Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Kama kichwa kinavyojieleza najua Jf kuna watu mbalimbali ninatatizo la kukosa usingizi (insomnia) naomba mwenye kujua dawa sahihi anijuze
 
tafuta turbo moja lenye mgongo ufanye nalo kazi kisawasawa, baada ya hapo utalala mpaka kesho jioni tena. ( Utani mkuu usichulie serious).

Stress, Mawazo kupita kiasi, tabia ya kujichelewesha kulala ubongo umezoea, kutoridhika na maisha yako, mwili kurelax sana mchana. Jaribu kuuchosha mwili mchana kwa kufanya kazi au mazoezi jioni.
 
Mkuu shughuli zako za kila siku zinakufanya uuchangamashe mwili labda kutembea? Kama sivo jaribu kunyoosha viungo lisaa 1 kabla ya kulala uta relax zaid...

wenzangu wanaopandia bus stand ya stesheni kwenda mbande, kisewe kwanzia mida ya 11 jioni nafikiri hawana hili tatizo ukifika, ukaoga, ukala, itakulazimu ulale utake usitake! Unaweza kua unakula huku una doze off
 
Fanya mazoezi mida za jioni kiasi lisaa au zaidi.

Usitumie kinywaji chenye caffeine au chocolate pia Sio nzuri.

Unywaji wa maji uishie walau saa 12 jioni au saa moja usiku (wakati mwengine kwenda haja ndogo mara kwa mara kunakusababishia kutokulala vizuri)

Km una mwenza pendelea kufanya matusi mara kwa mara inasaidia kupata usingizi mwororo.

Fanya maombi/sala kabla kulala.

Wanasema maziwa ya vuguvugu na asali yanasaidia pia.

Ndizi mbivu na lozi pia zinasaidia pendelea kutumia kwenye milo yako ya kila siku.

Pole sana, insomnia mbaya sana. Mie pia ni mhanga. Wakati mwengine inabidi kula dawa za usingizi.
 
Fanya mazoezi mida za jioni kiasi lisaa au zaidi.

Usitumie kinywaji chenye caffeine au chocolate pia Sio nzuri.

Unywaji wa maji uishie walau saa 12 jioni au saa moja usiku (wakati mwengine kwenda haja ndogo mara kwa mara kunakusababishia kutokulala vizuri)

Km una mwenza pendelea kufanya matusi mara kwa mara inasaidia kupata usingizi mwororo.

Fanya maombi/sala kabla kulala.

Wanasema maziwa ya vuguvugu na asali yanasaidia pia.

Ndizi mbivu na lozi pia zinasaidia pendelea kutumia kwenye milo yako ya kila siku.

Pole sana, insomnia mbaya sana. Mie pia ni mhanga. Wakati mwengine inabidi kula dawa za usingizi.
hii kitu inatesa mno,mimi muhanga wa hili pia, nimejaribu vyote hivyo lakini nipata usingizi ni masaa mawili tuu,hata nikimeza dawa za usingizi😭
 
hii kitu inatesa mno,mimi muhanga wa hili pia, nimejaribu vyote hivyo lakini nipata usingizi ni masaa mawili tuu,hata nikimeza dawa za usingizi[emoji24]
Jaribu kuweka music laini wakati wa kulala, it's so refreshing na ukijastuka uko unaota ndoto simba kabeba kombe la dunia.. [emoji23]
 
hii kitu inatesa mno,mimi muhanga wa hili pia, nimejaribu vyote hivyo lakini nipata usingizi ni masaa mawili tuu,hata nikimeza dawa za usingizi[emoji24]
Mie nikizidiwa sana ndio huwa nakula dawa.

Inasumbua mno. Yaani mtu unafanya kazi kutwa, unachoka halafu usiku hulali.

Ila mazoezi yanasaidia sana sana.

Mie ninapofanya mazoezi at least napata kupumzika. Walau hata masaa manne mfululizo.
 
Kama ni mkristo ukikosa usingizi soma Biblia utalala Tu hata kabla hujamaliza.
 
Kuna kitu wanaita Internal Clock, Body Clock au Circadian Clock.
Ni natural way ya mwili juu ya kudetect muda kwa kutumia mwanga na kupanga huu ni muda wa kulala na huu ni wa kuamka lakini vilevile inaweza kuwaadjusted na ratiba yako.
Ni pattern ambayo ubongo wako unaifuata lakini ikivurugwa kinachotokea ni kuamka usiku na kulala mchana au kusinzia.

Utalala au kusinzia mchana sababu ni wazi ubongo wa binadamu ni lazima kulala ili uweze kufunction collectively.
Sasa kama kawaida huwa unalala saa 5 lakini wewe kivyovyote vile ikapelekea ulale saa 7 na kuamka saa 12 ndani ya week tu au zaidi.
Basi internal clock yako itajiadjust wewe kukaa macho mpaka saa 7 bila tone la usingizi na kuamaka saa 12.
Technically ubongo wa binadamu wa mtu mzima unahitaji atleast saa 7 za usingizi chini ya hapo lazima uwe unasinzia na kulala mchana ili kulipia hizo saa 2 sababu jana ulilala kwa saa 5 pekee.
Matokeo yake ukilala mchana ni lazima usiku ukose usingizi sababu well, ulishalala mchana.

Huo mzunguko ukiendelea matokeo yake utakuwa unaweza kukaa macho usiku kucha mpaka saa 12 asubuhi alafu utalala na kuamka saa 12 jioni kama popo.
Na hapo hata ukae kitandani hutopata usingizi hata mtu akupige na kitu kizito kichwani.

Good thing ni kwamba kama hiyo Internal Clock inaweza kuvurugwa na kuwa adjusted na ratiba zako basi unaweza kuirekebisha vilevile na wewe kuanza kulala kawaida kama zamani.

Ni simple tu badirisha ratiba yako ya kulala, badala ya kusinzia au kulala mchana sababu hukulala usiku wa jana basi jitahidi na hakikisha usisinzie wala kulala mchana kivyovyote vile hata kama utasikia na kujihisi ubongo wako unataka kumwagikia masikioni au kichwa kinauma mfulululizo na ni lazima ujisikie hivyo sababu ubongo unakuwa umechoka na kuhitaji kupumzika hivyo kukulazimisha kuzima lakini wewe sema NO, NOT TODAY.

Hiyo njia ya kurekebisha body clock ni mateso yasiyoelezeka utajihisi kuchoka na mwili kuishiwa nguvu pia kichwa kuuma kusiko kawaida na mood yako kuwa kama teja lakini ndio njia pekee inayofanya kazi effectively, hii ni moja ya njia yq mateso wanayotumia secret services wanaita Psychological Torture.

Baada ya hapo ni lazima utalala usiku haijalishi kama una insomnia au ni kuvurugwa kwa Internal clock sababu ni lazima kwa ubongo na mwili wa binadamu kulala na kupumzika, na vilevile ukiwa na insomnia ni lazima uwe unalala na kusinzia hovyo mchana.
Fanya hivyo kwa week au zaidi na matokeo yake baada ya muda utaanza kulala usiku kama kawaida.
 
Dah mm simu ndo inanikosesha usingizi aisee. Si kwamba mm kijana no umri umesonga japo sio mzee I am in 40-43 ila usiku lazima niingie jf umekuwa ulevi wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom