Tatizo kwenye ndoa yangu naomba msaada

Pole sana dada, this is a very serious problem which needs a very technical approach in dealing with, hapo ulipo si mahali salama tena kuwepo, ingawa watoto wenu wanahitaji malezi ya baba na mama, hapa cha msingi ni separation, unawezaje kuwa on the safe side katika kupata hiyo separation: anza kwa wasimamizi wa bdoa yenu washirikishe, nenda kashtaki kwa wazazi kifanyike kikao cha familia zote, mpeleke kwa mchungaji wa kanisa mnalosali kote huko toa ushahidi wa ufedhuli huo, ukiomba guarantee ya matunzo kwa familia, hakikisha matunzo kwa familia yanatolewa ila, omba separation ambayo wewe utakuwa on the safe side katika ngazi zote, kisheria, kidini na kijamii..hapo kinachofuata ni UKIMWI..
 
endelea kumng'ang'ania huyo mwanaume mpaka akuletee magonjwa uache wanao wadogo walelewe na mama wa kambo!!!!!!

Kama unawapenda wanao nivyema ukasonga mbele.....
 
Pole sana Binti mmoja, kwa haya yaliyokukuta ma dia.
Yakwangu ni haya, ndoa yeyote ukiishi hamuwez kusema kuwa mnajuana vizuri pasi kuish miaka kuanzia kumi mkiwa pamoja. Chini ya hapo ni kwamba mnakuwa mnaish kwa kwa kupretend tu. Na ukweli ni kwamba maisha ya kupretend huwa hayadumu kwani mtu utafanya hivyo kwa mwaka but kwa miaka mitano huwez lazima zile tabia ulizo kuwa umezificha zionekane tu. Hili alilolifanya mumeo ndio tabia yake ya wazi wala haifichiki ma dia. Sikukatish tamaa ila that is the reality.

Naliona tatizo hili katika pande mbili tofauti kwanza kuna swala la amani yako binafsi na pili kuna swala la malezi ya wanao. To me hali ikiwa ngumu sana haya yote huwa nasema yatajipa yenyewe. Nikimaanisha kuwa amani yangu nitaipata kwa kujiweka huru kifikra, kimatendo na kiimani. pia amani na malezi ya watoto itapatikana kwa kuwaambia ukweli pasi kuchochea chuki juu ya hali halisi ya maisha yao.

Sikwambii uondoke nyumbani kwako ila mwambie aondoke yeye akuache na wanao. Tena kama mmejenga ndio vizuri kabisa, baki hapo nyumbani kwako ila mwambie kuanzia leo humtaki tena wala asirudi nyumbani aende huko kwenye maisha mengine. Najua ni ngumu lakini usibebe kitu eti unaondoka aende yeye manake ndiye aliye kukataa wala hajafukuzwa. kuhusu tendo la ndoa utajua cha kufanya ila huyu mwanamume asiruke hapo kwako. Mpige marufuku.

pole sana naumia sana juu yako but hapa huna jinsi mfukuze tu.
 
Last edited by a moderator:
mimi nikisema mnaona navuta bange...mshauri basi
Smile haina maana hiyo na i was expecting to see you on this. Najua mdogo wangu these matters are turning you off but nakutia moyo sio wote maidia waweza bahatisha mzuri. au nikupe mwanagu yeye hatoweza kukutenda kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hapo dai separation mpaka atakapojifunza KUFUNGA ZIPU; na akirudi kukuomba masamaha (which is most likely); kituo cha kwanza angaza tena mpime for six months; asiporudi to hell!

Na mimi ningekuwa wewe hata hela ya matumizi simwombi; ili ajue naweza ishi bila yeye. Si umesema una kipato; ishi kadiri ya kipato chako acha kumwomba ela maana atachukulia unajilengesha tena kwake kiaina.

Sikatai tunawapenda saana waume zetu lakini kuna thin line between love and hate.
 
Pole sana. Tatizo kama hili ni vizuri uwashirikishe wale waliosimamia ndoa yenu, wazazi wa pande zote na hata ikibidi wachungaji wenu. Linaweza kukuweka huru kwenye nafsi yako. Usikae nalo tatizo hili wewe mwenyewe, litakukondesha mno. Japo unapaswa pia kutambua kuwa 80% ya wanaume huwa na vimada nje ya ndoa lakini huwa wanawaheshimu sana wake zao wa ndoa. Hivyo unapowafuatafuata sana madhara yake huwa kama haya yako, wanatumia ubabe wao kuhalalisha haramu. Kwa kuwa una kazi yako, nakushauri piga kazi tu, lea wanao, huyo mumeo bado atabaki kuwa mumeo na ninauhakika atarudisha upendo kwako tu. Kwa kuwa sikuhizi kuna magonjwa hakikisha mnapima pindi anaporudi kwako. Endelea na maisha yako mama.
 
Hivi ambao waume zao wanakufa, walipanga watoto wakelewe bila baba?

Dada grow up, yaani nashindwa hata kushauri kwa hasira!

Kama ni wakusikia umepata ushauri as kutosha tu!
 
pole cna dada! me nakushauri kwanza ukapime afya yako ujujue thn washirikishe wazazi wa pande zote mbili thn ujue msimamo wa huyo mwenzio je anajua amekosea ?je yupo teyari kujirekebisha? na kama yupo teyari akupe mkakati na mambo ambayo atachange isije ikawa unapoteza nguvu nyingi kwa m2 ambaye hana mpango.
 
Mimi ni mwanaume na nimeoa, ni mkristu ninaeamini ndoa ya mke mmoja na mme mmoja mpaka kufa lakini kwa hilo nakushauri achana nae. Ila kabla hujamuacha fanya maombi ya kutosha, funga novena usali hata kwa mwaka mmoja huku ukimwacha aendelee na mambo yake, wala usimuulize kuhusu hao malaya wake, we endelea na mambo yako na umfanyie mambo yote kama mme wako isipokuwa tendo la ndoa. Soma biblia na utagundua kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu, na kuwa bado una nafasi ya kumrudisha mme wako wa Mungu.
KUMBUKA KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA!!!!!!! MWISHO USIKUBALI KUFANYA NAE TENDO LA NDOA BILA KUPIMA.
 
Nina ushuhuda wa ndoa ambayo mme alikuwa mkorofi, mlevi, malaya zaidi hata ya huyo mme wako, na mimi niliona hayo kwa macho yangu, nilimuombea huyo mwanaume na ndoa yake kwa muda wa miaka minne mwisho nikachoka, nikamwambia Mungu, hapo nilipofika nimechoka mapenzi yako yatimizwe. Lakini cha ajabu miezi sita baada ya kuacha kumuombea, huyo jamaa aliacha pombe, wanawake na ukorofi, sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na mke wake huyo aliyeteseka kwa zaidi ya miaka saba na huyo baba kwa sasa ni mzee wa kanisa na mshauri wa ndoa zenye matatizo kama aliyokuwanayo yeye. Mimi nitakukumbuka katika sara na nawaalika wa jf tumuombee dada yetu!!!
 
I'm so sorry mamie. hapo ndo huwa natofautiana na wanaume wenzangu walio wengi, kwanini mtu unakua mnyama tena kwa familia yako. mke ulioa mwenyewe na watoto kakuzalia ila bado unafanya mambo ya ajabu mitaani. Ita wazazi muwekeni jamaa chini kama atakubali kuachana na vimada wade it will be well and good ila akizingua jichukulie 50 zako mama, ndoa sio mateso maisha yenyewe mafupi haya kuanza kupigishana kelele na watu.
 
Kwa nini ulisubiri tatizo liwa kubwa ndio ulitatue? hapo juu nime underline dalili zote za mvua inayo kunyeshea sasa hivi. It is very sad you did not take any action when you could. Hata hivo wanasema it is never too late to act.

Kwanza kabisa elewa kua wewe hujakosea (zaidi ya kumuonesha uvumilivu wa kupindukia). Kama ndoa yenu inayumba leo ni kosa lake yeye, sio lako. So stop feeling guilty for something you did not cause. and stop trying to fix somebody else's mess.
Hata kama hujajipanga kulea watoto bila baba nadhani umefika hatua ya kubadili mipango sababu hawana baba tena. Mtu anakaa miezi 2 bila kuja home wakati anaweza, na akija anaondoka bila kuacha pesa. Na pale unapo jaribu kuongea nae anakujibu kuny* hafai kuitwa baba tena, amesha jitoa kwenye ndoa hiyo.

Mwache aendelee na huyo dada mngine, wewe jipange upya tu. Unaweza kuamua ku-divorce kabisa au unaweza kuamua separation tu (Ningeshahuri separation tu hadi pale utakapo kua na uhakika). Umesema unafanya kazi, basi anza kubadili taratibu zako za maisha ili mshahara wako uweze kufunika expences zako. Kama utakwama kabisa unaweza kuongea nae juu ya mahitaji ya watoto.
Usilazimishe, huyo mtu hakupendi, na inaonekana hajawahi kupenda in 5 years of marriage. Ukiendelea kua nae utapata magonjwa ya kila aina, kuanzia BP, moyo, depression hadi magonjwa ya zinaa. Don't let anyone ruin your life, move on!

After all, wahenga walisema: MLA NAWE HAFI NAWE ILA MZALIWA NAWE!! Huyu mlikutana duniani mmeshakuwa wakubwa, mkapendana/akakudanganya kuwa anakupenda etc. Sasa kama uongo wake ameuweka wazi achana nae, mlikutana barabarani/duniani, achana nae. Never let some one frustrate your short life on earth (our life is short-miaka makumi mawili matatu na moja according to the bible). Kuna msemo iusemao: OH LORD GIVE US POWER TO CHANGE WHAT CAN BE CHANGED, COURAGE TO WITHSTAND WHAT WE CAN NOT CHANGE AND WISDOM TO DIFFERENTIATE BETWEEN THE TWO!!!!
 
Dada muache tena kimbia fasta! You live only once na life is not a reharsal its a performance muulize mrisho mpoto ndio kasema hivyo! nimekuja kugundua kuwa sababu ya wanaume kuendelea kucheat ni sisi wanawake kuwasamehe, laiti kama tungekuwa tunawapiga chini fasta wakiharibu, bongo hii cheating ingepungua au wangecheat responsibly. HAWEZI KUACHA STAGE ALIYOFIKIA NI KUMUACHA TU ASIKUDANGANYE MTU.
 
Sikushauri utafute suluhu eti uite vikao, wewe ndio muamuzi wa mwisho na ni maisha yako and at the end of the day you are the only person responsible for your actions,vikao havisaidii chochote trust me, utajidharaulisha wewe na yeye wewe toa taarifa tu kituo cha polisi na ndugu zako wa karibu kuwa its over umeamua kuondoka. na usientertain kumweleza mtu chochote kuhusu your move, be calm, mimi imenitokea haya mambo ya kuita vikao kila siku, mara wazee wa kanisa mara ndugu na marafiki, hakuna kikao kilichonisaidia, matokeo yake tumetengana lakini stori kila mtu anaijua I dont think ni vizuri for both of you.
 
Mimi ni binti wa miaka kama 30 hivi nina watoto wawili niko kwny ndoa ya kikristo kwa miaka mitano kwa sasa, Nimekuwa ninapata matatizo kwenye ndoa yangu mara kwa mara mimi na mume wangu, kiukweli naweza sijakaa kufurahia raha ya ndoa ni machungu tu mara nyingi. nina elimu ya kutosha nina kazi ya uhakika na mume wangu pia as well amenizidi kipato. Toka nimeanza maisha ya ndoa mimi ni kugombana na wasichana wake kwenye simu tu anatoka Asha, anaingia Hadija, akitoka anaingia ashura mpaka sasa hawahesabiki, kipindi chote hiko nimemvumilia nikijua ni utoto unamsumbua. inafika mahali mpaka anakuwa down mpaka kipato kinakuwa tabu kwake anakua amelost anakuwa na mapenzi sana na mimi tunajitahidi pamoja tunainuka.

Sasa hivi karibuni amehama kazi kimkoa nilipo mimi ameenda mkoa mwingine kabla ya kuhama kulikuwa na ugomvi juu ya msichana fulani alikuwa anatembea nae, kiukweli sijawahi kufika kwake cause nilikuwa pregnant kwa wakati huo na hata baada ya kujifungua nikawa nalea mtoto pia job na niliona si vizuri kusumbua watoto kusafiri safiri especially mtoto mchanga na pia sababu alikuwa anakuja kuja mara kwa mara. Ikapita muda kidogo almost miezi miwili hajakuja nyumbani ila pesa akawa anatuma kama kawaida. juzi juzi kaja home akadai simu yake imezima chaji sikushtuka cause namjua tabia yake. asubuhi naenda job nikatumiwa sms na yule msichana anaetembea nae tht nimwambie mume wangu awashe simu anataka pesa ya cliniki dizaini ana mimba yake. nilikuwa namjibu kistaarabu yule dada amenitukana saaaana. ok nikamwambia mwenzangu akaleta visingizio vya hapa na pale, nilikuwa kazini niliporudi home sijamkuta mume wangu akawa amesafiri mkoa anaofanya kazi, siku iliyofuatia nilienda ule mkoa anaofanya kazi cause hajaacha hata pesa ya kutumia home namimi naishi na mama mkwe wangu na watoto wawili home.

