Tatizo si vyeti- ni kuelimika

Tatizo si vyeti- ni kuelimika

Watanzania acheni umbea na uongo fanyeni kazi " tunahitaji somo la" CHANGE MANAGEMENT".
 
Nchi gan inaendeshw na watu ambao hawakwenda shule?? Haya maajabu nayaona tanzania tu ya ambao hawajaenda shule kuonekana ni wazuri kuliko ya walioenda shule,jamani tuacheni kujipendekeza kiasi hicho,hilo ni kosa tu tayari mlikubali,bashite amefoji tu msitetee mambo ya ovyo ovyo haipendezi jamani,

Dunia yeyote inaongozwa na wasomi ili mambo yakae sawa,ndiyo maana zikawepo shule ili watu waelimike, ndiyo maana hata elimu ya rushwa inafundishwa toka shule ya msingi ili mtu aelimike na aelewe madhara ya rushwa,sasa mtu asipojifunza hili toka mwanzo ataelewaje madhara yake?? shule ni ya muhimu tu,mwalimu nyerere ndiyo maana alianzisha UPE ili kupigana na madhari ya kutokujua kusoma na kuandika,

Mwizi hana shule anaweza akawa hajaenda shule na anaweza akawa na elimu yake ya kutosha na bado akawa mwizi,mtoa mada usitetee issue ya vyeti kwa mhusika makonda,issue ya vyeti iko pale pale anatakiwa afanyiwe uhakiki tu kama watu wengine na awajibishwe kama wengine tu.
 
nani kaenda shule tanzania?, angalia nchi yako ilivyo miaka mingapi sasa ya uhuru? bado umasikini ni tatizo, Maji ya bomba ni machafu, miundo mbinu mibovu, foleni kila dakika, vumbi kila sehemu, watu hawakusoma walio soma elimu mbovu hakuna wanachofanya ni wizi tu.

Raisi wa awamu ya nne kasoma, kafanya nini, awamu ya tatu kafanya nini? awamu ya pili kafanya nini?. kipindi chote hiki kulikuwa hakuna uadilifu, wizi, rushwa, madawa ya kulevya ,WOTE WAMEIBA WAMEMALIZA MADALAKA YAO. MIMI NA WEWE, NA MASIKINI WENGI WAKITANZANIA TUNA NINI, TUNANUFAIKA VIPI NA NCHI YETU.
 
Back
Top Bottom