Tawi la Chadema Marekani

mzee mtei walau umenena kuna sredi mtu anadai ulipwe fidia kwa kuanzisha cdm? Unaliongeleaje hili?
 
Asante sana mzee wetu kwa maelezo mazuri , na kwenye ushauri wako hapo kwenye nyekundi nadhani ndio msingi muhimu kabla ya kitu chochote kufanya kwenye kufungua haya matawi, na kama utaratibu utabuni vizuri haya matawi hayata tumika kwa maslahi binafsi lakini pia itasaidi ni nchi gani haya matawi yanaweza kufunguliwa maana kuna baadhi ya wenzetu inaweza kuwa ni kinyume na sheria zao
Kwa taarifa ya WanaJF, mwaka wa 1994, nilitembelea Washington DC kwa mashughuli binafsi (actually kuhudhuria mahafali ya mwanangu), na nilichukua fursa hiyo kukutana na Watanzania na baadhi yao wakajiunga na CHADEMA. Nikiwa njiani kurudi nyumbani nilikuwa New York pia kwa siku kadhaa na niliweza kuwaridhisha baadhi ya WaTz waliokuwa wanaishi New York kuchukua kadi za CHADEMA.

Itakumbukwa kwamba kulikuwa na tafrani ya aina yake wakati balozi wa Tanzania ktk Umoja wa Mataifa, Bw. Anthony Nyakyi, rafiki yangu wa siku nyingi, aliponikaribisha nyumbani kwake kwa chakula cha jioni. Wizara ya Mambo ya Nje, kwa kukurupuka, ilimwita Nyakyi nyumbani na kukatisha uteuzi wake, licha ya kwamba umahiri wake ulitumiwa na Mwalimu Nyerere ktk juhudi zake za usuluhishi katika migogoro ya nchi za Maziwa Makuu. Baadaye Nyakyi aliteuliwa na Katibu Mkuu wa UN alimteua Nyakyi kuwa mwakilishi wake huko Liberia.

Niliacha tawi la CHADEMA Washington DC, na nakumbuka Daudi Ballali ndiye aliliongoza, na tuliwasiliana kwa muda, nikimpelekea kadi za chama kupitia mwanangu aliyekuwa anaendelea kumalizia masomo yake. Tawi la CHADEMA la Washington DC, linaonekana lilififia baada ya Ballali na Sadikieli Kimaro kuitwa na Rais Benjamin Mkapa kuja kuwa washauri wake wa kiuchumi. Of course, Ballali aliteuliwa Gavana wa BoT, na hangeweza kuendelea kuwa active kama MwanaChadema. Vituko vya huyu ex-mwanaCDM, ambaye ni marehemu sasa, kuhusiana na EPA n.k. ni mambo yanayonifedhehesha mpaka leo.

Nakubaliana na mawazo kwamba wanaCDM waliopo ughaibuni wanaweza kuimarisha Chama kwa kutupa ushauri, na hata wakati nikiwa Mwenyekiti Taifa, CHADEMA tulipokea vifaa kadhaa kama zawadi au michango yao kuimarisha chama. Nakumbuka baadhi ya fax machines na electric type-writers za kwanza Makao Makuu ya Chadema vilikuwa ni vifaa vilivyotolewa na hawa ndugu zetu wanaoishi ng'ambo.

Ningeshauri kwamba utaratibu unaoeleweka ubuniwe na viongozi wa CDM ili WaTz wanaoishi ughaibuni na wanaoamini ktk itikadi na misimamo ya CHADEMA, washirikishwe kikamilifu.
 
mkuu mimi sio msemaji wa mzee , lakini hakuna fidia kubwa kama
wanachadema wakimuenzi mzee mtei kwa matendo , hii ni pamoja na uadilifu ndani na nje ya chama
mwisho KILA ANAYEWATENDEA WEMA BINADAMU WENZAKE AU KUWASUMBUKIA WATU ATALIPWA NA MUNGU TU, sisi binadamu hatuna uwezo wa kuilipa hiyo fidia, MARTIN LUTHER Jr, jina lake bado linaishi mpaka leo.
lakini JINA LA KIKWETE ambaye yuko hai kila mtu hapa anajua thamani yake.
mzee mtei walau umenena kuna sredi mtu anadai ulipwe fidia kwa kuanzisha cdm? Unaliongeleaje hili?
 
nyumba BUTIHAMA
Ulimaanisha Butiama, nafikiri zawadi nzuri ya watu kama hawa (waanzilishi) si kuwajengea nyumba nzuri au kaburi zuri kama la Kenyata, zawadi nzuri ni kuyaenzi yale mazuri waliyoyanzisha mfano Azimio la Arusha nk.
 
Nashukuru kuna WanaJF wanaunga mkono wazo la kuwa na matawi ya CHADEMA nje ya Tanzania. Of course, matawi hayo ni lazima yafunguliwe kulingana na sheria za nchi husika na uongozi uchaguliwe kufuata masharti,maadili na miiko yetu.

Sasa nijibu maswali yasiyohusika na matawi ya CDM niliyoona nikisoma michango ktk thread hii hapo juu:-

Katika picha ya avatar ya "lifeofmshaba" mtu aliyekaa kati ya Kawawa na jamaa aliyeshika kichwa ni Edward Moringe Sokoine.

Kuhusu mimi kulipwa fidia kwa kuanzisha CHADEMA kama "Superfisadi" anavyokumbusha kuwa kuna thread iliyopendekeza hivyo, kwanza nikiri kwamba sijasoma hiyo thread.

Pili ningetaka kusema kwamba kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa najisikia ninafurahi sana kwamba Chama nilichoshiriki kuasisi kinapiga hatua mbele kuelekea katika malengo yake. Kila siku namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba ameniwezesha kuona baadhi ya matunda ya juhudi hizi: ambayo ni kuingiza na kusimika nchini Tanzania, demokrasia ya kweli. Najua bado hatujaweza kuonyesha mafanikio ktk maendeleo ya kweli kiuchumi na kijamii, lakini naamini mchango wa CDM unaanza kudhihirika, na endapo Watanzania wataamua tuchukue dola, basi mambo yatanoga.

Tatu kuhusu kulipwa fidia, nieleze ni kweli kwamba katika miaka yangu sita niliyotumikia CHADEMA kama mwenyekiti taifa, sikulipwa mshahara wowote na sikusaidiwa kodi ya nyumba nilipokuwa naishi Dar es Salaam. Pia nilitoa magari yangu kwa shughuli za chama pale mwanzoni, na wakati chama kilipomudu kunipa gari kwa safari za chama, nililiacha Dar es Salaam kwa mashughuli ya chama ilipokuwa ni lazima nirudi nyumbani kwa mashughuli ya kifamilia.

Nne nieleze kwamba katika utumishi wangu kwa umma (mfano Gavana BoT, Katibu Mkuu, EAC na Waziri wa Fedha nililipwa kiinua mgongo, yaani gratuity) na sasa nalipwa pensheni kidogo kwa kuwa civil servant kwa miaka 7 kabla ya uGavana na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kwa miaka 4. Kwa hiyo huyo mwanaJF aliye pendekeza Chadema inifidie, labda alielezwa juu ya kujitolea kwangu kwa umma na mafao yangu yaliyo kiduchu.

Nilivyoeleza hapo mwanzo, ni furaha kwangu iliyoje kwamba tumeweza kuifikisha CHADEMA hapa ilipo. Itambuliwe pia kwamba, the supreme effort and sacrifice is still to come kama tunavyoelekea 2015. Hata hivyo, endapo uongozi wake utakuwa na uwezo wa kufidia waliowezesha CDM kufika hapo ilipo, bila kuathiri malengo yetu matakatifu, makuu na muhimu, basi iwe hivyo.
 
Mzee Edwin Mtei,

Nashukuru sana kwa kutupa some background information zinazohusiana na kuwa na matawi ya chama nje ya nchi pamoja na direction ya kutaka Uongozi wa Chama uweke utaratibu unaoeleweka.

Jambo moja muhimu ambalo ningependa lifahamike ni kwamba nimefanya utafiti usio wa kisayansi na usio rasmi katika nchi za Marekani na Ulaya na kugundua kwamba miongoni mwa watu wanaopinga CDM, zaidi ya asilimia 95% yao wanapinga CDM si kwa sababu ya sera bali kwa misingi ya propoganda zenye udini na personal and unfounded attacks on the leadership and waliokuwa candidates.

