TB Joshua Ajitetea Kashfa Ya Panama paper

mrimbeni

Member
Dec 10, 2015
30
16
TB Joshua, muhubiri maarufu barani Afrika na raia wa Nigeria, ametajwa kwenye nyaraka za kashfa ya ukwepaji kodi za Panama, akidaiwa kuwa na hisa kwenye kampuni iliyosajiliwa visiwa vya British Virgin Islands.

Mwanzilishi huyo wa Kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote (Synagogue Church of All Nations) na mkewe Evelyn wanadaiwa kuwa na hisa kwenye kampuni hewa ya Chillon Consultancy Limited iliyo kisiwa cha Tortola, ambacho ni kikubwa kuliko vyote vya British Virgin na ambacho hakuna watu wengi wanaoishi.

Wote wawili wanamiliki hisa moja, ingawa kampuni hiyo yenye namba ya usajili 1033675, inaidhinishwa kutoa hisa zisizozidi “50,000 kwa thamani ya hisa ya daraja moja.” Haieleweki ni biashara gani TB Joshua alifanya na kampuni hiyo ambayo haina ofisi kwenye kisiwa hicho cha Tortola.

Lakini muhubiri huyo, amekanusha vikali tuhuma hizo zilizoandikwa na gazeti la Premium Times la Nigeria, akisema zina lengo la kumchafua yeye na kanisa lake na kwamba aliyeandika habari hiyo, Nicolas Ibekwe aliwahi kumtuhumu kuwa alimpa rushwa wakati jengo la nyumba ya wageni la kanisa lake lilipoanguka.

“Mimi si mfanyabiashara na sina biashara. Kitu alichonipa Mungu si cha kawaida. Sihusiki na nyaraka za Panama,” alisema TB Joshua katika taarifa yake aliyoituma kwenye ukurasa wa facebook.

“Mimi na familia yangu tutaendelea kuwa kwenye shamba la Mungu. Premium Times – msiruhusu kampuni yenu kutumika. Msiruhusu kampuni yenu kupingana na Mungu. “Huu ni uongo! Zingatia – habari hii imeandikwa na mwandishi yule yule ambaye alinituhumu kuwa nilimuhonga wakati wa tukio la jengo kuanguka na alienda kwenye vyombo tofauti vya habari – vya ndani na vya kimataifa – kutangaza mambo hayo ya kutunga.

“Tangu wakati wa tukio la jengo, kumekuwa na mfululizo wa vitisho dhidi ya huduma yangu na mimi binafsi kutoka kwa mwandishi huyo, Nicholas Ibekwe, ambaye anawakilisha kikundi cha watu.”

Alisema: “Baada ya yote hayo yaliyofanywa kujaribu kuimaliza huduma hii, hiki ndicho alichoamua kukifanya. Hata picha iliyotumika kwenye habari ilipigwa kwenye mkutano wa injili nilioufanya Mexico. Nilikwenda kwenye mkutano wa injili, na si vinginevyo.”

Muhubiri huyo alitaka nyaraka za Panama zisitumike kushambulia watu ambao wamekuwa wakiwatafuta ili wawachafue kwa kuwa si kila mtu anayetuhumiwa na vyombo vya habari kuhusika kwenye sakata hilo, amehusika.

“Suala langu ni mfano mzuri,” alisema. TB Joshua amejizolea umaarufu kutokana na kutabiria watu matukio yanayotarajiwa kuwatokea na amekuwa akivuta waumini kutoka kila kona ya Afrika kwenda Nigeria kumsikiliza.
 
...Ha ha ha...Eti yuko shamba la Mungu...khaa ...endelea tu kukamua minyumbu yako mm wala hunipati
 
Muongo tuu aliwatangazia waumini yakwamba tar 1,4, raisi wa malawi atafalikii lakini mpaka leo anapeta uyonimchawi tuu kama wachawi wengine
 
Ameen!
Watuache sie tulioamua na tulioona ni mtumishi wa kweli wa Mungu.
Waamini wanachoamni wao na hatujawalazimisha kuamini tb joshua ni mtumishi wa kweli wa mungu!! ipo siku
Umenena Mkuu! Ubarikiwe sana, tena sasa iv ndo nazid barikiwa na Mungu kupitia kwa mtumish wa Mungu wa kweli Tb Joshua, Nimeacha fegi na kitungi na hayo yote c ktk uweza wangu bali katika uweza wa Mungu kuptia kwa Nabii wa Ukweli Tb Joshua, asante Mungu
 
Wajumbe wote wa kuzimu washindwe in Jesus Name. Watakuja kwa njia moja, Bwana atawatawanya kwa njia saba. Wavikwe koti la aibu na fedheha.
 
Tarifa iyo niyakweli kabsa nahata apa jamii forums iliwekwa ambapo kutokana nahofu yawananchi wa malawi rais musalika alitumia terevishen ya taifa kuhubia taifa nakumshutumu tb joshua naakamwambia amezoea uongo mwaka huu hatokufa naatakuepo nakweli tar imepta naungo wake
 
Tarifa iyo niyakweli kabsa nahata apa jamii forums iliwekwa ambapo kutokana nahofu yawananchi wa malawi rais musalika alitumia terevishen ya taifa kuhubia taifa nakumshutumu tb joshua naakamwambia amezoea uongo mwaka huu hatokufa naatakuepo nakweli tar imepta naungo wake
umeambiwa weka ushahid hata wa video tb joshua akiongea hayo!nabii zake zote hata youtube zipo ..Weka basi
 
Bora kaongea manake mimi binafsi nilishaamini anahusika ikiwemo hiyo ya kutoa rushwa jengo lilipoanguka.
 
kusema vibaya watumishi wa MUNGU ni dhambi mbaya sana,.......
mnashutumu muna uhakika??????hamna mtu alieziona hizo pesa ilhali ni hbr tu kisa panama wametoa,........
epukeni kuwasema watumishi wa MUNGU mujiepushe na laana..........
 
Back
Top Bottom