Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Habarini.
jamani mwenzenu nina tatizo hilo la kutoa harufu mbaya kinywani kusema kweli linaninyima raha kabisa hapa majuzi nimemaliza kutumia mouth wash moja inaitwa MEDI-ORAL nilifikiri ingemaliza tatizo lakini naona bado.

Tafadhalini naomba msaada wa nini nifanye/kutumia ili niondokane na tatizo hili, kusema kweli linaninyima uhuru wakati wa mazungumzo.
Uko wapi nikutumie dawa bora ambayo utaleta mrejesho hapa?
Imetengenezwa na madaktari bingwa toka India na Usa baada ya utafiti wa miaka 7
 
Tatizo laweza kuwa sio kinywa tatizo linaweza kuanzia tumboni unakojaza vyakula visivyosagika kirahisi na matokeo yake vinaoza na kushindwa kutoka kwa njia ya haja kubwa hivyo unabaki kutembea na choo tumboni na harufu kutokea kinywani.
Naweza kukubaliana nawe hasa kwenye hiyo point.
Kuna jamaa yangu anaswaki mara mbili kwa siku,tena kwa mswaki ambao haujachakaa,anaswaki muda ulioshauriwa kwa maana anahakikisha kuwa anagusa maeneo yote ya mdomo lakini hilo tatizo halijaisha.
Hakuna sababu zingine za mdomo kutoa harufu?
 
Tumia bicarbonate of soda au baking soda na limau
weka bicarbonate kijiko kimoja kwenye kikombe then kamulia limao
tumia mswaki kusugulia meno kwa mda wa wiki 2...hua inaondoa kabisa harufi
 
When you remove the source will be healthy completely

Kunywa maji mengi one hr before usingizi kunywa maji mengi asbh

It might coming from the gut

Jitahidi kula chakula cha nyuzi nyuzi kitakusaidia

Ila ikishindikana nenda Hosp
Possibily you are suffering from dental diseases

Yeh
 
Tatizo laweza kuwa sio kinywa tatizo linaweza kuanzia tumboni unakojaza vyakula visivyosagika kirahisi na matokeo yake vinaoza na kushindwa kutoka kwa njia ya haja kubwa hivyo unabaki kutembea na choo tumboni na harufu kutokea kinywani.

Kama unakula vyakula vigumu kusagika tumboni kama nyama na vyakula vyenye gesi nk.tafadhali acha sasa fanya hivi asubuhi kunywa maji ya uvuguvugu halafu ufanye mazoezi kidogo hata ya kuruka kamba baada ya muda utapata choo na mchana kula chakula chepesi na usiku baada ya muda hilo tatizo litaisha.

Pia nyama ngumu zinazonasa kwenye meno sometimes zinaoza na kusababisha hiyo shida possibly matatizo chanzo chake kinasababishwa na hayo mambo mawili.
Umesema kweli kabisa
 
Aisee pole sana ndugu.

Swali lingine, hivi utajijuaje kama unatoa harufu mdomoni, manake unaweza jitamba unaongea sana kumbe unatoa harufu mdomoni halafu hujui.

Njia sahihi ya kujua kama unatoa harufu mdomoni wewe mwenyewe ni zipi jamani???
Njia sahihi ni kulamba nyuma ya kiganja/ kiwiko cha mkononi Halafu nusa Ndio kipimo pekee kujua harufu itokayo mdomoni Kwako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom