Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,833
- 2,790
Pamoja na michango ya JF wenzangu hapo juu na wale watakao fuata nami ningependa kutoa mawazo yangu: Kuwa tatizo la Mume na Mke kutofanikiwa kupata watoto liko miongoni mwao. Moja ambalo linaweza kuwa ndilo tatizo ingawa Mume anatema "cheche" kama kawaida ni kuwepo kwa MAKOVU yanayotokana na magonjwa ya zinaa kama vile kaswende ama gono. Magonjwa haya huathiri kuta au mrija unaosafirisha mbegu kutoka katika korodani. Ikiwa kingo za kuta katika mirija hii zilisha wahi kukumbwa na magonjwa niliyotaja hapo juu basi huacha makovu ambayo wakati huu yana sababisha mikia ya mbegu za mwanaume ikijigonga katika kingo hizo inakatika na kusababisha kutokwenda kwa speed kama inavyotakiwa. Hali hii husababisha mbegu kufa muda wake ukifika maana zinakuwa zimechelewa kuivisha yai ambalo linakuwa likisubiri kuivishwa na mbegu ya kiume. Vivyo hivyo kwa mwanamke wakati yai likijaribu kutoka eneo lake kwenda "sebuleni" kusubiri mbegu ya kiume linakwama katika mirija ya falopian tube aidha kwasababu imeathirika kwa sababu ya magojwa hayo ama imebana kwasababu mbalimbali. Ushauri wangu kama walivyosema wenzangu ni kwenda HOSPITAL kupima utafurahi ukiambiwa tatizo lako limekwisha mara utakapo chukua umamuzi huu MUHIMU.