moja: namna ya kutumiasilaha za vita vyetu vya kiroho. Biblia inaziita silaha za Mungu. Si silahazetu. Tunapozitumia, tunamruhusu Mungu kupigana kwa niaba yetu.Mbili: tambua uhusiano waroho zinazotutumikia, yaani malaika, na maisha yetu ya kiroho. Na ni lazimakuwa makini sana na kile kinachotokea mioyoni mwetu; kama mwongozo wa kileambacho kinatakiwa kutokea rohoni kutuhusu sisi.Tatu: ni Roho Mtakatifu.Roho Mtakatifu hatakiwi kuja kama mtumishi wetu, kututumikia na kutuletea vitumbalimbali. Hakimbiikimbii kwa Baba kumweleza kile ambacho tunataka. Hiyo nikazi ya malaika. Lakini Yeye husimama pamoja nasi. Anafanya nini? Anatuongoza,anatufundisha, anatutangulia, anatusaidia kuomba inavyotakiwa. Na mambo hayayanapotokea kwenye ulimwengu wa roho, anatuambia. Wakati mwingine anakuamshausiku na kukwambia, "Omba." Wewe unasema, "Hapana! Muda wangu haujafika." Naanasema, "Omba sasa!" Kwa nini inakuwa hivyo? Ni kwa sababu Yeye anaona kilakinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Wakati mwingine anasema, "Kesho nikufunga." Wewe unasema, "Hapana, nitaanza Jumatatu!"Lakini kumbuka kuwaYeye anaelewa kile kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Ni lazima tujifunzekuwa makini na Roho Mtakatifu. Anatuongoza kwenye njia za haki. Wapendwa,tuishie hapa. Labda wakati mwingine tutaongea jinsi ambavyo tunaweza kuombahadi kupata mpenyo, maana sasa tunajua mapambano yaliyoko rohoni na jinsi yakupenya; na namna tunavyoweza kudumu tukiwa na mpenyo tuliopata. Na maratunapojifunza hili, linakuwa ni jambo la furaha sana. Tukumbuke tu jambo moja:vita si vyetu, bali ni vya Bwana! Haleluya!Hebu tusimame.Mwangalie mwenzio machoni na utafakari ni mara ngapi amekosa kile ambacho Mungualikiandaa kwa ajili yake. Lakini shikaneni mikono kama inawezekana; watuwawili au watatu, kisha tu muambiane, "Hakuna haja ya kushindwa tena! Tunawezakushinda! Iko nguvu ya kutosha kushinda! Yesu tayari ameshafanya kazi yote."Muombeane ninyi kwa ninyi ili Bwana aweze kutusaidia kushinda. Hatutakiwikushindwa. Iko neema ya kutosha; nguvu ya kutosha kuleta ushindi!Asante Yesu.
 
Last edited by a moderator:
Mm emmanuel tv imenipatia kazi nitashuhudia siku zote maana Mungu alinisikia. Ilikuwa mwezi wa 3 mwaka huu nilisali ile sala ya viewers all over the world.., ilikuwa j2 na pale Tb Joshua anasema after 7 days utapata majibu, yaani j2 iliyofuata nikiwa church simu iliita nikachungulia nikaona ni wale walionisumbua na kunikatisha tamaa kwa majaribu mengi ya hiyo kazi, nikatoka nje nkaenda toilet kupokea simu ananiambia ameamua tu kunisaidia na kwamba kesho yake j3 nipeleke cv na vyeti. Mwezi wa 4 niliingizwa kwenye payrol na mshahara nakula sasa kama kawaida..
Kwa ushauri tu msidharau sala na watumishi wa Mungu maana kuna wengi wanasaidika sana kupitia hao watumishi.
 
