Tazama, mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Tazama, mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
786
Reaction score
1,315
[Yoh1:6]Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.

[Yoh1:7]Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.

[Yoh1:8]Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.

[Yoh1:19]Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?

[Yoh1:23]Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.

[Yoh1:25]Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?

[Yoh1:26]Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.

[Yoh1:27]Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

[Yoh1:29]Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

[Isa53:2]Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.

[Isa53:3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

[Isa53:4]Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

[Isa53:5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

[Isa53:6]Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

[Isa53:7]Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

[Isa53:8]Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

[Isa53:10]Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;

[Isa53:11]Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki;
Naye atayachukua maovu yao.

[1Pet2:24] Yeye mwenyewe alizibeba juu mtini dhambi zetu mwilini mwake, ili tuwe wafu kwa mambo ya dhambi na tupate kuishi katika haki. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom