Tatizo ni sisi wenyewe

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
Mimi ni bwana mdogo tu sijaona mengi kbsaa kuliko kaka na baba zangu lakini katika hichi kipindi kidogo nilicho zawadiwa uhai na kuishi huku na kule pamoja na kuona haya na yale nmekuwa nikijiuliza kwanini mataifa haya ya Africa na hasa Taifa langu hatupigi hatua na sio kwenye eneo moja ni maeneo yote hata bhasi tungekuwa tunajivunia eneo fulani lakini ni maeneo yote sisi washika mikia.

Africa yote inakaribia kufanana kwa hali za maisha katika kila nyanja, utawondoa waarabu na SA.

Katika kujiuliza kwangu huku nikapata nafasi ya kusoma baadhi ya vitabu vinavyo zungumzia maendeleo na mabadilko katika jamii nikapata kitu, waandishi wanasema maendeleo ya jamii fulani yanategemea na mizozo na migogoro ya ndani ya nafsi ya kila mwanajamii ya kutokubaliana na hali fulani mizozo hii ndani ya nafsi ndo inayopeleka mabadiliko aidha kwa kuungana pamoja watu wenye mgogoro mmoja au mtu kupambana mwenyewe, umeme na gunduzi mbali mbali kutoka kwa wanasayansi ilitokana na nafsi ya mtu kutokubaliana na giza au jambo fulani na kupelekea kufanya majaribio na tafiti bila kuchoka hadi matokeo yalipo onekana.

Jamii ili itoke hatua moja kwenda nyingine inahitaji wana jamii walio na migogoro ndani ya nafsi zao ya kutokubaliana na hali au changamoto fulani, harakati za kuondoa migogoro hii ndani ya nafsi ndio iliyofanya mapinduzi ya viwanda kuja katika mataifa ya ulaya lakini migogoro hii ndio imefanya mataifa ya uchina na baadhi ya Asia kupiga hatua na kukua sana kiuchumi kwasababu kila mwana jamii ana halakatii za kuhakikisha anatatua changamoto fulani au anapiga hatua fulani kuondoa kinachomsumbua nafsini mwake.

Ukiwa na mgogoro ndani ya nafsi juu ya umaskini na njaa ulizonazo tafsiri yake utauchukia na utahakikisha kila hatua unayopiga ufanyi makosa yatakayofanya uwe maskini wewe na kizazi chako. Hivyo ndivyo mataifa yaliyo na maendeleo yaliendelea na ndivyo mataifa yaliotuzidi kila kitu watu wake walivyo.

Hitimisho:
Baada ya kuyajua hayo nilyoyasema hapo juu nikakubaliana na halmashauri ya kichwa changu kuwa waafrika hatuna migogoro ya ndani ya nafsi inayotupeleka kuwa kama simba windoni kutatua na kuondoa shida na changamoto zinazotuletea shida na migogoro nafsini.

Sisi ni watu wa kuridhika na kila hali na kumwachia Mungu ambaye alishatupa utashi na akili ili tutumie kutatua ya duniani sisi atutumii tunamuachia yeye. Sisi tuko hapa sio kwa bahati mbaya au kwasababu ya serikali zetu tupo hapa tulipo kwasababu ya tulivyo tatizo ni sisi kuanzia kwa mtu mmoja, familia,jamiii mpaka ngazi ya nchi.

Serikali isiyofaa aiwezi kuongoza wananchi wenye migogoro nafsini mwao juu ya uonevu na umaskini na shida nyingine ndomana Donald Trump aliongoza marekani miaka mnne na sio nane. Africa pekee ndio utakutana na kijana asiye na kipato chochote wala assets yoyote na ana watoto anaokwambia aliwazaa bahatii mbayaa wanawake wenyewe aliozaa nao awaelewi ilikuwa ajali tu kazini.

Africa kukutana na kijana unaemuliza kwanini unasoma kozi hii na akakujibu nilichaguliwa tu sio tatizo, ukimuuliza umejipangaje na changamoto ya ajira utajibiwa serikali ndo miyeyusho lakini Mungu ni mwema hataniacha niteseke.

Kwa nchi yenye watu wa aina hii wasio na migogoro ya ndani inayowapeleka kutafuta majibu waondokane na migogoro iyo hata malaika waongoze serikali amna hatua itapigwa.
 
Mimi ni bwana mdogo tu sijaona mengi kbsaa kuliko kaka na baba zangu lakini katika hichi kipindi kidogo nilicho zawadiwa uhai na kuishi huku na kule pamoja na kuona haya na yale nmekuwa nikijiuliza kwanini mataifa haya ya Africa na hasa Taifa langu hatupigi hatua na sio kwenye eneo moja ni maeneo yote hata bhas tungekuwa tunajivunia eneo fulani lakini ni maeneo yote sisi washika mikia. Africa yote inakaribia kufanana kwa hali za maisha katika kila nyanja, utawondoa waarabu na SA.
Katika kujiuliza kwangu huku nikapata nafasi ya kusoma baadhi ya vitabu vinavyo zungumzia maendeleo na mabadilko katika jamii nikapata kitu, waandishi wanasema maendeleo ya jamii fulani yanategemea na mizozo na migogoro ya ndani ya nafsi ya kila mwanajamii ya kutokubaliana na hali fulani mizozo hii ndani ya nafsi ndo inayopeleka mabadiliko aidha kwa kuungana pamoja watu wenye mgogoro mmoja au mtu kupambana mwenyewe, umeme na gunduzi mbali mbali kutoka kwa wanasayansi ilitokana na nafsi ya mtu kutokubaliana na giza au jambo fulani na kupelekea kufanya majaribio na tafiti bila kuchoka hadi matokeo yalipo onekana.
Jamii ili itoke hatua moja kwenda nyingine inahitaji wana jamii walio na migogoro ndani ya nafsi zao ya kutokubaliana na hali au changamoto fulani , halakatii za kuondoa migogoro hii ndani ya nafsi ndio iliyofanya mapinduzi ya viwanda kuja katika mataifa ya ulaya lakini migogoro hii ndio imefanya mataifa ya uchina na baadhi ya Asia kupiga hatua na kukua sana kiuchumi kwasababu kila mwana jamii ana halakatii za kuhakikisha anatatua changamoto fulani au anapiga hatua fulani kuondoa kinachomsumbua nafsini mwake.
Ukiwa na mgogoro ndani ya nafsi juu ya umaskini na njaa ulizonazo tafsiri yake utauchukia na utahakikisha kila hatua unayopiga ufanyi makosa yatakayofanya uwe maskini wewe na kizazi chako. Hivyo ndivyo mataifa yaliyo na maendeleo yaliendelea na ndivyo mataifa yaliotuzidi kila kitu watu wake walivyo.
Hitimisho:
Baada ya kuyajua hayo nilyoyasema hapo juu nikakubaliana na halmashauri ya kichwa changu kuwa waafrika hatuna migogoro ya ndani ya nafsi inayotupeleka kuwa kama simba windoni kutatua na kuondoa shida na changamoto zinazotuletea shida na migogoro nafsini. Sisi ni watu wa kuridhika na kila hali na kumwachia Mungu ambaye alishatupa utashi na akili ili tutumie kutatua ya duniani sisi atutumii tunamuachia yeye. Sisi tuko hapa sio kwa bahati mbaya au kwasababu ya serikali zetu tupo hapa tulipo kwasababu ya tulivyo tatizo ni sisi kuanzia kwa mtu mmoja, familia,jamiii mpaka ngazi ya nchi. Serikali isiyofaa aiwezi kuongoza wananchi wenye migogoro nafsini mwao juu ya uonevu na umaskini na shida nyingine ndomana Donald Trump aliongoza marekani miaka mnne na sio nane. Africa pekee ndio utakutana na kijana asiye na kipato chochote wala assets yoyote na ana watoto anaokwambia aliwazaa bahatii mbayaa wanawake wenyew aliozaa nao awaelewi ilikuwa ajali tu kazini, Africa kukutana na kijana unaemuliza kwanini unasoma kozi hii na akakujibu nilichaguliwa tu sio tatizo, ukimuuliza umejipangaje na changamoto ya ajira utajibiwa serikali ndo miyeyusho lakini Mungu ni mwema hataniacha niteseke.

Kwa nchi yenye watu wa aina hii wasio na migogoro ya ndani inayowapeleka kutafuta majibu waondokane na migogoro iyo hata malaika waongoze serikali amna hatua itapigwa.
Kwani Afrika ina mikia mingapi?
 
Nafikiria kuondoka kabisa Tanzania kuvua hii Laana ya utanzania.
Tatizo alikimbiwi huko unakokimbilia kuna watu waliumia kupaona ivyo palivyo 😁 unapaswa kuumia hapa kwa ajili ya wengine kesho acha ubinafsi tengeneza nafasi ya wengine kuishi vizuri Kesho kwenye mazingira haya mabaya
 
Tatizo alikimbiwi huko unakokimbilia kuna watu waliumia kupaona ivyo palivyo unapaswa kuumia hapa kwa ajili ya wengine kesho acha ubinafsi tengeneza nafasi ya wengine kuishi vizuri Kesho kwenye mazingira haya mabaya
Hakuna uzalendo kwenye umaskini na hakuna kuumia kwa ajili ya wajinga walio ridhika na umaskini wao.

Watanzania wengi wamesha ridhika na umaskini wao na wala hawako tayari kujikomboa.

Kila kitu ni hovyo hovyo tu.
Siasa za Hovyo, Elimu ya Hovyo, huduma za afya duni, miundombinu hovyo hovyo tu.

Bora kuepusha kizazi changu na hii laana ya Utanzania.
 
Unavyoona England viwanja vizuri vya mpira ,hoja Kwa hoja kuna watu waliumia Sasa wewe huchukui hatua unakaa kimya watoto wako watakuja kukuchukia lakini Leo wazungu watoto wao wanafurahia Kwa sababu Babu zao waliumia CHUKUA HATUA
 
Tanzania yenye miaka 62 ya uhuru wa kujitawala yenyewe, Bado inasumbuliwa na Umaskini licha ya kuwepo kwa rasilimali nyingi ambazo zingeweza kuleta maendeleo,

Unadhani kuna watu waliumia kweli kwa ajili ya nchi yao?

Au wali jinufaisha wao binafsi na vizazi vyao?

Tanzania hii, Kuna mifumo mibovu kila sehemu kiasi kwamba kuleta haya maendeleo bila mabadiliko ya mifumo haiwezekani.

Tanzania yenye miaka 62 ya uhuru bado ni ombaomba misaada na mikopo!!

Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Back
Top Bottom