Tatizo la Panya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Panya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kanyafu Nkanwa, Mar 20, 2011.

 1. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wama Jukwaa naombeni msaada

  Panya wamevamia nyumba yangu mwezi wa tano huu. Nimejaribu sana kupambana nao kwa namna zote imeshindikana kabisa. Mwanzoni nilijaribu kuwauwa kwa sumu. Kwa hakika walikufa sana. Nyumba ikawa kimya kabisa. Waliporudi mara hii, sumu hata ukiweka nyama hawaikaribii. Wanapita mbali kabisa. NImejaribu gundi ya panya. Mwanzoni walinasa kadhaa na kufa. Lakini sasa hivi nikiweka njia zao ama hawapita au wanaruka!

  Ni tatizo kubwa sana. Nawaomba wajuzi wa kupambana na panya wanisaidie.

  Natanguliza shukrani sana
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Umejaribu kufuga Paka?
   
 3. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Panya huwa hawahitaji hasira mzee. Uliwachukia ukaamua kuwapa sumu kali ili wafe. Lakini huwa hawafi wote kinamna hiyo.

  Kwanza ufahamu kuwa ukitaka kuwacontrol wasije kwako, lazima na majirani zako wafanye hivyo hivyo. vinginevyo ukiwaua ndani ya nyumba yako, wale wa jirani wanachukulia nyumba yako kama hilo ni jimbo huru, wanajimuvuzisha na kuanzisha makao.

  Pili ufahamu kuwa panya ana akili kuliko kuku na ana kumbukumbu inayokaa muda wa karibu miezi 6. Na huwa anatilia mashaka kitu chochote kipya kwenye eneo lake. Hivyo ukimwekea mtego mpya leo, anaweza akaushit kwanza mpaka auzoee.

  Ukiwapa sumu kali inayoua haraka, si wote watakula ile sumu. Na watakapokufa, waliobaki watakumbuka muda mrefu kuwa hiyo kitu siyo ya kugusa. Ndio maana mtego au sumu za namna hiyo zinafanikiwa mwanzo halafu baadaye hamna kitu.

  Dawa inayofaa ni ile inayoua taratibu (chronic poisoning). Leo wanakula, hawafi, kesho wanakula tena hivyo hivyo, baada ya siku kadhaa wanaanza kufa. Na hapo hawawezi kukumbuka chakula gani ndio kimewaua kwa vile wanakula na kuchanganya na vingine. Utawazoa mpaka utafurahia.

  Dawa ya namna hiyo inatakiwa iambatane na juhudi zingine kama vile usafi wa jumla, kuziba maeneo wanakofichama, pamoja na ufugaji wa paka. Pia kama unaweza kula (kanyafu nkanwa) nayo inasaidia kuwapunguza (Don't take this seriously, It is just a joke).

  Sumu inayoua taratibu, inapatikana katika kitengo cha utafiti wa mapanya (wizara ya kilimo) pale morogoro, njia ya kwenda Mzinga karibu na lango kuu la kuingilia SUA. Wameichanganya kwenye tambi za rangi ambayo ndege hawaipendi kwa hiyo usiwe na wasi wasi kama wewe ni mfugaji.
   
 4. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Dah! Asante sana ndugu yangu kwa maelezo mazuri namna hii. Tatizo hapa ni namna ya kupata hiyo dawa. Sehemu ingine mikoani, kwa mfano huku Dom, siwezi ipata?
  Pili, suala la usafi najitahidi sana. Kuziba nyumba nimefanya ila hata sijui wanaingilia wapi?! Majirani kuwapangia maisha ni ngumu, kwani wengine hata toilet zao kuingia siwezi kwa jinsi zilivyo chakaa!
  Nadhani nimechagua sehemu siyo kuishi.
   
 5. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kama una jamaa yeyote aliyeko pale morogoro mjini anaweza kukuchukulia na kukutumia kwa njia ya basi. Dawa haizidi sh 1000 kwa kisachet kimoja. Ukinunua hata viwili vinakutosha. Gharama ya kutuma haizidi 5000 kwa mabasi ya HOOD na ABOOD, mabasi mengine sifahamu. Ni kitu rahisi. Hata mimi nimeishaagiza sana kwa njia ya basi nikaletewa.
   
 6. apakati

  apakati Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna pia dawa ya kiteknolojia, ni kifaa kinatoa kelele kubwa sana (yaani kama vile umefunga mashine ya kuranda mbao chumbani kwako) ila binadamu haisikii hii sauti ipo katika frequency (masafa) wanayosikia panya (rodents), so kwao ni bonge la kelele. Ulizia madukani mie sikumbuki maduka, ila vipo bongo for sure.
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dawa pekee ni kufuga Paka na kuweka mazingira safi na kuziba mianya yote inayotumiwa na panya kujificha na kuingia ndani.
   
 8. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa uharaka nakushauri ununue vidonge aina ya Indocid caps (za binadamu)na uchanganye unga wake na chakula kingine kama vile dagaa, unga wa mahindi, samaki nk. Hakikisha kauna maji karibu na vyakula hivyo kwani dawa hii humkausha utumbo panya, process ambayo huleta kiu kali kwake. Akinywa maji tu amepona, na akikosa maji ndo kiama chake.
   
 9. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Kwa nini asijaribu Valiums angalau atakuta wamelala fofofo then unawamalizia tu na makwenzi ya vichwani.....Ugumu waweza kuwa kugundua walipolalia...
   
 10. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Unaweza kutusaidia jina la hiki kifaa mkuu?, maana ukitaka kuuliza uwe angalau na jina.
  Shukrani.
   
Loading...