Tatizo la PayPal Refunds kwenye CRDB Account

Tatizo la PayPal Refunds kwenye CRDB Account

Brakelyn

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2009
Posts
1,181
Reaction score
521
Habari zenu wakuu. Nahitaji msaada kutoka kwa wale wazoefu wa internet transactions.

Nimekuwa nikifanya purchases online either kununua bidhaa au kulipia huduma mbali mbali kwa muda wa miaka 6 sasa toka 2009. Benki yangu ni CRDB na natumia Debit card ya VISA. Nilijiunga na PayPal na kuverify account yangu so huwa nafanya malipo kiusalama zaidi kupitia PayPal.

Mara nyingi ninapofanya malipo ya bidhaa au kulipia huduma huwa napokea bidha zangu successfully na hata nisipozipokea huwa napata refunds kupitia PayPal.

Mwaka juzi nimegudua kuwa kuwa baadhi ya Refunds zangu huwa haziingii kikamilifu kama zinapotoka. PayPal huwa wanarefund kiasi kile kile cha fedha kilichokatwa kwenye account, na kwa kutumia Exchange Rate ile ile ya original transaction. Kuna baadhi ya Refunds zinaingia kikamilifu na zingine zinarudi zimekatwa.

Huu hapa mfano wa transaction ambayo haikurudi kikamilifu. Chini yake ni email ya PayPal wakinitaarifu kuwa wameRefund pesa yangu in full. Original transaction nililipa 2,170,053.72/= na baada ya kupata Refund zikaingia 2,021,349.38/= tu. Hapa Imekatwa almost 150,000/= kirahisi kabisa.

1.jpg

2.jpg

Untitled.jpg

hii hapa refund transaction iliyoingia kikamilifu. Tarehe 10 Nov, 2014 kiasi cha shilingi 31,907.76 kilikatwa na tarehe 18 Dec, 2014 nikapokea Refund kiasi hicho hicho cha 31,907.76/=. Sasa sielewi kwanini refund zingine zinakatwa, zingine hazikatwi na zingine haziingizwi kabisa.

View attachment 223565

View attachment 223568

nilienda CRDB nikawaeleza tatizo langu wakaliona na waliniambia niandike barua watashughulikia swala langu. Niliandika barua na kuacha contacts ili wanipatie feedback lakini mpaka leo hii sikuwahi kujua ni wapi ziliibiwa.

Niliwaandikia PayPal kuwataarifu kuwa refund zangu zinaingia zikiwa pungufu na walinijibu kuwa wao huwa wanarudisha kiasi kile kile kwenye VISA Card iliyotumika kufanya original transaction kwahiyo niendelee kufuatilia na Bank yangu.

Nataka kujua kama wenzangu mnaofanya online transactions mnakumbana na kitu kama hiki au inakuaje? Pia nafikiria kuihama CRDB nifunge account yangu nitafute Bank nyingine ambayo haina magumashi.

Shukrani..
 
heri yako refund zinaingia, wengine hatuzioni hata hizo nusu, na huduma kwa wateja ni sifuri...WIZI MTUPU!
 
Mkuu mimi nadhani uende cRDB hq second floor uliza idara inayohusika na mambo ya kadi. Au Tuma email CRDB customer care Mkuu! Hili ni tatizo DOGO sana
 
heri yako refund zinaingia, wengine hatuzioni hata hizo nusu, na huduma kwa wateja ni sifuri...WIZI MTUPU!

Inasikitisha sana mkuu, miezi miwili iliyopita nilipokea refund kwa transactions 5, kati ya hizo tano ni moja tu ndio iliyorudi in full. Zingine zote mpaka sasa hazijarudi kabisa.

Niliwafuata CRDB wiki iliyopita lakini habari ni ile ile, kuandika barua na kusubiri. Nafkiri kuna idara ndani ya crdb inayohusika na hizi internet transactions na ndio wanaobana pesa zetu..
 
What i understand is this PayPal Hawana wakala here in Tanzania so hatuwezi kureceive payment WHY Our banks hawaja jiregister na Paypal So tunaweza kutuma tuu Na if you're money refunded back on your PayPal account Dont withdrawal it.

Ingia kwa website fungua payoneer register with them It will take yu karibia miezi miwili kupata card yao ya Payoneer master card
After hapo unauwezo wa kuhamisha pesa zako From paypal account to payoneer ambapo unaweza kuzitoa katika ATM mashine yeyote inayokubali mastercard

Natumaini umenielewa
 
Mkuu mimi nadhani hapa Siyo sehemu sahihi ya kutatua tatizo lako, Naomba uende cRDB hq second floor uliza idara inayohusika na mambo ya kadi. Au Tuma email CRDB customer care Mkuu! Hili ni tatizo DOGO sana
Sipo Dar nipo mkoani, nimeenda mara nyingi sana crdb headquarter, Arusha Branch, nimewaeleza yote lakini sikuwahi kupata ufumbuzi wa tatizo langu. Unanishauri nifunge safari hadi makao makuu Dar??
 
What i understand is this
PayPal Hawana wakala here in Tanzania so hatuwezi kureceive payment WHY
Our banks hawaja jiregister na Paypal
So tunaweza kutuma tuu
Na if you're money refunded back on your PayPal account
Dont withdrawal it
Ingia kwa website fungua payoneer register with them
It will take yu karibia miezi miwili kupata card yao ya
Payoneer master card
After hapo unauwezo wa kuhamisha pesa zako
From paypal account to payoneer ambapo unaweza kuzitoa katika ATM mashine yeyote inayokubali mastercard
Natumaini umenielewa

Unachozungumzia ni kitu tofauti, hapa inaongelewa refund kwenda kwenye card yako.
 
inasikitisha sana mkuu, miezi miwili iliyopita nilipokea refund kwa transactions 5, kati ya hizo tano ni moja tu ndio iliyorudi in full. Zingine zote mpaka sasa hazijarudi kabisa. Niliwafuata CRDB wiki iliyopita lakini habari ni ile ile, kuandika barua na kusubiri. Nafkiri kuna idara ndani ya crdb inayohusika na hizi internet transactions na ndio wanaobana pesa zetu..

kaka mimi nilishapoteza mara nne, jumla karibia 3M, niko mkoani....nachojibiwa ni "tutajuaje kama kweli pesa umerudishiwa?"......"kama hao paypal wamekudanganya?"...fk!
 
What i understand is this
PayPal Hawana wakala here in Tanzania so hatuwezi kureceive payment WHY
Our banks hawaja jiregister na Paypal
So tunaweza kutuma tuu
Na if you're money refunded back on your PayPal account
Dont withdrawal it
Ingia kwa website fungua payoneer register with them
It will take yu karibia miezi miwili kupata card yao ya
Payoneer master card
After hapo unauwezo wa kuhamisha pesa zako
From paypal account to payoneer ambapo unaweza kuzitoa katika ATM mashine yeyote inayokubali mastercard
Natumaini umenielewa
mkuu nimekuelewa, lakini kama nilivyosema hapo awali, kuna transactions zinaingia in full bila shida yoyote na zingine haziingii kabisa na pia zingine zinaingia kwa kukatwa. Sipo na Statement ya mwezi uliopita inayoonyesha moja ya transaction refund iliyoingia in full, nitaitoa alafu niweke hapa uone. Nafkiri PayPal haina shida na bank accounts zetu, tatizo ni loyalty ya wafanyakazi kwenye benki zetu..
 
What i understand is this PayPal Hawana wakala here in Tanzania so hatuwezi kureceive payment WHY Our banks hawaja jiregister na Paypal So tunaweza kutuma tuu Na if you're money refunded back on your PayPal account Dont withdrawal it.

Ingia kwa website fungua payoneer register with them It will take yu karibia miezi miwili kupata card yao ya Payoneer master card
After hapo unauwezo wa kuhamisha pesa zako From paypal account to payoneer ambapo unaweza kuzitoa katika ATM mashine yeyote inayokubali mastercard

Natumaini umenielewa

Dragondreamx ushauri wako mzuri sana, hasa kuhusu kufungua payoneer acc mimi nimeshafungua acc kwao, ila mbona inachukua muda mrefu kupata kadi yao?? je ni vitu gani vinawezasababisha usikubaliwe???
 
Last edited by a moderator:
Dragondreamx ushauri wako mzuri sana, hasa kuhusu kufungua payoneer acc mimi nimeshafungua acc kwao, ila mbona inachukua muda mrefu kupata kadi yao?? je ni vitu gani vinawezasababisha usikubaliwe???
What i understand is this PayPal Hawana wakala here in Tanzania so hatuwezi kureceive payment WHY Our banks hawaja jiregister na Paypal So tunaweza kutuma tuu Na if you're money refunded back on your PayPal account Dont withdrawal it.

Ingia kwa website fungua payoneer register with them It will take yu karibia miezi miwili kupata card yao ya Payoneer master card
After hapo unauwezo wa kuhamisha pesa zako From paypal account to payoneer ambapo unaweza kuzitoa katika ATM mashine yeyote inayokubali mastercard

Natumaini umenielewa
kaka mimi nilishapoteza mara nne, jumla karibia 3M, niko mkoani....nachojibiwa ni "tutajuaje kama kweli pesa umerudishiwa?"......"kama hao paypal wamekudanganya?"...fk!
pole sana mkuu #Rene Jr .

hii hapa transaction ya tarehe 10 Nov, 2014 kiasi cha shilingi 31,907.76 kilikatwa na tarehe 18 Dec, 2014 nikapokea Refund kiasi hicho hicho cha 31,907.76/=. Sasa sielewi kwanini refund zingine zinakatwa, zingine hazikatwi na zingine haziingizwi kabisa.

1.jpg

2.jpg
 
pole sana mkuu #Rene Jr .

hii hapa transaction ya tarehe 10 Nov, 2014 kiasi cha shilingi 31,907.76 kilikatwa na tarehe 18 Dec, 2014 nikapokea Refund kiasi hicho hicho cha 31,907.76/=. Sasa sielewi kwanini refund zingine zinakatwa, zingine hazikatwi na zingine haziingizwi kabisa.

View attachment 223565

View attachment 223568

Ni vema ungeweka kiasi cha transaction kwa USD au any other foreign currency ili labda tu estimate labda kipindi una nunua mzigo na kipindi unapata refund Conversion rate hazikuwa sawa
assuming exchange rate hucheza 1694 mpaka 1776
Mfano 1776tzs nimewai kupigwa huko Amazon maana wana include na TAX kwenye conversion rate
Haya ndo maneno walinambia mara ya mwisho hawa CRDB kwamba siku hela inaingizwa kwenye acct itaingizwa kwenye conversion rate ya siku hiyo hiyo na sio siku ulipofanya purchase maana ndo option rahisi

Inshort niliamua ku abandon CRDB mm maana wamekaa na 800,000/= ya refund kwa mwaka mzima ila baade nilipanda kule kwenye department nikawakomalia mpaka wakaiweka maana nilileta attachments,niliandika barua lkn sikupata mssaaada wowote
 
Mkuu tuma tatizo lako ukiambatanisha Na vielelezo vyako vyote customer-hotline@crdbbank.com; pia ukiona hupati ushirikiano ingia kwenye website ya crdbbank Plc, hapo utakuta email za wakurugunce wote wa Crdb escalate issue yako: na kuhakikishia masaa 12 Ni Mengi Swala lako litakuwa limekwisha!
 
Crdb wameshaona hapa ndipo pa kulia

Mie kuna siku nilienda CRDB nikawaambia kuwa nataka nifungue account yangu nyingine kwa ajili ya kufanya transaction online..

