Tatizo la mafuriko mjini Dar mvua zikinyesha

Tatizo la mafuriko mjini Dar mvua zikinyesha

View attachment 1096645


Hili tatizo linazorotesha shughuli za uchumi pia ni aibu kwa nchi yetu. Wageni wanaoishi, kufanya kazi au kutembelea Dar Es Salaam wanakwenda na taswira gani ya nchi yetu wakirudi makwao?

Itolewe tender na mzabuni atakae kuja na suluhisho apewe zabuni ya kujenga. Hawa wasomi wetu wa chuo cha ardhi na chuo kikuu hamuelewi pa kupeleka mfumo wa maji taka mvua ikinyesha.?


Mji wa London ulikuwa na tatizo la central sewege system na ilipelekea mji kunuka. 1848 engineer Joseph Blaganzar alipata zabuni ya kujenga system hiyo kwa malipo ya £3,000 then. Mpaka sasa hiyo ndiyo main plan ingawa inaboreshwa lakini tatizo limekwisha.
Mzungu hajakariri kasoma na kuelewa
 
Huwa nasikia aibu mtu akijiita mhandisi
Tatizo hili sio kubwa hivyo kwa sababu mikondo ya maji yote iliyokuwa ina flow naturally imezibwa na hilo ndio tatizo
Haihitaji elimu kubwa kutatua hili
Shame on you guys
 
Bwawani city , eti hili ndo jiji kuu la kibiashara la Nchi . Poor planning and infrastructures , junks and trashes every where & on top of that massive floods

What a joke this is
 
Bwawani city , eti hili ndo jiji la biashara la Nchi . Poor planning and infrastructures , junks and trashes every where & on top of that massive floods

What a joke this
Tunapoteza pesa nyingi hali ikiwa hivi
 
Source kubwa ya maji kujaa kila mahali ni uchafu unaolimbikizwa sehem moja muda mrefu inapotokea mvua kama hivi huzoa uchafu na kuingiza kwenye mitaro then mitaro kuziba ndipo kusababisha maji kujaa na kutapakaa kila mahali kwa kukosa njia ya kupita ukiangalia kila mitaa mto msimbazj unapopita ndipo mahali ambapo watu wa hiyo mitaa wanatupia uchafu na uchafu unaenda hadi pale jangwan na ukichangia wachina walivyokosea kujenga pale jangwani maji yote yanakusanyika pale kwa kushindwa kupita kwenye zile kalavati za jangwani hence kunakua bahari
Tokea plan za miaka ya 70 inafahamika bayana kwamba bonde la Msimbazi kuja jangwani, kupitia Muhimbili mpaka baharini ni njia kuu ya maji, hili halina ubishi lakini kwa kuwa tuna mipango ya zima moto haya ndiyo matokeo yake.
 
Waende Amsterdam wajifunze. Mji umezungukwa na maji lakini kusikia mafuriko eti sababu ya mvua ni nadra Sana.
 
Kwa akili tu ya kawaida bila kuangalia mbali, geografia ya dar ina mito na mabonde machache na bahati yote yanaelekea baharini. Bahati mbaya njia za maji kuelekea kwenye mabonde haya zimezibwa kwa kuta na majengo na hakuna juhudi zozote za kuyafungua maeneo hayo.
Kwa mfano ukiangalia mto msimbazi kuanzia mwanzo wake mpaka ulipopaswa kuingia baharini ( sijui unaingilia wapi) ingekuwa rahisi ukafanyiwa usafi.
 
Back
Top Bottom