Tatizo ni Katiba ya 1977, Wananchi au Viongozi?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,192
1,971
Tuliaminishwa kuwa suala la ufisadi Tanzania mwarobaini wake ulikuwa ni Katiba Mpya! Wengine walidai kwamba Katiba ya Mwaka 1977 ina mapungufu 99. Hizo zilikuwa ni enzi za "Maisha Bora kwa kila Mtz" ambapo ufisadi ulifikia kiwango cha kutisha sana! Hadi sasa JPJM anazoa lundo la takataka zilizosababishwa na uongozi uliopita!
Kinachoshangaza ni pale Katiba ya 1977 ilisemekana mapungufu yake yalileta ufisadi na Katiba hiyo hiyo inatumika kufagia ufisadi huo huo!
Je, tuseme kweli tatizo ni Katiba ya 1977 au tatizo ni Wananchi au ni Viongozi?
Mawazo yenu wadau maana Katiba ni ile ile, Wananchi ni wale wale, Chama ni kile kile (CCM), ila tu Uongozi ndio umebadilika!
Tukiijua SIRI hii hatutayumba tena katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa katika mstari ulionyooka kila wakati!
 
Back
Top Bottom