Tattoo inanikosesha amani

madala mujipa

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,421
Reaction score
864
Amani kwenu,

Wadau nimepata mwanamke ninae taka kuoa kwa maana ya mke wa pili,tatizo kwa haraka haraka alilonalo amejichora tattoo kwenye paja tattoo hiyo ina jina la mwanaume wake aliemuacha na jina lenyewe lipo kwenye paja.

Yaani ni sehemu nyeti na mimi nimefika nataka kuchukua jumla lakini kila nikifiria nakosa amani na mwenye jina lake anaweza kuwa bado ana nguvu na kuweza kutaka kuona jina lake kama bado linadumu.

Nashauri kina dada wakati wa mapenzi yenu kumbukeni kuna kuachana sasa kizazaa kama hiki cha kuolewa na majina ya watu ni hatari.

Wadau nisaidieni ushauri mimi ndio nishaoza lakini nikifikiria jina nakosa amani.
 
Cha msingi je amemfuta moyoni? Unaweza ifuta tattoo Hiyo isionekane, lakini kama bado yupo moyoni mwake ni kazi bure.
Inaweza kuwepo tattoo ila kama hampendi tena, then nafikiri haina madhara.

Cc mshana jr tattoo inamadhara gani? Kiimani
 
hata asingekuwa na tattoo yenye jina la ex wake kama ni mwanamke asiye mtulivu na asiyejitambua angekuwa anapasha kiporo ila kama ameamua kwa dhati kuwa nawe usitie shaka.
 
umewaza vyema mkuu
 
hata asingekuwa na tattoo yenye jina la ex wake kama ni mwanamke asiye mtulivu na asiyejitambua angekuwa anapasha kiporo ila kama ameamua kwa dhati kuwa nawe usitie shaka.
Aksante mkuu
 
Wewe mwenyewe umeshatumika,tena dhairi kabisa alama iko nyumbani,namaanisha kua umeshaoa,.
Wewe maandishi tu inayoonuesha kama alishatumika unaumia nini?
 
Wewe mwenyewe umeshatumika,tena dhairi kabisa alama iko nyumbani,namaanisha kua umeshaoa,.
Wewe maandishi tu inayoonuesha kama alishatumika unaumia nini?
kutumika si tatizo asije akatumika wakati yupo ndani kwangu
 
Mwanamke anayejielewa ambaye hata kesho Na kesho kutwa wewe unaweza ondoka na akaendesha familia bila tatizo hawezi kua na akili kama za huyo wako anayewaza kuchora tatoo huko sehemu nyeti!!

Hebu jiulize anafunua mapaja yake kwa ajili ya huo ujinga atakuwa na akili za kuwaza maendeleo saa ngapi?

Anyway kama unataka huyo Mwanamke for commercial purposes mchukue ila kama unataka wife material wa kujenga nae strong family huyo sio!!
 
Mkuu nitukane tu sitakuwa na wasi ila ikiwa unaemke wako tulia nae, roho imeshasita atakuongezea mzigo wa matatzo huyo. Ukiona ameachwa kuna sababu na huenda hicho kinachofanya roho isite ikawa sababu yenyewe
 
ushauri mzuri maamuzi magumu
 
Mkuu nitukane tu sitakuwa na wasi ila ikiwa unaemke wako tulia nae, roho imeshasita atakuongezea mzigo wa matatzo huyo. Ukiona ameachwa kuna sababu na huenda hicho kinachofanya roho isite ikawa sababu yenyewe
Nimekusoma mkuu
 
Usijudge vibaya wengine wanadanganywa na wanaume wanafanya kwa mapenzi ila sio kwa matakwa yao mwisho wa siku wanaambulia kuachwa
 
Wanawake wengine nao jamani,kwani Tattoo lazima? wengine hata maana yake hawajui wala hawafikirii mara 100 kabla haja chora,mie Hubby anisamehe tuu bure anataka Hinna ntaandika jina lake mwili mzima ila sio tattoo..
 
Mkuu ukiona vipi achana nae....

Picha tafadhali kama ipo
 
Mkuu mvizie akiwa amelala na wewe umtie chapa yako ya pasi hapo hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…