TATIZO LA KUVUJA NYUMBA: KAGUA NYUMBA YAKO MWENYEWE

mdesi

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,349
2,087
Kumekuwa na mijadala mingi juu ya nyumba zilizoezekwa kwa mtindo wa kuficha paa la nyumba, ilionekana nyingi zinavuja sana. Mimi mwenyewe nikiwa mhanga wa jambo hilo.
Nyumba ilikuwa ikivuja sana kwenye gata utadhani hapajaezekwa. Nikawa najiuliza inakuwaje gata linavuja hivyo?
Nikamuita fundi aliyejenga akaja na suluhisho la kuweka tiles kwenye gata lakini ikawa kama hajafanya chochote. Nikaona huu ni ujinga!
Nikapanda juu mimi mwenyewe nikaunga bomba la maji toka changing nikamwaga kwenye gata nikaona maji yanaflow vizuri ila overtime yakawa yanajaa walitumbukiza chupa ya energy wakati wanajenga iliziba angle ya bomba kwa chini. Nikaacha yajae nione km ndo chanzo cha kuvuja wakati mvua inanyesha lakini haikuvuja. Nikazibua yakatoka yote.
Mda kidogo mvua ikaanza kunyesha nikaona gata linavuja, nikapanda juu kukagua nikagundua yale maji yanaingilia kwenye miisho ya mabati kwamba wameezeka bati hadi usawa wa gata na maeneo ambayo bati limepitiliza kidogo haikuwa inavuja. Hivyo solution ni kuongeza urefu wa mabati na si kuweka tiles km fundi alivyo sema.
Nilichojifunza:
1. Hawa mafundi wetu uelewa wao ni mdogo mmno hasa wa kuchukua time na ku Identify tatizo na kutoa proper solution, wanafanya kubuni tu na hivyo kukuingiza hasara.
2. Mafundi hawapigi mahesabu kabla wakati wanajenga. Wanatabia ya ku ignore vitu vya msingi ambavyo baadae vinaleta shida kubwa kwa kujifanya wajuaji.
3. Ukiona kunatatizo usitegemee zaidi mafundi kubaini chanzo cha tatizo, baini mwenyewe muite fundi afanye kwa maelekezo na usimamizi wako mwenyewe.
4. Usiwaamini mafundihawajali kabisa ubora wa kazi zaidi wanajali fedha
 

Attachments

  • 20231216_154202.jpg
    20231216_154202.jpg
    1.1 MB · Views: 16
Safi sana mkuu.
Najua kuna wadau watakuja kuandika ujinga hapa kuwa eti tumejua na wewe unamiliki nyumba.
 
Back
Top Bottom