Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

nimekuelewa mkuu, lakini tatizo hili lilianza kunisumbua toka nikiwa mdogo sijamaliza hata kidato cha nne, na hata nilikuwa sijamjua mwanamke, pia sivuti sigara wala sinywi pombe
 
Nunua mswaki boss. Three times a day kila baada ya chakula.
Pia uwe una floss at least mara moja kwa wiki.
Nunua mouthwash/ breath freshener uwe unatembea nayo mfukoni. La sivyo tumia mints.
 
Habarini za kazi,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 31 kwa sasa, ninatatizo linalonisumbua sana hadi nakosa raha kabisa, nilienda pharmacy nikapewa dawa ya kusukutua na nyingine kama mafuta naweka mdomoni inakaa wa mda kama dakika mbili, nili itumia kwa mda lakini tatizo bado liko pale pale, yaani napata shida sana.

Naomba msaada wenu jamani.
Usianze kupoteza mda humu nenda hospital kamuone mtaalam, kumbuk kwa kadri unavozid kusubir ushari humu ndo tatizo linazidi kuongezeka
 
Sasa hiyo point ya kabla hata sijamjua mwanamke sijaielewa ina uhusiano gani na kunuka kwako mdomo!

By the way, pole sana! Tumia karafuu
 
Sasa hiyo point ya kabla hata sijamjua mwanamke sijaielewa ina uhusiano gani na kunuka kwako mdomo!

By the way, pole sana! Tumia karafuu
kuna mwana jmf alimwamvia (chumvini)ndio maana akaiweka hiyo sentes
 
Harufu ya kinywa kwa watu wasafi inaweza kusababishwa na vifuko kwenye Koo, ambavyo hutunza vipande vya chakula na kuvifanya kutoa harufu Kali. (Tonsils stone)

Nenda kamuone daktari bingwa wa pua, Koo na masikio maarufu kama E.N.T. Kama tatizo ni kubwa, basi wataziondoa tonsils.
 
Pia epuka kula nyuma iwapo unajua hutokua na uwezo wa kusafisha kinywa kwa wakati huo. Vipande vya nyama vinavobaki kati kati ya meno husabisha harufu mbaya
 
Ushauri huu unaweza kukusaidia,kuna kipindi nilikuwa na tatizo hilo yaani unaweza kuwa umekaa ukasikia kama kitu kinakusumbua kooni ukijikoholesha kinatoka kijipunje kinachotoa harufu mbaya sana ila mie sikwenda kwa doctor nilienda pharmacy nikanunua medioro{sina hakika sana kama spelling ziko sawa ni dawa ya kusukutua mdomoni}nikawa nasukutua asubuhi na jioni pamoja na kupiga mswaki kila siku asubuhi na usiku hasa mdomoni kwa juu unahakikisha mswaki unafika kooni kabisa.namshukuru Mungu tatizo liliisha sasaivi nikipiga mswaki usiku nikiamka asubuhi najisikia kinywa kisafi tofauti na kipindi hiko iwe mchana iwe jioni yaani nilikuwa nikipiga mswaki asubuhi nikikaa mpaka saa7 mdomo wote haufai.

Harufu mbaya ya kinywa inakufanya mtu unashindwa kuwa free mbele za watu jaribu kufanya haya uone.nimemaanisha ushauri alioutoa @FromSirwithLove
 
Ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya na mnapambana kulijenga taifa kwa wagonjwa, majeruhi na waliopata majanga au matatizo mbalimbali poleni sana Mungu yuko pamoja nanyi.

Bila kupoteza muda twende kwenye mada ndugu wanajf nimekuwa na tatizo la kunuka kinywa hasa kwa mwaka huu imefikia hatua hadi mpenzi wangu na rafiki zangu wakaribu na wenye mapenzi mema wameniambia kuhusu kutoa harufu mbaya kinywani.

Kwa kweli najisikia vibaya sana kwa tatizo hili kuna jino la chini (gego) limechimbika na kuoza naombeni ushauri wenu nifanyeje kinywa changu kiwe safi na kisinuke angali nasukutua mara mbili au tatu kwa siku? Asanteni sana na natanguliza shukrani wakuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom