Namche Bazar
Senior Member
- Apr 8, 2019
- 122
- 179
Heshima kwenu wote.
Sisi wakazi wa kata ya Pongwe jijini Tanga yapata siku 10 sasa hatupati maji kabisa hasa katika maeneo ya Pongwe kusini (Sanawari) maji hayatoki hata tone moja.Hatujapata taarifa yeyote kuhusu tatizo la maji kama hapo nyuma ilivyokuwa na matengenezo nk
Tumeenda kwenye ofisi za mamlaka ya maji (Tanga uwasa) lakini majibu yao hayaridhishi.
Tumepata habari za kuaminika kuwa maji yote yamepelekwa vijiji vya wilaya ya Muheza ili kumtengenezea njia mbunge wa wilaya hiyo Adadi Rajabu aliyewaahidi wapiga kura wake watapata maji kabla ya 2020.
Tuonanyo sisi wananchi wa kata ya Pongwe huu ni ukatili mkubwa kwetu sisi ikiwa sisi ni wateja wa miaka mingi wa mamlaka ya maji ya Tanga,iweje leo sisi tunyimwe maji na kupelekea wateja wapya? Basi kama ni kutanua huduma za utoaji huduma ya maji kwanini kusiwepo na taarifa rasmi inayohusu mgao?
Tunamuamba waziri wa maji na naibu wake watufikirie na sisi katika kupata huduma hii muhimu ya maji hasa katika kipindi hiki cha Korona ambacho tunatakiwa kunawa maji tiririka kila wakati.
Tunaiomba ofisi ya TAKUKURU mkoa/taifa ije ichunguze huu mradi wa maji kwenda Muheza katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu,huenda meneja wa mamlaka ya maji Tanga mjini amepewa kitita cha fedha na kuruhusu maji yote yaende Muheza ili mbunge wa jimbo hilo apate kura?
Tunaomba tusaidiwe hivi sasa tunakunywa maji ya kwenye visima vifupi ambavyo vipo wazi na hatari kwa maisha yetu kwa ujumla wake.
Asanteni.
CC Prof Makame Mbarawa (waziri wa maji)
Juma Aweso (Naibu waziri wa maji)
Ummy Mwalimu (mtia nia ubunge Tanga mjini kupitia CCM.)