Msaada: Tatizo la harufu mbaya kinywani

olambo12zc

New Member
Feb 13, 2023
4
6
Mtu ambae anajua dawa ya kumaliza tatizo la kunuka mdomo nisaidieni!

Napiga mswaki mara tatu kwa siku, nimetumia mouth wash mpaka nimechoka, nimetolewa tonsils lakini wapi!πŸ˜”πŸ˜”

Nisaidie jamani nahisi kwenda maporini nikaishi na miti na wanyama, sababu nimeachana na mpenzi kisa tatizo hili, darasani nilifanya vibaya kisa tatizo hili. Nimetumia gharama kubwa kununua madawa wapi.😭

Mtu aliyewahi kuwa na tatizo hili na akapona aniambie basi na mimi niishi kama binadamu wengine.

Nipo Dar, nahitaji msaada wenu wananzengo!
 
Mkuu hospitali umeenda? Ukapata tiba gani? Au unanunua tu dawa? Umeonana na specialist wa maswala ya kinywa na meno?..

Maelezo yako hayajitoshelezi bado.

Kuna sababu nyingi zinazosababisha io hali, ukiachana na usafi wa kinywa, meno na ulimi kila siku ilikuondoa bacteria, unaweza kuwa na upungufu wa madini zinc, kutofautiana kwa vichocheo mwilini(hormone imbalance) pamoja na magonjwa mengine kama GERD au reflux,intestinal obstruction, matatizo ya ini etc..

Hivyo ni lazma ujue io tatizo lako linasababishwa na nini haswa ili upate matibabu sahihi.. NENDA HOSPITALI.
 
Mtu ambae anajua dawa ya kumaliza tatizo la kunuka mdomo nisaidieni!

Napiga mswaki mara tatu kwa siku, nimetumia mouth wash mpaka nimechoka, nimetolewa tonsils lakini wapi!πŸ˜”πŸ˜”

Nisaidie jamani nahicsi kwenda maporini nikaishi na miti na wanyama, sababu nimeachana na mpenzi kisa tatizo hili, darasani nilifanya vibaya kisa tatizo hili. Nimetumia gharama kubwa kununua madawa wapi.😭

Mtu aliyewahi kuwa na tatizo hili na akapona aniambie basi na mimi niishi kama binadamu wengine.

Nipo Dar, nahitaji msaada wenu wananzengo!
Ohh so sorry jamani
 
Harufu mbaya ya mdomo inayosababishwa na mate ya koo inaweza kuwa ni ishara ya shida ya kiafya, kama vile kuvimba kwa koo au koo la tumbo. Ni muhimu kumuona daktari wako ili kugundua chanzo cha tatizo na kupata matibabu sahihi.

Kwa kuongeza, unaweza kuchukua hatua zifuatazo ili kupunguza harufu mbaya ya mdomo:

1. Kunywa maji mengi - kunywa maji mengi husaidia kuondoa mate ya koo na kusaidia kudumisha unyevu kinywani.

2. Safisha meno yako mara kwa mara - safisha meno yako mara kwa mara na kwa uangalifu. Piga mswaki mara mbili kwa siku na kutumia dawa ya kusafisha mdomo. Hii itasaidia kuondoa bakteria na mabaki ya chakula kinywani, ambayo yanaweza kusababisha harufu mbaya.

3. Tumia mkusanyiko wa chumvi ya maji ya uvuguvugu kufanya kipigo cha koo - mkusanyiko huu wa chumvi unaweza kupunguza uvimbe na kutoa mabaki ya chakula kwenye koo ambayo yanaweza kusababisha harufu mbaya.

4. Kula vyakula vyenye afya - kula vyakula vyenye protini, mboga na matunda kwa wingi na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari na wanga. Hii itasaidia kupunguza uzalishaji wa mate ya koo na kuzuia kuwepo kwa bakteria kinywani.

5. Kuzuia uvutaji wa tumbaku - uvutaji wa sigara na tumbaku unaweza kusababisha harufu mbaya ya mdomo na kuharibu afya ya koo na mapafu.

6. Pumzika vya kutosha - kupumzika vya kutosha husaidia kupunguza mafadhaiko na kuimarisha mfumo wa kinga.

Kumbuka kuwa ni muhimu kushauriana na daktari wako ikiwa una harufu mbaya ya mdomo inayosababishwa na mate ya koo, kwani hii inaweza kuwa dalili ya shida ya kiafya.
 
Halufu mbaya huwa inaanzia kwenye ulimi kama unaelekea kwenye koo, so unaposugua menu sugua hata ulimi Kwa ndani kabisa , halafu leta mrejrsho
 
Mkuu hospitali umeenda? Ukapata tiba gani? Au unanunua tu dawa? Umeonana na specialist wa maswala ya kinywa na meno?..

Maelezo yako hayajitoshelezi bado.

Kuna sababu nyingi zinazosababisha io hali, ukiachana na usafi wa kinywa, meno na ulimi kila siku ilikuondoa bacteria, unaweza kuwa na upungufu wa madini zinc, kutofautiana kwa vichocheo mwilini(hormone imbalance) pamoja na magonjwa mengine kama GERD au reflux,intestinal obstruction, matatizo ya ini etc..

Hivyo ni lazma ujue io tatizo lako linasababishwa na nini haswa ili upate matibabu sahihi.. NENDA HOSPITALI.
Nimeenda kila hospitali ! Mwananyamala , Albert Kairuki, RABININSIA, Almandari posta na pharmacy ndo usisemeee! I’m totally tired of living!πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”
 
Nimeenda kila hospitali !
Una uhakika na hili jibu lako mkuu?umeenda kila hospitali sawa, alafu huwa wanakwambia tatizo ni nini baada ya vipimo? ..
Nilikushauri uonane na specialist au super specialist wa kinywa na meno, ilo pia umeshawai fanya?
 
Acheni ujinga huyu mtu anatakiwa kuonana na specialist wa kinywa, msidhani watu walienda darasani kuuza sura...
 
Nimeenda kila hospitali ! Mwananyamala , Albert Kairuki, RABININSIA, Almandari posta na pharmacy ndo usisemeee! I’m totally tired of living!πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”
Almandari ndio hospital gani jomba? Hebu kuwa serious. Au umemega kipande cha nnya broπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜‚
 
Mtu ambae anajua dawa ya kumaliza tatizo la kunuka mdomo nisaidieni!

Napiga mswaki mara tatu kwa siku, nimetumia mouth wash mpaka nimechoka, nimetolewa tonsils lakini wapi!πŸ˜”πŸ˜”

Nisaidie jamani nahisi kwenda maporini nikaishi na miti na wanyama, sababu nimeachana na mpenzi kisa tatizo hili, darasani nilifanya vibaya kisa tatizo hili. Nimetumia gharama kubwa kununua madawa wapi.😭

Mtu aliyewahi kuwa na tatizo hili na akapona aniambie basi na mimi niishi kama binadamu wengine.

Nipo Dar, nahitaji msaada wenu wananzengo!
Mkuu pole kwa kunuka mdomo wako dawa ninayo mimi ukikosa dawa nitafute mimi ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom