Tatizo la mafuriko mjini Dar mvua zikinyesha

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,433
1096645

Hili tatizo linazorotesha shughuli za uchumi pia ni aibu kwa nchi yetu. Wageni wanaoishi, kufanya kazi au kutembelea Dar Es Salaam wanakwenda na taswira gani ya nchi yetu wakirudi makwao?

Dar Es Salaam ni mji wa ki historia, Gavana alipoamua kuhamisha makazi yake kutoka Bagamoyo kuja Dar aliona umuhimu wa jiki hili. Bandari na Airport vinalifanya jiji kuwa lango la biashara. Kweli kwa hali ilivyo kwenye picha unaweza kuiita a Dar financial capital?

Itolewe tender na mzabuni atakae kuja na suluhisho apewe zabuni ya kujenga. Hawa wasomi wetu wa chuo cha ardhi na chuo kikuu hamuelewi pa kupeleka mfumo wa maji taka mvua ikinyesha.?

Mji wa London ulikuwa na tatizo la central sewege system na ilipelekea mji kunuka. 1848 engineer Joseph Blaganzar alipata zabuni ya kujenga system hiyo kwa malipo ya £3,000 then. Mpaka sasa hiyo ndiyo main plan ingawa inaboreshwa lakini tatizo limekwisha.
 
suluhisho ni kujenga mji mpya ndugu yangu huu wa sasa umesha corapt
Hapana mji mpya si suluhisho, kukiwa na sewage system inayochukua maji barabarani hakutakua na mafuriko.
 
Source kubwa ya maji kujaa kila mahali ni uchafu unaolimbikizwa sehem moja muda mrefu inapotokea mvua kama hivi huzoa uchafu na kuingiza kwenye mitaro then mitaro kuziba ndipo kusababisha maji kujaa na kutapakaa kila mahali kwa kukosa njia ya kupita ukiangalia kila mitaa mto msimbazj unapopita ndipo mahali ambapo watu wa hiyo mitaa wanatupia uchafu na uchafu unaenda hadi pale jangwan na ukichangia wachina walivyokosea kujenga pale jangwani maji yote yanakusanyika pale kwa kushindwa kupita kwenye zile kalavati za jangwani hence kunakua bahari
 
Tulipogundua makosa yaliyofanywa na ujenzi wa wa China tulichukua hatua gani?
Nini kifanyike kuzuia watu kutupa uchafu hovyo?
 
Hapana mji mpya si suluhisho, kukiwa na sewage system inayochukua maji barabarani hakutakua na mafuriko.
Yaainaweza kuwa suluhishi lakini kigeografia dar ni kama bondeni hivi, na waliopanga mji walipanga bila kuzingatia haya tunayo rapata sasa hivi, sasa kubomoa na kujenga upya miundombinu bora ni heri kuweka kipao mbele miji mipya
 
Hahaaa hao wasomi wetu waliokariri theories tena kwa lugha ya kigeni,tusbapiga kelele wee mama Ndalichako anahusika nae kwenye hili 😂😂😂😂
 
Yaainaweza kuwa suluhishi lakini kigeografia dar ni kama bondeni hivi, na waliopanga mji walipanga bila kuzingatia haya tunayo rapata sasa hivi, sasa kubomoa na kujenga upya miundombinu bora ni heri kuweka kipao mbele miji mipya
Dar ni historical city, commercial and financial city, kuwepo kwa bandari na Airport kumeifanya kuwa lango la biashara.
Kuujenga upya ni serikali kuwa tayari kupanua huduma za jamii kama umeme na maji na kuhamishia watu kwenye outskirts na kuupanga upya mji.

Si umeona uhamisho wa kwenda Dodoma unavyo sua sua. Kuifanya Dodoma kuwa financial capital si rahisi.
 