Nilipofika huko mkoani kwake nilikuta dalili zote za mtu kuishi na hawala mule ndani, nilikuta mafuta, na vikolokolo vyote vya wanawake. alikiri mbele ya ndugu yangu kuwa huyo mtu anakujaga mara moja moja kiukweli niliumia saana. tukalala asubuhi akaanza kuniambia maneno ya kijeuri tht huyo mwanamke hata nikimkuta pale kwake tutakaa wote na anaweza kuja huku home nilipo yaani popote atapoenda atakuwepo yule hawala cause ana mimba yake. nikamwacha nimerudi huku nilipo nikijua tatizo limeshakua kubwa na nahitaji kulitatua. NIKO NJIA PANDA SIJUI NITATUEJE NISAIDIENI WADAU. Maana nahisi watoto wangu mwisho wao siuoni na sijapanga watoto wangu waishi bila baba. sina la kufanya.
Vua gamba vaa gwanda!
 
:biggrin1: nimeipenda sentensi yako..wewe ni BINTI wa miaka 30 na watoto wawili na umeolewa..jamani wewe sio MAMA/MWANAMKE kweli au??
 
Mmhhh....naomba nipite kimya kimya leo, zaidi labda nikupe tu pole sana Binti mmoja na kila kheri kwenye maamuzi yako.
 
Last edited by a moderator:
Binti mmoja:Ukiwa kama mama wa familia ni lazima uwe mtu wa kuomba..na kama unadumu kwenye maombi haya yatapita ,kumbuka huna mamlaka na huo mwili kwakuwa uliunganishwa siku ya ndoa.
Wengi wanakushauri umnyime unyumba nk kumbuka shetani aliyemuingiz mumeo anataka kukuangusha ili msambaratike..mimi im your age mate..nimepitia hali kama yako niling'ang'ana na Mungu hadi kikaeleweka..
1.
"Chagueni wenyewe hivi leo mtakayemtumikia." Yoshua 24:15.Mungu anatoa changamoto kwa viumbe wake aliowaumba kwa mfano wake ili wachague kutenda mema kwa sababu uwezo wao wa kufikiri unawaambia kwamba "Njia ya Mungu ni bora kuliko zote." Kisha kugeukia mbali na makosa kwa sababu uwezo wao wa kufikiri unawaonya dhidi ya matokeo ya uasi na dhambi.

Ni viumbe wale tu walio na uwezo wa kufikiri na kuchagua wawezao kuwa na upendo wa kweli. Mungu alitamani sana kuwaumba watu ambao wangeweza kuijua na kuithamini tabia yake, kuitikia kwa kuonyesha upendo wao kwake, na kujazwa na upendo wake, kwa ajili ya wengine. Mungu alitaka sana kuwashirikisha upendo wake hata akawa tayari kujiingiza katika hatari kubwa mno ya kuwaumba malaika na wanadamu wenye uwezo wa kuchagua..
Binti mkabidhi yeye ndoa yako atakulipia yote atakunasua kwenye mtego waliokutegea kwa siri...mumeo anakuhitaji ili umuombee si akili zake ..kumbuka wanadam tuna njia nyingi za kufanya kurubuniana huwezi jua mumeo yuko kwenye mtego upu ila wa kumuokoa ni wewe...achana na mambo ya kuhangaika kwa akili na nguvu zako..Natamani Roho mtakatifu akufunue uelewa wako wa mambo ya rohoni ili umshike sawasawa ktk mapito yako.

3.Tena fanya toba kwaajili ya hizo roho chafu zisisambae katika watoto wako nani anayejua hebu muulize mama mkwe wako baba mkwe enzi zake alikuwaje?tubu kwa machozi ndg yangu okoa familia yako...ukimwi upo sitaki ufe nao lakini ukiwa mwaminifu kwa Mungu kamwe hatokuacha uaibike,jitakase kwa damu ya Yesu usiku na mchana takasa mwili wa mumeo na watoto wako.nina mengi ya kusema ila hapa naona sio ,PM kama unataka ushauri zaid
 
Back
Top Bottom