Tazameni Takukuru wanavyotufanya mafala

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0

Takukuru wameshindwa kubaini aliyeiba 40bn/- mali ya Umma wa Watanzania kupitia Kagoda -- hela zilizopitia katika akaunti za matawi ya CRDB -- na ilikuwa kazi rahisi kuwauliza CRDB walilipa zile hela kwa nani. Leo hii wanafuatilia na kuwanasa polisi kwa Sh 2m/- walizochukuwa kuhusu masuala ya utapeli wa mtu binafsi -- padri.

Soma hii stori!!!!

Takukuru yanasa maofisa wa polisi

Daniel Mjema, Moshi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewatia mbaroni maofisa wawili wa polisi wa Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Himo mkoani hapa, kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh2.3 milioni kupitia akaunti ya benki.

Habari za uhakika zilizopatikana jana mjini Moshi, zilieleza kuwa kiini cha sakata hilo kinatokana na kutapeliwa kwa Padri mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, kulikofanywa na mfanyabiashara mmoja mwanamke.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Lucas Ng’hoboko, jana alilithibitishia Mwananchi kukamatwa kwa kwa polisi hao, lakini akakataa kuzungumzia kwa undani kwa sababu linahusu Takukuru.

“Hilo tukio ni vyema mkawauliza Takukuru, kwa sababu ni kesi inayohusu polisi kukamatwa na Takukuru, lakini nataka niwaambie hakuna mtu aliye juu ya sheria hata kama ni polisi…muulize Kamanda wa Takukuru,” alisema Ng’hoboko.

Hata hivyo, Kamanda wa Takukuru Mkoa Kilimanjaro, Lawrence Swima, hakuweza kupatikana jana baada ya simu yake kutopatikana kwa siku nzima, lakini taarifa zinadai maofisa hao walinaswa juzi jioni wakiwa kituoni hapo.

Habari za awali zililidokeza Mwananchi kuwa, mmoja wa maofisa wanaohojiwa na Takukuru ni mwanamke mwenye cheo cha Koplo, mwingine ni Konstebo ambaye ndio kwanza amehitimu Chuo cha Polisi Moshi (CCP).
Inadaiwa mfanyabiashara mmoja mwanamke alikuwa amemtapeli Padri Sh2 milioni na kesi hiyo kufikishwa kortini, lakini Padri aliomba ifutwe na kwamba amemsamehe.

Hata hivyo, taarifa zinadai polisi hao walimkamata mfanyabiashara huyo na kumfungulia kesi ya utapeli na baadaye kumwachia kwa dhamana kwa masharti akatafute Sh2 milioni zirejeshwe kwa Padri na Sh300,000 za kufunga jalada.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, mfanyabiashara huyo aliafiki sharti hilo na kuachiwa kwa dhamana na kutoa taarifa Takukuru ambao walimshauri awashawishi wapokee fedha hizo kupitia Benki.

Inadaiwa kuwa polisi mwenye cheo cha Koplo alidai hana akaunti benki, hivyo akamtafuta polisi mwenzake ambaye alitoa nambari za akaunti yake na fedha hizo Sh2.3 milioni ikaingizwa.

Polisi huyo aliyemaliza CCP (jina tunalo) alikwenda benki na kutoa Sh300,000 zilizodaiwa ni za kumaliza kesi na maofisa wa Takukuru waliokuwa wakifuatilia walipokwenda kituoni na kumkamata ambapo alimtaja mshirika mwenzake.

Chanzo: Mwananchi
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,605
2,000

Takukuru wameshindwa kubaini aliyeiba 40bn/- mali ya Umma wa Watanzania kupitia Kagoda -- hela zilizopitia katika akaunti za matawi ya CRDB -- na ilikuwa kazi rahisi kuwauliza CRDB walilipa zile hela kwa nani. Leo hii wanafuatilia na kuwanasa polisi kwa Sh 2m/- walizochukuwa kuhusu masuala ya utapeli wa mtu binafsi -- padri.

Soma hii stori!!!!

Takukuru yanasa maofisa wa polisi

Daniel Mjema, Moshi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewatia mbaroni maofisa wawili wa polisi wa Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Himo mkoani hapa, kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh2.3 milioni kupitia akaunti ya benki.

Habari za uhakika zilizopatikana jana mjini Moshi, zilieleza kuwa kiini cha sakata hilo kinatokana na kutapeliwa kwa Padri mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, kulikofanywa na mfanyabiashara mmoja mwanamke.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Lucas Ng'hoboko, jana alilithibitishia Mwananchi kukamatwa kwa kwa polisi hao, lakini akakataa kuzungumzia kwa undani kwa sababu linahusu Takukuru.

"Hilo tukio ni vyema mkawauliza Takukuru, kwa sababu ni kesi inayohusu polisi kukamatwa na Takukuru, lakini nataka niwaambie hakuna mtu aliye juu ya sheria hata kama ni polisi…muulize Kamanda wa Takukuru," alisema Ng'hoboko.

Hata hivyo, Kamanda wa Takukuru Mkoa Kilimanjaro, Lawrence Swima, hakuweza kupatikana jana baada ya simu yake kutopatikana kwa siku nzima, lakini taarifa zinadai maofisa hao walinaswa juzi jioni wakiwa kituoni hapo.

Habari za awali zililidokeza Mwananchi kuwa, mmoja wa maofisa wanaohojiwa na Takukuru ni mwanamke mwenye cheo cha Koplo, mwingine ni Konstebo ambaye ndio kwanza amehitimu Chuo cha Polisi Moshi (CCP).
Inadaiwa mfanyabiashara mmoja mwanamke alikuwa amemtapeli Padri Sh2 milioni na kesi hiyo kufikishwa kortini, lakini Padri aliomba ifutwe na kwamba amemsamehe.

Hata hivyo, taarifa zinadai polisi hao walimkamata mfanyabiashara huyo na kumfungulia kesi ya utapeli na baadaye kumwachia kwa dhamana kwa masharti akatafute Sh2 milioni zirejeshwe kwa Padri na Sh300,000 za kufunga jalada.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, mfanyabiashara huyo aliafiki sharti hilo na kuachiwa kwa dhamana na kutoa taarifa Takukuru ambao walimshauri awashawishi wapokee fedha hizo kupitia Benki.

Inadaiwa kuwa polisi mwenye cheo cha Koplo alidai hana akaunti benki, hivyo akamtafuta polisi mwenzake ambaye alitoa nambari za akaunti yake na fedha hizo Sh2.3 milioni ikaingizwa.

Polisi huyo aliyemaliza CCP (jina tunalo) alikwenda benki na kutoa Sh300,000 zilizodaiwa ni za kumaliza kesi na maofisa wa Takukuru waliokuwa wakifuatilia walipokwenda kituoni na kumkamata ambapo alimtaja mshirika mwenzake.

Chanzo: Mwananchi
Ukweli ni kuwa hao polisi si wanamtandao wenzao.................
 
Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,000
2,000
Takukuru..Ni mbwa asiye na meno..ataendelea kulamba supu tu..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom