Tatizo la Majina ya Kiislam Katika Viya ya Maji Maji 1905 - 1907

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
TATIZO LA MAJINA YA KIISLAM KATIKA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji Maji utakutana na jina Mkomanile.

Linaandikwa jina moja tu, ''Mkomanile.''

Kwa nini liandikwe jina moja tu?

Huyu ndiye mwanamke pekee katika majina karibu 67 ya mashujaa wa Vita Vya Maji Maji aliyenyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki Mahenge Songea.

Huyu mwanamke jina lake ni Khadija Mkomanile.
Kwa nini jina la Khadija halikuandikwa?

Tuseme hawakulijua?

Ukisoma historia ya Maji Maji utasoma jina Chinyalanyala jina moja tu.

Kwa nini liandikwe jina moja tu?

Jina lake ni Omar Chinyalanyala.
Inawezekana kuwa jina la Omar hawakuifahamu?

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji maji utasoma jina la Songea Mbano.

Hapa unasoma majina mawili jina moja halikutajwa.

Kwa nini jina lake la kwanza halikuandikwa lifahamike?
Huyu jina lake lake la kwanza ni Abdulraufu.

Hili jina Abdulraufu hawakulijua?
Kuna ''Kazembe'' lakini jina lakini la kwanza halipo.

Haya yanashangaza sana.

Kipande hicho hapo chini kinatoka katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Chifu Songea bin Ruuf wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng'ambo ya Mto Ruvuma katika Msumbiji.

Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga anaandika (barua hii ipo katika herufi za Kiarabu):

Sultan Songea bin Ruuf anasema:

''Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga.
Asalaam Aleikum,

Ninakuletea barua kupitia Kazembe.

Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.

Tupo katika kupigananao hapa.

Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.

Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.

Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).

Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.

Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.

Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.

Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.

Chupa hii, na dawa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita.

Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.

Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,

Sultan Songea bin Ruuf.''

Msikilize Mwalimu Hussein Bashir mwandishi wa vitabu kadhaa vya historia akizungumza:

 
Kuna dhana ya upotoshaji wa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ionekana kuwa ni dini fulani ndiyo walipigania uhuru. Kwani kimsingi mwafrika mtanganyika ni muhanga tu wa dini za kigeni zilizoletwa na wavamizi waliotawala tanganyika. Hao wavamizi walileta utamaduni wao ikiwemo dini, waafrika wakatekwa na tamaduni, mila na dini za wavamizi, waafrika wakaanza kujiita majina ya dini zilizowatawala. Huo uislamu si utamaduni wala dini kwake, uislamu uliletwa na waarabu toka uarabuni. Zama hizi kukuta muafrika anajinasibu na kushadidia dini ambayo awali haikuwepo afrika ni ulimbukeni wa kuendeleza mila na tamaduni za wavamizi
 
Kwa hiyo ilikua vita vya Uislamu dhidi ya Wazungu? Kuna ushahidi kwamba watu wa imani tofauti na Uislamu hawakushiriki hiyo vita? Kama walishiriki why Waislamu tu?
Magn...
Nami nikijiuliza kwa nini Waislam wamekuwa mbele katika vita vile?

Ukitazama minara ya kuwaenzi wazalendo walionyongwa na Wajerumani Songea na Kilwa majina yaliyopo katika kumbukumbu hizo ni ya akina Abdulraufu Songea Mbano na Omar Makunganya.

Nini sababu yake?
 
Kuna dhana ya upotoshaji wa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ionekana kuwa ni dini fulani ndiyo walipigania uhuru. Kwani kimsingi mwafrika mtanganyika ni muhanga tu wa dini za kigeni zilizoletwa na wavamizi waliotawala tanganyika. Hao wavamizi walileta utamaduni wao ikiwemo dini, waafrika wakatekwa na tamaduni, mila na dini za wavamizi, waafrika wakaanza kujiita majina ya dini zilizowatawala. Huo uislamu si utamaduni wala dini kwake, uislamu uliletwa na waarabu toka uarabuni. Zama hizi kukuta muafrika anajinasibu na kushadidia dini ambayo awali haikuwepo afrika ni ulimbukeni wa kuendeleza mila na tamaduni za wavamizi
Loth...
Lakini kwa nini iwe Waislamu ndiyo waliokuwa mbele katika harakati ya kupigania nchi yao?
 
"WOKE" is the name of the game
Ni Kama vile Mzungu Mweupe hataki kuambiwa ukweli wa historia ya utumwa na mateso ya ubaguzi wa watu weusi, anasema ni uchonganishi....
Mzee Mo.....endelea kupiga kwenye mshono.....
 
Vizuri, tupe madini
The Rep...
Chukua mfano huu mmoja.

Watu wanasomeshwa historia siyo ya chama cha TANU.

Historia ambayo chanzo chake ni African Association na waasisi wake mmoja wao katuachia mswada wa kitabu vipi na ni akina nani walioasisi chama hicho na majina yote kayataja.

Historia hii ipo ndani ya kitabu alichohariri mwanahistoria bingwa John Iliffe.
Katika hawa waasisi Waislam ni 6 na 3 ndiyo Wakristo.

Huu ni ukweli na kuna sababu kwa nini ilikuwa vile.

Sababu zinaelezwa kuwa Kanisa lilikuwa inawakataza waumini wake kujiiingiza katika harakati za siasa.

Unachotakiwa kusema na unaelezwa kuwa ati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifika Dar es Salaam kakuta kuna chama cha cha TAA ambacho hakikuwa na mwelekeo na Baba wa Taifa akakipa mwelekeo na kuandika katiba ya TANU.

Ukieleza kuwa hayo si kweli na huyu anaekuambia si kweli ni mtoto na mjukuu wa hao waasisi wa AA na TANU na anaeleza historia anayoijua vyema hasira zinapanda unatukanwa.

Inasikitisha sana.
 
Kwa hiyo ilikua vita vya Uislamu dhidi ya Wazungu? Kuna ushahidi kwamba watu wa imani tofauti na Uislamu hawakushiriki hiyo vita? Kama walishiriki why Waislamu tu?
Kanisa halina miaka 170 tz,hao wakiristo wangetoka wapi 1905!?
 
"WOKE" is the name of the game
Ni Kama vile Mzungu Mweupe hataki kuambiwa ukweli wa historia ya utumwa na mateso ya ubaguzi wa watu weusi, anasema ni uchonganishi....
Mzee Mo.....endelea kupiga kwenye mshono.....
Tek...
Ally Sykes alikuwa na mashine nyumbani kwake Mtaa wa Kipata No. 69 akiburuza makaratasi ya siri kuwahamasisha wananchi kujiunga na TAA kwa wingi.

Haya makaratasi Waingereza wakiyachukulia kuwa ni makaratasi ya uchochezi na wakawa wanamtafuta mtu aliyekuwa anayasambaza.

Mwishowe walimjua na Special Branch wakamwekea mtego.
Ally Sykes aliwaponyoka kwa kudra ya Allah.

Huyu Ally Sykes kadi yake ya TANU ni No. 2 na kadi No. 1 ni ya Julius Nyerere na kaandikiwa na Ally Sykes na huyu Ally Sykes ndiye liyechapa kutoa mfukoni kwake kadi 1000 za kwanza za TANU.

Hutakiwi kueleza historia hii unaitwa mdini.
Mifano iko mingi sana.
 
Hao wajerumani walikuwa wahindu ?

Kama 1905 wajerumani walikuwepo unategemea vipi ukristo usiwepo ?
Walioanza kufika ni walutheri kule tabora,Hawa Wana rekodi Hadi za harakati za milambo,lakini iliwachukua muda gani kupata waamini!?..maana walipata waamini kupitia huduma za jamii,elimu na tiba...mpaka 1905 miaka 107 iliyopita walikua na waamini kiasi gani!?
 
Back
Top Bottom