Tulipogundua makosa yaliyofanywa na ujenzi wa wa China tulichukua hatua gani?
Nini kifanyike kuzuia watu kutupa uchafu hovyo?
Hapo ni uwajibikaji ni mdogo kwa mfano kuna maafisa afya wengi sana wale wangekua kazi yao ni kuhkikisha kila mtaa unakua na ile sehem ya kuchomea taktaka kama hospital na uchafu usikae hata kidogo mda wote lile tanuru liwe linafanya kazi na hakuna hata karatasi around hilo eneo
 
Dar ni historical city, commercial and financial city, kuwepo kwa bandari na Airport kumeifanya kuwa lango la biashara.
Kuujenga upya ni serikali kuwa tayari kupanua huduma za jamii kama umeme na maji na kuhamishia watu kwenye outskirts na kuupanga upya mji.

Si umeona uhamisho wa kwenda Dodoma unavyo sua sua. Kuifanya Dodoma kuwa financial capital si rahisi.
ni kweli kabisa. cha kwanza tuache kulaumu wataalam husika kwa maana hata sisi ni wataalamu katika fani zetu na hatujatimiza majukumu yetu ipasavyo.

pili kati kati ya mji wa dr kumekuwepo na shuguli nyingi sana za kijamii na kiserikali na huduma muhimu pia, hivyo kupelekea kuwepo kwa idadi kubwa sana ya watu wanaoenda huko kupata huduma.
sasa kinachotakiwa serikali itoe mipango mji mzuri kwa maeneo mengine ili kupunguza shuguli kati kati ya mji, amini mkuu hata hayo mafuriko unayoyaona leo kama watu wakiwa ni wachache hayata kuwepo.
 
Hapo ni uwajibikaji ni mdogo kwa mfano kuna maafisa afya wengi sana wale wangekua kazi yao ni kuhkikisha kila mtaa unakua na ile sehem ya kuchomea taktaka kama hospital na uchafu usikae hata kidogo mda wote lile tanuru liwe linafanya kazi na hakuna hata karatasi around hilo eneo
Rushwa pia inachangia, kungekua na zabuni za kukusanya uchafu na wanye zabuni wanalipwa katika muda.

Pia wanaotupa uchafu hovyo walipishwe fine.
 
kitu kingine kinachochangia ubovu wa miundombinu ya Dar,mfano maeneo ambayo kuna mabonde makali unakuta maji ya mitaronihayaendi mbele wala nyuma yapo yametulia na kuozeana.hivyo mvua ikinyesha kidogo tu maji yanajaa barabarani mfano hii chang'ombe road kutoka veta mpaka huku barabara y mandela,mandera road pia inatatizo hilo hasa maendeo ya mabonde.maji hayana njia za kutokea mpaka yazame ardhini yenyewe
 
Mie naona waweke mipaka,hakuna kujenga katikati ya mji,haiwezekani city centre yetu iwe na hospital na makazi ya watu humo ..lol
 
kitu kingine kinachochangia ubovu wa miundombinu ya Dar,mfano maeneo ambayo kuna mabonde makali unakuta maji ya mitaronihayaendi mbele wala nyuma yapo yametulia na kuozeana.hivyo mvua ikinyesha kidogo tu maji yanajaa barabarani mfano hii chang'ombe road kutoka veta mpaka huku barabara y mandela,mandera road pia inatatizo hilo hasa maendeo ya mabonde.maji hayana njia za kutokea mpaka yazame ardhini yenyewe
Haya ndiyo matatizo ambayo anatakiwa mzabuni wa kuzibua mifumo ya maji na kuhakikisha iko wazi. Mbona baada ya uhuru hatukua na matatizo haya? Tukitumia vichwa vyetu tutaweza kuyatatua.
 
kabisa.sasa serikali ndo inataka ifanye yote kisiasa.Lakin haya mambo ni ya kitaalamu na hayhitaji siasa.
 
Wasomi wetu hata toothpick tuna agiza china, sponge za kuoshea vyombo Italy na china,
kwahiyo hilo unalosema mmm ni kusubili sana
hata pamba ya kuoshea vidonda hospitali zote za Tanzania zinatoka Kenya
 
Back
Top Bottom