Nitakuja na thread nyingine siku za usoni kuhusiana na hilo ila kwa sasa ningependa kufikisha ujumbe kwamba tuko Waumini wengi wa dini ya Kiislamu ambao tungependa kupinga propoganda za udini kwa vitendo.
 
ilikua inamjibu huyo aliyesema nyerere alipewa nini?
ulimaanisha butiama, nafikiri zawadi nzuri ya watu kama hawa (waanzilishi) si kuwajengea nyumba nzuri au kaburi zuri kama la kenyata, zawadi nzuri ni kuyaenzi yale mazuri waliyoyanzisha mfano azimio la arusha nk.

kwani nyerere alilipwa sh ngapi kuwaanzishia ccm.
 
kwa hali hiyo kuna umuhimu wa kukufikiria kwa kweli, maana wewe ulitoamuda na mali na sasa chama kina dunda, nadhani siku za usoni hekima itatumika
Nashukuru kuna WanaJF wanaunga mkono wazo la kuwa na matawi ya CHADEMA nje ya Tanzania. Of course, matawi hayo ni lazima yafunguliwe kulingana na sheria za nchi husika na uongozi uchaguliwe kufuata masharti,maadili na miiko yetu.

Sasa nijibu maswali yasiyohusika na matawi ya CDM niliyoona nikisoma michango ktk thread hii hapo juu:-

Katika picha ya avatar ya "lifeofmshaba" mtu aliyekaa kati ya Kawawa na jamaa aliyeshika kichwa ni Edward Moringe Sokoine.

Kuhusu mimi kulipwa fidia kwa kuanzisha CHADEMA kama "Superfisadi" anavyokumbusha kuwa kuna thread iliyopendekeza hivyo, kwanza nikiri kwamba sijasoma hiyo thread.

Pili ningetaka kusema kwamba kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa najisikia ninafurahi sana kwamba Chama nilichoshiriki kuasisi kinapiga hatua mbele kuelekea katika malengo yake. Kila siku namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba ameniwezesha kuona baadhi ya matunda ya juhudi hizi: ambayo ni kuingiza na kusimika nchini Tanzania, demokrasia ya kweli. Najua bado hatujaweza kuonyesha mafanikio ktk maendeleo ya kweli kiuchumi na kijamii, lakini naamini mchango wa CDM unaanza kudhihirika, na endapo Watanzania wataamua tuchukue dola, basi mambo yatanoga.

Tatu kuhusu kulipwa fidia, nieleze ni kweli kwamba katika miaka yangu sita niliyotumikia CHADEMA kama mwenyekiti taifa, sikulipwa mshahara wowote na sikusaidiwa kodi ya nyumba nilipokuwa naishi Dar es Salaam. Pia nilitoa magari yangu kwa shughuli za chama pale mwanzoni, na wakati chama kilipomudu kunipa gari kwa safari za chama, nililiacha Dar es Salaam kwa mashughuli ya chama ilipokuwa ni lazima nirudi nyumbani kwa mashughuli ya kifamilia.

Nne nieleze kwamba katika utumishi wangu kwa umma (mfano Gavana BoT, Katibu Mkuu, EAC na Waziri wa Fedha nililipwa kiinua mgongo, yaani gratuity) na sasa nalipwa pensheni kidogo kwa kuwa civil servant kwa miaka 7 kabla ya uGavana na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kwa miaka 4. Kwa hiyo huyo mwanaJF aliye pendekeza Chadema inifidie, labda alielezwa juu ya kujitolea kwangu kwa umma na mafao yangu yaliyo kiduchu.

Nilivyoeleza hapo mwanzo, ni furaha kwangu iliyoje kwamba tumeweza kuifikisha CHADEMA hapa ilipo. Itambuliwe pia kwamba, the supreme effort and sacrifice is still to come kama tunavyoelekea 2015. Hata hivyo, endapo uongozi wake utakuwa na uwezo wa kufidia waliowezesha CDM kufika hapo ilipo, bila kuathiri malengo yetu matakatifu, makuu na muhimu, basi iwe hivyo.
 
Vazi la chadema haliendani na demokrasia ya kweli wanaitangaza, naikubali kama chama cha siasa, japo bado sijahama CCM, lakini itasaidia kuchapisha kazi vitumbo vilivyovimbiwa.
nashauri waondoe vazi lililokaa kijeshijeshi au kimapinduzipinduzi, au ki fidelkastro, au ki che, ni maana yangu, kwa vazi hili wataonekana wako kikomunisti zaidi kwa nchi za nje, kama kimujahidina au kiaina ambavyo inatisha kwa usalama.
wapendwa viongozi wa chadema, vaeni mashati ya kawaida au suti ambolo ndio vazi la dunia iliyo staarabika, Tazama viongozi wote wa nchi zenye ustaarabu, china, japan, marekani, ulaya yote, south afrika, kenya na mengineyo.
 
haya mambo ya kuabudu nchi za nje nalo ni gamba pia.
 
Kama unatafuta vazi na si sera PONA ina vazi zuri sana.
 
poleni sana, badu mko nyuma kweli,vazi halina sera? duh, kweli jamii bado sana.
 
Kwa taarifa ya WanaJF, mwaka wa 1994, nilitembelea Washington DC kwa mashughuli binafsi (actually kuhudhuria mahafali ya mwanangu), na nilichukua fursa hiyo kukutana na Watanzania na baadhi yao wakajiunga na CHADEMA. Nikiwa njiani kurudi nyumbani nilikuwa New York pia kwa siku kadhaa na niliweza kuwaridhisha baadhi ya WaTz waliokuwa wanaishi New York kuchukua kadi za CHADEMA.

Itakumbukwa kwamba kulikuwa na tafrani ya aina yake wakati balozi wa Tanzania ktk Umoja wa Mataifa, Bw. Anthony Nyakyi, rafiki yangu wa siku nyingi, aliponikaribisha nyumbani kwake kwa chakula cha jioni. Wizara ya Mambo ya Nje, kwa kukurupuka, ilimwita Nyakyi nyumbani na kukatisha uteuzi wake, licha ya kwamba umahiri wake ulitumiwa na Mwalimu Nyerere ktk juhudi zake za usuluhishi katika migogoro ya nchi za Maziwa Makuu. Baadaye Nyakyi aliteuliwa na Katibu Mkuu wa UN alimteua Nyakyi kuwa mwakilishi wake huko Liberia.

Niliacha tawi la CHADEMA Washington DC, na nakumbuka Daudi Ballali ndiye aliliongoza, na tuliwasiliana kwa muda, nikimpelekea kadi za chama kupitia mwanangu aliyekuwa anaendelea kumalizia masomo yake. Tawi la CHADEMA la Washington DC, linaonekana lilififia baada ya Ballali na Sadikieli Kimaro kuitwa na Rais Benjamin Mkapa kuja kuwa washauri wake wa kiuchumi. Of course, Ballali aliteuliwa Gavana wa BoT, na hangeweza kuendelea kuwa active kama MwanaChadema. Vituko vya huyu ex-mwanaCDM, ambaye ni marehemu sasa, kuhusiana na EPA n.k. ni mambo yanayonifedhehesha mpaka leo.

Nakubaliana na mawazo kwamba wanaCDM waliopo ughaibuni wanaweza kuimarisha Chama kwa kutupa ushauri, na hata wakati nikiwa Mwenyekiti Taifa, CHADEMA tulipokea vifaa kadhaa kama zawadi au michango yao kuimarisha chama. Nakumbuka baadhi ya fax machines na electric type-writers za kwanza Makao Makuu ya Chadema vilikuwa ni vifaa vilivyotolewa na hawa ndugu zetu wanaoishi ng'ambo.

Ningeshauri kwamba utaratibu unaoeleweka ubuniwe na viongozi wa CDM ili WaTz wanaoishi ughaibuni na wanaoamini ktk itikadi na misimamo ya CHADEMA, washirikishwe kikamilifu.

Mzee Mtei kwa hili naomba kutokukubaliana nawe kabisa. Lingekuwa la maana zaidi kama Chadema, tofauti na CCM, ingejikita katika kuimarisha umoja wa Watanzania waliopo ughaibuni kwa kutanguliza utaifa badala ya itikadi. Naamini kwa dhati kuwa kufungua matawi ya vyama nje ya nchi ni upofu uliosababishwa na mfumo mfu chini ya utawala wa chama kimoja.

Kama tulivyoweza kupiga marufuku matawi ya chama makazini, yafaa tuendelee hadi kwa vijana, wazazi na wengineo. Tunashabikia mambo yasiyo na manufaa yoyote kwa jamii katika kujenga utaifa kwani kuna siku tutaanzisha umoja wa wanasoka wa Chadema au umoja wa walaji wa Chadema ! Hizo ni mbinu za kibaguzi za CCM na hazina nafasi Chadema.

Ni mawazo kama hayo yanayowafanya hata wabunge wasahau jukumu lao la kutetea maslahi ya taifa na badala yake kulinda ubinafsi. Tanzania kuna mambo tunayafumbia macho lakini madhara yake huko mbele ya safari ni makubwa mno. CCM inabidi ifanye hivyo kwa sababu hawana nia madhubuti ya kuachia madaraka kwa njia ya amani hivyo silaha yao kubwa ni uchonganishi na ubaguzi.

Natamani CCM wangeturudisha huko huko kuliko kudai walitutoa mbali kumbe tumeganda pale pale kama viwete huku wenzetu wakikata mbuga. Badala ya vijana kujiendeleza kwa bidii katika masomo huko kwa wenzetu, wamekaa kufungua matawi ya CCM, ujinga mtupu. Haya matawi sana sana yanatoa tu hifadhi kwa watoto, wajukuu na washikaji wa mafisadi.
 
Mi tangu mwanzo nimeonyesha kutokubaliana na hoja hii.....
 
Vazi la chadema haliendani na demokrasia ya kweli wanaitangaza, naikubali kama chama cha siasa, japo bado sijahama CCM, lakini itasaidia kuchapisha kazi vitumbo vilivyovimbiwa.
nashauri waondoe vazi lililokaa kijeshijeshi au kimapinduzipinduzi, au ki fidelkastro, au ki che, ni maana yangu, kwa vazi hili wataonekana wako kikomunisti zaidi kwa nchi za nje, kama kimujahidina au kiaina ambavyo inatisha kwa usalama.
wapendwa viongozi wa chadema, vaeni mashati ya kawaida au suti ambolo ndio vazi la dunia iliyo staarabika, Tazama viongozi wote wa nchi zenye ustaarabu, china, japan, marekani, ulaya yote, south afrika, kenya na mengineyo.

Lile ni vazi linalotumika sana na farmers, hata mimi nilikuwa nalo, nyerere alikuwa nalo. Unaboa:lalala:
 
kwangu mimi nikiwa mtanzania nayethamini uhuru wa kutoa mawazo na kuanzisha vikundi, sioni ubaya wa suala hili, naikiwezekana watanzania wote walio nje jiungeni kwa pamoja kuweza kutoa mawazo yenu hasa ya mabadiliko, ili tutokomeze ufisadi kabisa. Naamini wote kwa mamoja tukiungana tutaweza, na kila mmoja akitimiza ajibu wa kutetea raslimali za tanganyika ambazo ndizo zinaliwa na mchwa hawa
 
USA ni heshima kuwa mwanajeshi na viongozi wao wengi ni wanajeshi na jeshi ni kila kitu, wachini ni wakomunist mpaka leo, naona kama umeweka hoja gongana.
AFRIKA KUSINI ZUMA mambo yake uyajui?
mimi sio tatizo la hiyo vazi, kama ni la kikombozi inaleta maana zaidi maana watanzania wanaitaji ukombozi wa fikra zaidi kwa sasa,
kwa mfano kuna wasomi na wanaoka mjini hawa hawabigi kura wansema hawapendi siasa, kuna masikini wanauza kadi za za kupigia kura wakizani watapata nafuu kwa kupewa pesa kidogo, kuna wanaopenda kuva suti kama unavyosema wakati hali ya wenzao ni ngumu,
mimi nadhani washauri ccm waondoe JEMBE NA NYUMBO KWENYE NEMBO YAO WAWEKE (EPA. RICHMOND, IPTL, DOWANS, ROSTAM, NA NYOKA MWENYE MAGAMBA.)

Back
Top Bottom