Tatizo nini, mzazi mwenye familia kula migahawani au vibanda vya chipsi na hayupo mbali na nyumbani?

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,451
9,373
Wadau niende moja kwa moja kwenye mada hii inawahusu wana familia hususani wana ndoa hii tabia ipo mijini na vijijini

Unakuta baba au mama lakini mara nyingi kina baba, ana familia mke na watoto na hayupo mbali na nyumbani au anatoka nyumbani kabisa anafika mgahawani anagiza chakula, au kwenye banda la chips anagiza chipsi na mishikaki kadhaa ana kula, ukifutilia nyumbani mkewe yupo watoto wapo tatizo nini, uchoyo, ujinga au uroho?

Familia zingine utaona mtu na mkewe wameongozana kwenye mabanda ya chips na nyama choma ukiuliza vipi watoto utasikia aaah bwana kuna mboga imepikwa uko haipandi kabisa ajabu unaona mkewe yupo naye ila watoto au dada wa kazi wamewaacha nyumbani
 
Kwa Mwanaume inatakiwa ule mahali ndio uende nyumbani........

Na ukitengewa chakula usimalize.....Kama nyama wape watoto....Sasa ikiwa haujala nje hutaweza ..

Vilevile mke anaweza kukukaraisha ukajikuta huli ... Sasa Kama hukujiongeza ukala kabla utapata vidonda vya tumbo bure ...
 
Huo ni upumbavu kama upumbavu mwingine.
Ni kukosa hekima.
Malipo huwa ni hapa hapa dunian, na hajui causes za Kisukari (Diabetes mellitus)

Ukishakipata kisuri ndo unakuja kujua sasa husababishwa na nn??
 
Tumbo nalo huwa halina break, kama watoto hawapo karbu si utajikuta unakimaliza chote tena.
Kwa Mwanaume inatakiwa ule mahali ndio uende nyumbani........

Na ukitengewa chakula usimalize.....Kama nyama wape watoto....Sasa ikiwa haujala nje hutaweza ..

Vilevile mke anaweza kukukaraisha ukajikuta huli ... Sasa Kama hukujiongeza ukala kabla utapata vidonda vya tumbo bure ...
 
Huo ni upumbavu kama upumbavu mwingine.
Ni kukosa hekima.
Malipo huwa ni hapa hapa dunian, na hajui causes za Kisukari (Diabetes mellitus)

Ukishakipata kisuri ndo unakuja kujua sasa husababishwa na nn??
Kuna kisukari Cha kurithi. Na sio wore wanao kula chips wanapata kisukari.
 
Mzazi wa hivyo ni bahili, hataki kutumia gharama kubwa kula na watoto; au ni mchoyo kidogo alichonacho hataki kushare; au ni kiki na yeye aonekane yupo mjini anamudu kula chips bandani.
 
Kisuri cha kurithi huanza kuonesha dalili utotoni.
Lakini ukiona mtu kapata kisukari ukubwani jua katengeneza yeye mwenyewe.

Na tambua kua ukizidisha intake ya chakula bila mazoezi ya kuendana na chakula unachokula lazima kilo za mwili kuwa juu na ndio unavozidi kujiweka kwenye risk ya kupata kisukari.
Kuna kisukari Cha kurithi. Na sio wore wanao kula chips wanapata kisukari.
 
Ubinafsi tu hakuna kingine, Binadamu wengi hawastahili kuwa na Familia wala kulea watoto, hawana huo uwezo ila wanalazimisha na wanachokifanya ni kuharibu watoto wanaowalea, matokeo yake hao watoto wakikuwa na wao wanaendeleza ubinafsi kwa familia watakazoanzisha na kuendelea bila ukomo, ni laana!
 
Kwa nini ubakishe ulazima huu unayoka wapi, nyama watoto si wanapewa zao na most of times wanakuwa wameshakula.


 
REJESHO HURU,
Mtafute mhusika umuulize ili akambie tatizo nini.

Watz wengi wanapenda taarifa za udaku na umbea umbea. Wanaposikia kitu huwa ni wagumu sana wa kuwa face wahusika na kuwauliza ukweli wa kile walichosikia au kuambiwa.
 
Mtafute mhusika umuulize ili akambie tatizo nini.

Watz wengi wanapenda taarifa za udaku na umbea umbea. Wanaposikia kitu huwa ni wagumu sana wa kuwa face wahusika na kuwauliza ukweli wa kile walichosikia au kuambiwa.
Unataka tuzungumzie mambo ya peponi wakati hatujui, tunazungumzia uhalisia wa maisha
 
REJESHO HURU, Ingawa wengine watasema ni upumbavu, lakini kuna siri nyingi zimefichika kwenye ndoa. Tatizo mojawapo laweza kuwa MAPISHI, hili ni janga la kitaifa siku hizi. Zamani chakula cha nyumbani kilikuwa kitamu kweli kweli, baada ya kuoa chakula cha mgahawani hadi mke anakitamani. Kwa msingi huu utakuta mwanamume anakula nyumbani kidogo tu kuzuga, kwa sababu hawezi kumweleza wife, kisha anakwenda kupata chakula kitamu mahali pengine.

Kama ukitaka vita kuu ya tatu ya dunia, jaribu kumkosoa mkeo kuhusu mapishi, ni mojawapo ya dhambi kubwa zaidi kwenye ndoa. Sasa wanaume wasiotaka maneno wataondoka kimya kimya na kujiridhiasha sehemu nyingine. Hii ni kulinda mahusiano mazuri kwenye ndoa.
 
Dah hapa kila mtu atawashambulia wababa kwa kutuita wabinafsi, wachoyo, wahuni n.k lakini ukweli ni kwamba tabia za hawa wakezetu tunazijue wenyewe.

Kitanda usicho lalia hujui kunguni wake utalaumu tu lakini hujui chanzo ni nini.
We unadhani mtu atafanya hivo bila sababu kweli.

Utakuta mke ni mjuaji sana haambiliki, Mume anajitahidi kutoa pesa ya matumizi nyumbani kukidhi mahitaji ya familia, lakini masikini utakuta mke kazi ya kuchukua hizo hela kupeleka kwenye vikoba nyumban inapikea tembele kila siku, halafu hizo hela zenyewe za vikoba hazionekani Cha maana anacho fanyia.
Toa hela utoavyo lakini nyumbani kila siku ni dagaa tu, hela zinaenda kwenye michango ya harusi na shida mamake huko nyumbani kwao.
Mume inafika mahala anachoka kumtimua mke si vema anahofia kutesa watoto basi ni tabu tupu, mwisho mtu anaona akitoka kazini apitie mahala ale kabisa ndo arudi nyumbani.

Hamujui tu kiasi gani watu wanateseka wakuu.
 
Back
Top Bottom