Tatizo la LUKU

killo

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
401
94
Za jioni Wapendwa,

Apparently kuna tatizo la luku kwa baadhi ya wateja, unaponunua luku ukiiweka meter inakupa error/haiikubali luku...
Badra Masudi naona unakula weekend umetusahau hata sie wateja wako, basi hata kutupa katangazo.. :nimekataa :nimekataa :nimekataa LOH...

Anyway... Nimepiga simu Tanesco helpline na nikapewa number za LUKU helpline 0689 077 460 / 0768 985 100
Ambapo nilipopiga niliulizwa meter number yangu, nikataja; kisha nikapewa mafungu mawili ya number ambayo nilitakiwa kuyaingiza kwenye luku yangu kama nifanyanvyo nikiweka Umeme,

Fungu la kwanza
2222 3333 1111 4444 5555 - kisha press OK (Hii ni Mfano tuu)
Fungu la pili
0000 5555 6666 7777 8888 - kisha press OK (Hii ni Mfano tuu)
Baada ya hapo meter yako iko tayari endelea na kuweka luku yako uliyonunua kama kawaida

TAHADHARI Kila meter number ina namba zake za kipekee zisioingiliana na meter nyingine... Usijaribu kuweka number tofauti.. Piga simu number za hapo juu upewe number zako binafsi.


Akhsanteni
 
Kwanza hata huo umeme wanaotuuzia nina wasiwasi wanatuwekea tarakimu tu unaisha haraka balaaa
 
Back
Top Bottom