Nisamehewe kama nakosea, but kwangu mimi huwa napenda kuwa na mahusiano binafsi na MUNGU na ambayo sitaki yawe influenced na vitu vingine, mimi nina mifano yangu binafsi ya KUMUONA MUNGU katika maisha yangu ya kila siku, hata kazi niliyonayo hii sikufanya Interview na ilikua in the last last minute, nimetangaza ndoa, sina kazi na muda umekaribia! Napata kazi kwa urahisi tu, huu ni mfano mdogo sana kati ya mingi. Usikubali kuweka middleman kwenye relation yako na MUNGU wako, hata ukienda kuombewa kumbuka na wewe kuomba mwenyewe! Tuache uvivu wa kutaka kufanyiwa kila kitu.

Ushauri wangu, subiri wakati wa MUNGU ufike, simaanishi kwamba usi-struggle No No wakati wa MUNGU unafika kwa wewe pia ku-struggle, work hard lakini pia mkumbushe MUNGU, mweleze, amka usiku omba, sali, kabla ya kulala mshukuru MUNGU ukiamka do the same, you dont need a two hour prayer or fifteen minutes praying NOP, na katika maombi yako ACHA KULALAMIKA bali mshukuru MUNGU kuwa wewe umzima na kwamba japo umzima lakini kuna mambo pia ungeyapenda uyaone kwa macho ya nyama (hapa wengi hua tunakosea kwasababu tunaomba vitu au kazi ili kuwakomoa wengine, ndugu yangu ukishaweka hayo mawazo sahau) maana MUNGU hataruhusu akupe vitu ambavyo vitakufanya uache ulokole wako au mapenzi yako kwa MUNGU yapungue, umeomba kazi, umepata kazi, sasa kuabudu hutaki kwasababu uko BUSY na KAZI, Mpuuzi wewe, MUNGU atachukua kazi hio na hutakua na cha kusema.

CC: Mamndenyi Aine ladyfurahia Mtambuzi na wapendwa wengine
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Melj.....nashukuru. Na ninaomba Mungu anisamehe kwa hilo koz watu wengi wameelewa kwamba nawakebehi au kuwadharau watumishi wa Mungu.Nilimaanisha mbona sifanikiwi na mimi?..Namuomba Mungu aliyekufanikishia muujiza wako afanye na kwangu pia..katika jina la Yesu Amina. Asante Yesu kwa kua unakwenda kutenda sasa kama Melj ulivyomfanikishia.
 
nimeguswa na hii habari, lakini preta kamaliza yote MUNGU yupo mahali popote pale sio lazima kwa mchungaji,keep praying
 
kb52;
Imani yako kwa Mungu ndiyo itakayokupa ushindi;

Maombi anza kujiombea wewe mwenyewe;
utakapoona kuna umuhimu washirikishe na watu wengine.

Mwambie Mungu sasa imetosha mimi mtumishi wako nataka kazi
itakayoniwezesha kupata pesa;

Mwambie Mungu ukiwa siriazi, tena mpe Mungu muda kabisa,
tena mkumbushe kila mara kuwa nataka kazi, ulisema wewe Mungu ni tajiri kwa nini mimi mwanao niwe masikini,

Ulisema asiyefanya kazi na asile;

Ulisema ombeni lolote kwa Jina langu Nitawapa;

Ulisema niiteni nami nitawaitikia,

sema sana sema sana na Mungu,
pia chukua jukumu, angalia marafiki na watu unaowafahamu waambie wakutafutie kazi;

.......Mungu wetu ni mwaminifu na hakika utafanikiwa.

Nimeshashika sana screen ya TV wakati anaomba ili nipate kazi lakini wapi??..yerewiiiii....majanga mbona majanga mwenzenu. Wanasema God's time is the best. Nataka niende pale kwa Reinard Bonke nikajaribu kuombewa but nasikia mastory yake tena mara ooh..alishawahi kukamatwa anaingiza sembe bongo...mara ooh..sijui eti eti hana upako sana...yan mpaka nachanganikiwa...yan full mastory. .mavimavi tu. Sio kwamba simwamini Mungu but sasa ivi kuna wachungaji wengi sana wanatumiwa na ibilisi. ...so yatupasa kua makini sana. Nani hapa anamjua Bonke vizuri......anikomvinc kupitia miujiza yake...
 
Back
Top Bottom