Tatizo la wanawake kushindwa kushika mimba linazidi kuwa kubwa

Vito Corleone

JF-Expert Member
Apr 4, 2023
2,229
4,781
Niaje wakuu kumekuwapo na wimbi la wanawake kutoshika mimba mitaani na hata wakishika zinatoka, wataalamu wamekaa kimya ila it's gonna be a disaster soon. Nimeishi na wanawake ambao wamekuwa wakiweka vijiti kuzuia ujauzito, ila kwa nyakati tofauti nimeona mabadiliko ambayo si mazuri, mizunguko yao ilivurugika na kushika mimba ya pili ni shida kinoma.

Ukisikiliza wataalamu wanasema P2 ndio chanzo, ila hizi njia za kuzuia mimba ikiwemo vijiti mmefanyia utafiti wa kutosha kiasi gani?

Maana dalili ni nyingi, kila mtu sasa hivi analalamika kisamaki, haya mambo hayakuwa miaka iliyopita. Watu tunasingizia dada zetu kuwa vicheche kumbe ni haya mambo ya Kizungu.

I need answers.
 
Kuna kansa ya shingo ya kizazi pia imeibuka miaka ya hivi karibuni. Wanawake kuwa na vitambi mpira na kasi ya wanawake kulazimika kutolewa mfuko wa uzazi, yote haya huenda yakawa na chanzo kimoja chenye vina na matangazo ya (p2, uzazi wa mpango n.k) kwa hisani ya watu wa ...
 
Mkuu uzazi wa mpango hauna tatizo kabisa kama utafuata maelekezo. Sema tatizo linakuja kwamba kuna baadhi ya hizo njia baada ya kuacha kuzitumia inakuchukua muda mrefu kushika ujauzito. Hii ni kutokana kwamba inabidi iishe kabisa mwilini mwako ili mzunguko wako urudi normal.

Hapa ni mtu tu anapaswa kujua atumie uzazi wa mpango upi na malengo yake ni yapi. Na pia baada ya kuacha kutumia ni vyema akutane na madaktari wa wanawake ili waweze kumsaidia ushauri.

Tatizo watu hawana elimu ya kutosha anataka akiacha kutumia leo mwezi huo huo au mwezi ujao ashike ujauzito. Ndio inawezekana ila ni kutokana na aina ya mpango ulioutumia na umeutumia ndani ya muda gani.

Suala la kuharibika kwa mimba hilo ni kawaida. Na hapa unaweza ukawa haujafanya kitu chochote kusababisha. Unaambiwa asilimia 10 hadi 20 ya mimba zote huwa zinaishia kwenye miscarriage na asilimia nyingi anayepata hizo miscarriage anakuwa hajasababisha ni mambo ya chromosomal abnormalities na umri pia.
 
Niaje wakuu kumekuwapo na wimbi la wanawake kutoshika mimba mitaani na hata wakishika zinatoka, wataalamu wamekaa kimya ila it's gonna be a disaster soon. Nimeishi na wanawake ambao wamekuwa wakiweka vijiti kuzuia ujauzito, ila kwa nyakati tofauti nimeona mabadiliko ambayo si mazuri, mizunguko yao ilivurugika na kushika mimba ya pili ni shida kinoma.

Ukisikiliza wataalamu wanasema P2 ndio chanzo, ila hizi njia za kuzuia mimba ikiwemo vijiti mmefanyia utafiti wa kutosha kiasi gani?

Maana dalili ni nyingi, kila mtu sasa hivi analalamika kisamaki, haya mambo hayakuwa miaka iliyopita. Watu tunasingizia dada zetu kuwa vicheche kumbe ni haya mambo ya Kizungu.

I need answers.
Kama kuna mwenye tatizo hilo mlete kwangu, nitamfanya kwa malipo kidogo. Nikigusa tu kitu na box
 
Umalaya

Wanawake wamekuwa na mabwana na madanga wengi na wote anafanya nao ngono

Imagine manzi ana madanga 7 kwa mwezi atakuwa amefanya ngono mara ngapi

Mwisho wa siku analazimika kutumia hizo mbinu za kuzuia mimba. Matokeo kushika mimba inakuwa changamoto

Amini mwanamke akiwa na mtu mmoja hahitaji hizo mambo maana kalenda tu na labda condom inatosha
 
Tatizo linaanzia kwa Wanaume sisi pia tuna shida.

Nikirudi kwa hawa wadada.. wengi wanatumia mavitu mengi sana kuanzia dawa za kuzuia au kutoa mimba, dawa za kubana uchi na kusafisha.

Hapo sijagusia Shisha na ulevi, Sonona na Magonjwa ya Afya ya akili.
 
Niaje wakuu kumekuwapo na wimbi la wanawake kutoshika mimba mitaani na hata wakishika zinatoka, wataalamu wamekaa kimya ila it's gonna be a disaster soon. Nimeishi na wanawake ambao wamekuwa wakiweka vijiti kuzuia ujauzito, ila kwa nyakati tofauti nimeona mabadiliko ambayo si mazuri, mizunguko yao ilivurugika na kushika mimba ya pili ni shida kinoma.

Ukisikiliza wataalamu wanasema P2 ndio chanzo, ila hizi njia za kuzuia mimba ikiwemo vijiti mmefanyia utafiti wa kutosha kiasi gani?

Maana dalili ni nyingi, kila mtu sasa hivi analalamika kisamaki, haya mambo hayakuwa miaka iliyopita. Watu tunasingizia dada zetu kuwa vicheche kumbe ni haya mambo ya Kizungu.

I need answers.
Katika mpango mzungu amefanikiwa kumaliza uzao wa mtu mweusi na afya zetu nikupitia hizi dawa za uzazi wa mpango!
Kwanza maambukizi ya VVU hupatia nafasi hapo, ile no hormone ikishaingia kwenye mfumo wa damu kuisha sio leo!
 
Back
Top Bottom