Wakanikatalia eti siwezi kuwa na account mbili so natakiwa nitumie account yangu hii hii ndio nituimie kununulia vitu online nikawaambia siamini ununuzi wa vitu online ndio maana nataka nifungue account nyingine separate ili acc ya kununua vitu online iwe na pesa ya kununulia vitu online tu

Wakakataa

Nilichogundua ni kwamba wameona watakosa pesa ya kuiba
Ndio maana wamekataa
 
Nashkuru sana mkuu #Njunwa wamavoko kwa kukubali kuwa crdb kwenyewe kuna tatizo. Hiyo transaction hapo juu ni ya USD 1295 na exchange rate ya siku ile ya transaction ilikuwa 1,675.72/= iliyokata kiasi cha 2,170,053.72/=. Siku tano baadae wakaweka Refund ya shilingi 2,021,349.38/= ambayo ina maana ukifanya computation ya exchange rate unapata 1,560.88/=/$. Ambayo sio kweli, dollar haikushuka hivyo ndani ya wiki moja. Nilifikiri hivyo pia mwanzoni na baada ya kumwonesha afisa mmoja wa crdb Arusha akanishauri niandike barua. Barua niliandika lakini baada ya wiki mbili za ufuatiliaji nikaona kama najisumbua vile. Ntachukua ushauri wako wa kwenda makao makuu kabisa kama wewe ulivyofanya. Ila ni wazi kabisa wafanyakazi CRDB kitengo husika wanatuibia sana hela zetu
 
Mkuu tuma tatizo lako ukiambatanisha Na vielelezo vyako vyote customer-hotline@crdbbank.com; pia ukiona hupati ushirikiano ingia kwenye website ya crdbbank Plc, hapo utakuta email za wakurugunce wote wa Crdb escalate issue yako: na kuhakikishia masaa 12 Ni Mengi Swala lako litakuwa limekwisha!
Asante mkuu, ntafanyia kazi kama ulivyonishauri.
 
Crdb wameshaona hapa ndipo pa kulia

Mie kuna siku nilienda CRDB nikawaambia kuwa nataka nifungue account yangu nyingine kwa ajili ya kufanya transaction online..

Wakanikatalia eti siwezi kuwa na account mbili so natakiwa nitumie account yangu hii hii ndio nituimie kununulia vitu online nikawaambia siamini ununuzi wa vitu online ndio maana nataka nifungue account nyingine separate ili acc ya kununua vitu online iwe na pesa ya kununulia vitu online tu

Wakakataa

Nilichogundua ni kwamba wameona watakosa pesa ya kuiba
Ndio maana wamekataa
Ni kweli kabisa mkuu, ni loophole kubwa sana hiyo na usipokuwa mfuatiliaji hautajua kama unaibiwa. Najaribu kufikiria ni watu wangapi wamefanya online transactions kwa miaka kumi iliyopita na ni kiasi gani kimeshaibiwa kimya kimya mpaka sasa. Hii lazima ifike mwisho, ikiwezekana kufungua kesi mahakamani kabisa
 
Infact mm CRDB Master card imeniumiza sana nimepata refunds nyingi sana lakini huwa haziwekwi automatically na hata nikiwatumia email au kwenda pale AZIKIWE nikawapa Printed email bado huwa hawafanyi hivo...
Wakati mwingine huwa napotezea sababu vinakua vihela kidogo kama 7$-15$

Ila ukweli kwamba tokea nimeanza haya manunuzi wamekula hela nyingi ila sasa unafatilia afu wasipokushughulikia unapotezea maana hizo route za kuja Posta mda nao unabana...

USHAURI: Ukienda Azikiwe Branch kama unataka solution ya fasta omba kuonana na wataalamu wa kitengo cha Onlind purchase hapo ndo utapata solution same day or next day...
 
Mkuu mimi nadhani uende cRDB hq second floor uliza idara inayohusika na mambo ya kadi. Au Tuma email CRDB customer care Mkuu! Hili ni tatizo DOGO sana

Sio kila mtu anaishi Dar useme aende huko HQ kupeleka complains zake. Na si kila mtu ana muda wa kushinda bank mara kwa mara kisa refunds. Ufike muda hiyo bank iweze kumaliza baadhi ya matatizo ya wateja kwenye branch. Kwenda HQ kwa Tatizo la refund ya 30,000 ni aibu kubwa sana kwa benki.

Na baadhi ya wafanyakazi wa hiyo benki hawajui hata paypal ni nin.
 
Kuna wakati naona ni mara mia ku-stick na haya mabenki ya nje kuliko hawa wezi wa CRDB
 
Back
Top Bottom