Tatizo kwenye ndoa yangu naomba msaada

Kwa nini ulisubiri tatizo liwa kubwa ndio ulitatue? hapo juu nime underline dalili zote za mvua inayo kunyeshea sasa hivi. It is very sad you did not take any action when you could. Hata hivo wanasema it is never too late to act.

Kwanza kabisa elewa kua wewe hujakoses (zaidi ya kumuonesha uvumilivu wa kupindukia). Kama ndoa yenu inayumba leo ni kosa lake yeye, sio lako. So stop feeling guilty for something you did not cause. and stop trying to fix somebody else's mess.
Hata kama hujajipanga kulea watoto bila baba nadhani umefika hatua ya kubadili mipango sababu hawana baba tena. Mtu anakaa miezi 2 bila kuja home wakati anaweza, na akija anaondoka bila kuacha pesa. Na pale unapo jaribu kuongea nae anakujibu kuny* hafai kuitwa baba tena, amesha jitoa kwenye ndoa hiyo.

Mwache aendelee na huyo dada mngine, wewe jipange upya tu. Unaweza kuamua ku-divorce kabisa au unaweza kuamua separation tu (Ningeshahuri separation tu hadi pale utakapo kua na uhakika). Umesema unafanya kazi, basi anza kubadili taratibu zako za maisha ili mshahara wako uweze kufunika expences zako. Kama utakwama kabisa unaweza kuongea nae juu ya mahitaji ya watoto.
Usilazimishe, huyo mtu hakupendi, na inaonekana hajawahi kupenda in 5 years of marriage. Ukiendela kua nae utapata magonjwa ya kila aina, kuanzia BP, moyo, depression hadi magonjwa ya zinaa. Don't let anyone ruin your life, move on!

Anasema ananipenda amechanganyikiwa na yeye for the situation sijui wakati anafanya haoni, nimepeleka mashtaka kwny baraza la kata akikataa kuja au wakishindwa naenda ustawi wa jamii. What I need to do ni kufuta dream za huyo mke mtarajiwa kwanza kupata assuarance ya pesa ya matumizi kwa watoto monthly bila usumbufu. abakishiwe pesa ya kutumia yeye. sijui nifanye nini kingine?
 
pole sana dada ila kweli kuna maudhi katika ndoa na hili hutokea pale mmoja napokuwa hayuko muwazi na pengine anafanya mambo ya ajabu haogopi kama kuna HIV na kama akikuambukiza je, watoto nani atawalea kwa ushauri wangu, kuachana ni suruhisho lakini kwa upande mwingine si suruhisho naomba wewe kaa na watoto wako muache wala usimufatilie fanya mambo yako ila siku moja atakuja na atakupigia magoti amini nenda kanisani/msikitini kulinagana na imani yako Mungu atatenda na mmeo atarudi.
 
Unajua mimi hili nilishalisema na nalirudia tena,wanawake kuondoka kwenye ndoa zao sio kama wanashindwa,kigumu kwao ni kuona una waacha watoto watateseka na baba asiye na muelekeo,pili hata akiondoka na hao watoto anafikiria ni jinsi gani watakavyokuwa wakimganda na mwaswali yao ya "mama mbona tumeondoka nyumbani,mama hivi baba yuko wapi,mama kwanini usimsamehe baba" n.k,am sure if you have kids utakuwa unajua haya maswali ya watoto ambayo yanaumiza sana.Kwa hiyo hapo akili ni kichwani mwako kwani am sure unampenda mumeo sana tu ila SHETANI ndio analeta haya mateso yote nyumbani kwako,muombe Mungu hakuna kisichowezekana kwake kila kitu kitakuwa kama unavyotaka.
 
Anasema ananipenda amechanganyikiwa na yeye for the situation sijui wakati anafanya haoni, nimepeleka mashtaka kwny baraza la kata akikataa kuja au wakishindwa naenda ustawi wa jamii. What I need to do ni kufuta dream za huyo mke mtarajiwa kwanza kupata assuarance ya pesa ya matumizi kwa watoto monthly bila usumbufu. abakishiwe pesa ya kutumia yeye. sijui nifanye nini kingine?
pole mwaya,
hapo unachotakiwa kufanya sababu yeye ni baba wa hao watoto wako ni kuhakikisha anahudumia hao watoto, lakini siyo kwa expense yako. na la maana sana ni kumwacha afanye kitu roho inapenda, ukimng'ang'ania wakati yeye roho yake ipo kwa huyo dada utakuwa unajidanganya tu upo na mtu wakati ki uhakika hayupo nawe.
lakini nakushauri tu, jitahidi kufanya kazi kwa bidii ili uweze kuhudumia watoto wako hata kama baba yao hatoi chochote
 
dada pole ngoja nifikiri ni ushauri gani unakufaa .

Ndio maana Smile kila siku anaendelea kukata tamaa :confused2:
 
Last edited by a moderator:
Pole Bintimmoja ,Usipigane kwa nguvu zako walausijichoshe mtwike yeye (BWANA) fadhaa zako,mwache aende anakoenda na afanyeanachofanya ila uwe mwaminifu mbele za Mungu yeye atakupigania kwa maanaimeandkiwa

Isaya 30;15 Kwa maanaBwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehemtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini;
God also convicts of sin and can make a husband feel empty and miserable as hecontinues in his unfaithfulness. Should a husband choose not to turn from hiswayward ways, God promises to care for wife as you trusts in Him.Atakufunguliamilango mipya mbele yako, atakupa hekima ya kuamua , supply strength for everyday and will be your companion in times of loneliness. Prayer brings God intoevery situation and when He comes He brings hope.

 
JAMANI NIMEPITIA THE SAME ROAD SAME SAME KABISA NA MIMI PIA NILISAFIRI NIKAKUTA HIVYO HIVYO, NA BAADAE AKAZAA NJE .bahati nilikuwa sijafunga naye ndoa ila nlikuwa na 2kids.

ushauri:
sikushauri kwasababu nilifanya hivi ila kwa uzito watatizo:
1.NINAAMINI KWAMBA KILA MTU ANA HAKI YAKUFURAHIA MAISHA MPAKA SIKU ANAPOITWA MBINGUNI'
2. NINATHAMANI KUBWA SANA NA NINAITAMBUA THAMANI YANGU BILAMTU YOYOTE KUNIAMBIA MIMI NI WATHAMANI NAMNA GANI
3.NINAAMINI MUNGU ALIPANGA NIISHI MAISHA FULANI AMBAYO KWAAKILI YANGU NILIWAHISHA MWENYEWE BILA KUMSHIRIKISHA MUNGU ,"KAMA MTOA MADA '
4.IBELIVE THAT -THE WILL OF GOD WILL NEVER
REMEMBER REMEMBER REMEMBER
[h=3]The will of God will never take you -[/h][h=3]Where the grace of God cannot keep you,[/h][h=3]Where the arms of God cannot support you,[/h][h=3]Where the riches of God cannot supply your needs,[/h][h=3]Where the power of God cannot endow you.[/h][h=3][/h][h=3]The will of God will never take you -[/h][h=3]Where the Spirit of God cannot work through you,[/h][h=3]Where the wisdom of God cannot teach you,[/h][h=3]Where the army of God cannot protect you,[/h][h=3]Where the hands of God cannot mold you.[/h][h=3][/h][h=3]The will of God will never take you -[/h][h=3]Where the love of God cannot enfold you,[/h][h=3]Where the mercies of God cannot sustain you,[/h][h=3]Where the peace of God cannot calm your fears,[/h][h=3]Where the authority of God cannot overrule for you.[/h][h=3][/h][h=3]The will of God will never take you -[/h][h=3]Where the comfort of God cannot dry your tears,[/h][h=3]Where the Word of God cannot feed you,[/h][h=3]Where the miracles of God cannot be done for you,[/h][h=3]Where the omnipresence of God cannot find you.[/h]ACHANA NA HUYU MTU ,MIMI NILIMPELEKA KWA WAZAZI,KWASABABU HATUKUWA NA NDOA HALALI ILIVUNJWA NA JAMII ILIYOKUWA INATUTAMBUA ,THEN BASI ,NA NILISIMMMA KAMA MAMA NA WATOTO WANGU MPAKA MUNGU AKANIPA RIGHT MAN TO LIVE WITH NATUMEFUNGA NDOA TUNAISHI KWA RAHA KABIS A,NAAMINI THE WILL OF GOD........
LAST SIKUSHAURI KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MAPYA UKIACHANA NA HUYU BWANA,FOCUS KUWARISE WATOTO KIDS ARE WORTH IN THIS WORLD AM TELLING YOU THE TRUTH .RISE THEM UNTIL THE WILL OF GOD TO FUL FILL YOU NEEDS









[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
Remember, Remember, Remember, Remember..The will of God will never take you
Where the grace of God cannot keep you,
Where the arms of God cannot support you,
Where the riches of God cannot supply your needs,
Where the power of God cannot endow you.
The will of God will never take you
Where the spirit of God cannot work through you,
Where the wisdom of God cannot teach you,
Where the army of God cannot protect you,
Where the hands of God cannot mold you.
The will of God will never take you
Where the love of God cannot enfold you,
Where the mercy of God cannot sustain you,
Where the peace of God cannot calm your fears,never take you
[/FONT]
Where the grace of God cannot keep you,
Where the arms of God cannot support you,
Where the riches of God cannot supply your needs,
Where the power of God cannot endow you.
The will of God will never take you
Where the spirit of God cannot work through you,
Where the wisdom of God cannot teach you,
Where the army of God cannot protect you,
Where the hands of God cannot mold you.
The will of God will never take you
Where the love of God cannot enfold you,
Where the mercy of God cannot sustain you,
Where the peace of God cannot calm your fears,
Where the authority of God cannot overrule for you.
The will of God will nWhere the omnipresence of God cannot find you.
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
[/FONT]
 
Anasema ananipenda amechanganyikiwa na yeye for the situation sijui wakati anafanya haoni, nimepeleka mashtaka kwny baraza la kata akikataa kuja au wakishindwa naenda ustawi wa jamii. What I need to do ni kufuta dream za huyo mke mtarajiwa kwanza kupata assuarance ya pesa ya matumizi kwa watoto monthly bila usumbufu. abakishiwe pesa ya kutumia yeye. sijui nifanye nini kingine?

Hongera kwa kuchukua hatua. Mimi ningekua nafasi yako ningefanya mambo mawili kwanza haraka haraka


  1. Kuhakikisha na-secure kila kitu tulichuma tukiwa pamoja ili iwe guarantee ya maisha ya watoto. kama kuna account, au nyumba etc, hakikisha hawezi kuvitumia na mtu mngine zaidi ya watoto (na wewe usitumie kwa mahitaji binafsi). Hapa tumia ujanja wote unao. kwa kupitia maongezi nae, familia, sheria etc.
  2. Kufuta ilepicha ya mume. So long as unamuona mume bado utahitaji kuongea nae kabla ya kufanya maamuzi sababu mume wako ni lifetime partner. But ikiwa utamuona kama ex husband, au baba watoto but not mume basi utam-consult only for those 'joint interest' (ie watoto).
Baada ya hapo ndio uje uconsider sasa kujenga maisha upya ya u-single mother, kutafuta kazi yenye pato la kufunika pengo la pato lake katika expenses zenu, kubadili ndoto zako na matarajio, kubadili relation yako na familia yake, kuwaambia watu wengine etc. Ni journey kubwa sana, you need to keep your head clear and your hear cool (but not frozen)
 
My dear YOU ARE PLAYING WITH POISON, DEATH WILL OVERTAKE YOU. Unasubiri nini!!!!!
Mtu mjinga siku zote hujifunza kutokana na makosa yake, lakini mwerevu hujifunza kutokana na makosa ya wenzake. ukisubiri ujifunze kutokana na makosa yako ujue unasubiria ukimwi. Fuata ushauri waliokupatia wachangiaji wengi
 
kwa nini ulisubiri tatizo liwa kubwa ndio ulitatue? Hapo juu nime underline dalili zote za mvua inayo kunyeshea sasa hivi. It is very sad you did not take any action when you could. Hata hivo wanasema it is never too late to act.

Kwanza kabisa elewa kua wewe hujakoses (zaidi ya kumuonesha uvumilivu wa kupindukia). Kama ndoa yenu inayumba leo ni kosa lake yeye, sio lako. So stop feeling guilty for something you did not cause. And stop trying to fix somebody else's mess.
Hata kama hujajipanga kulea watoto bila baba nadhani umefika hatua ya kubadili mipango sababu hawana baba tena. Mtu anakaa miezi 2 bila kuja home wakati anaweza, na akija anaondoka bila kuacha pesa. Na pale unapo jaribu kuongea nae anakujibu kuny* hafai kuitwa baba tena, amesha jitoa kwenye ndoa hiyo.

Mwache aendelee na huyo dada mngine, wewe jipange upya tu. Unaweza kuamua ku-divorce kabisa au unaweza kuamua separation tu (ningeshahuri separation tu hadi pale utakapo kua na uhakika). Umesema unafanya kazi, basi anza kubadili taratibu zako za maisha ili mshahara wako uweze kufunika expences zako. Kama utakwama kabisa unaweza kuongea nae juu ya mahitaji ya watoto.
Usilazimishe, huyo mtu hakupendi, na inaonekana hajawahi kupenda in 5 years of marriage. Ukiendela kua nae utapata magonjwa ya kila aina, kuanzia bp, moyo, depression hadi magonjwa ya zinaa. Don't let anyone ruin your life, move on!
supper advice good
 
....... Nilipofika huko mkoani kwake nilikuta dalili zote za mtu kuishi na hawala mule ndani, nilikuta mafuta, na vikolokolo vyote vya wanawake. alikiri mbele ya ndugu yangu kuwa huyo mtu anakujaga mara moja moja kiukweli niliumia saana. tukalala asubuhi akaanza kuniambia maneno ya kijeuri tht huyo mwanamke hata nikimkuta pale kwake tutakaa wote na anaweza kuja huku home nilipo yaani popote atapoenda atakuwepo yule hawala cause ana mimba yake. nikamwacha nimerudi huku nilipo nikijua tatizo limeshakua kubwa na nahitaji kulitatua. NIKO NJIA PANDA SIJUI NITATUEJE NISAIDIENI WADAU. Maana nahisi watoto wangu mwisho wao siuoni na sijapanga watoto wangu waishi bila baba. sina la kufanya.

Binti pole kwa yaliyokusibu. matizo kama hayo yapo mwa familia nyingi tu. mie nimeangalia maeneo hayo niliyoyabold tu
1. amekiri mbele yako na ndugu yako kuwa ni kweli ana mwanamke mwingine, ujue huyo yuko serious na hyo mwanamke, wanaume ambaye amefanya hayo bila dhamira ya kweli hata umkute kitandani atajitetea tu kuwa hana uhusiano.
2. Mimba ni kiashiria kingine cha kuwa na serious relationship kwa kuwa mimba inaleta muendelezo wa mahusiano (i.e. baada ya mtot kuzaliwa lazima kutakuwa na muunganiko tena mkubwa.
3. Suala la watoto wako kutokukua bila kuwa na baba... watoto wako bado wanae baba na wewe pia unae mume tatizo ni kachepuka tu pembeni lakini naamini atarudi tu.
La muhimu hapo, acha kumfuatilia kwa sasa maana unaweza kufanya kitu cha kijinga kwa kuwa bado una hasira, endelea na kazi yako kwa bidii zaidi na kulea watoto wako, endelea kumsisitiza mume alete matumizi kwani mkataba aliouanzisha na huyo mwanamke mwingine wewe haukuhusu kwa lolote, hasira zako zikipoa muite ukiwa na watu wengine wachache ili mjadili way forward/mustakabali wa ndoa yenu ili kama inakufa ujue mapema uendelee na maisha yako, kwani LIFE MUST GO ON WITH OR WITHOUT HIM!
 
pole mpendwa.
Mi naona utengane naye.
Heri watoto walelewe na mama tu kuliko ungannganie hapo halafu watoto wabaki yatima maana hapo risk ya wewe kuletewa magonjwa nikubwa.
Mungu akupe hekima za kuamua yaliyo mema kwako na kwa wanao..pia akupe faraja.
 
No fixed Point.Kuvunja ndoa it is not a solution:Nafikiri amevumilia sana pull up your soks .Huyo ni mume wake anatakiwa kumpigania sana kama alivyoapa.Upande mwingine labda dada umekuwa busy sana na kazi unakosa muda wa kumpa malovii muzee thus why anatafuta faraja kwingine .Nenda kwa wazazi ,mshenga na viongozi wa dini ikishindikana nenda Ustawi wa jamii nafikiri jibu litapatikana tu kwani kama hujaridhia mke mdogo huyo jambazi atatimuliwa tu na sheria!!!
 
achana naye bwana.....
unaogopa watoto wako kulelewa na wewe mwenyewe bila baba ila huoni hatari ya wewe kuambukizwa ukimwi na hivyo watoto wenu kuwakosa nyie wazazi wote?????:confused2::confused2::confused2:
 
Unajua mimi hili nilishalisema na nalirudia tena,wanawake kuondoka kwenye ndoa zao sio kama wanashindwa,kigumu kwao ni kuona una waacha watoto watateseka na baba asiye na muelekeo,pili hata akiondoka na hao watoto anafikiria ni jinsi gani watakavyokuwa wakimganda na mwaswali yao ya "mama mbona tumeondoka nyumbani,mama hivi baba yuko wapi,mama kwanini usimsamehe baba" n.k,am sure if you have kids utakuwa unajua haya maswali ya watoto ambayo yanaumiza sana.Kwa hiyo hapo akili ni kichwani mwako kwani am sure unampenda mumeo sana tu ila SHETANI ndio analeta haya mateso yote nyumbani kwako,muombe Mungu hakuna kisichowezekana kwake kila kitu kitakuwa kama unavyotaka.

thanks
 
pole sana dada ila kweli kuna maudhi katika ndoa na hili hutokea pale mmoja napokuwa hayuko muwazi na pengine anafanya mambo ya ajabu haogopi kama kuna HIV na kama akikuambukiza je, watoto nani atawalea kwa ushauri wangu, kuachana ni suruhisho lakini kwa upande mwingine si suruhisho naomba wewe kaa na watoto wako muache wala usimufatilie fanya mambo yako ila siku moja atakuja na atakupigia magoti amini nenda kanisani/msikitini kulinagana na imani yako Mungu atatenda na mmeo atarudi.

thanks
 
umeolewa ndoa ya kikristo lakini mumeo akitoka nje anatoka na kina ASHA,HADIJA NA ASHURA????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
???????????????????????????????????????????????????nimepata viulizo vingi hapo!au ni mifano tu?

well,hatua uliyofikia ya matatizo ni ya juu mno kiasi kwamba una option 2 tu,ambazo ni kuamua kuishi na matatizo yako mpaka ufe kwa maana ya kwamba hilo dudu haliwezi kurekebishika tena au umuache sasa hivi baada ya kumaliza kusoma post hii!kwaheri!
 
Dah mimi mwanaume lakini nimetetemeka, I can't imagine harusi tunazozichangia daily zinapelekea watu kuishi hivi, sikatai tunazingua wasichana sana but mke wa ndoa kufanyiwa hivi its a shame to manhood, I can't imagine my lovely sister aliyeolewa juzi ndo anakutana na hizi experience nahisi nitapiga shemej risasi,,, sometimes wadada msifosi ndoa,may be alikuoa kwa shinikizo,

Mzee mmoja job anapendaga kusema wanaume tunateleza sometime tuna cheat but fanya vyovyote mama watoto wako wala wanaomfaham asijue kwa vyovyote hata kwa kuhisi hairuhusiwi ni mwiko, sasa hadi kuzaa nje dah I can't imagine, ngoja niteme mate chini mie nikemee isije ikanikuta na mimi kufanya the same, dah lakini hata kama tugombane vipi kama ni ndoa siwezi, kwanza b mkubwa nitamuangaliaje mkwewe kufanyiwa hivyo nahisi atanichinja
 
Mimi ni binti wa miaka kama 30 hivi nina watoto wawili niko kwny ndoa ya kikristo kwa miaka mitano kwa sasa, Nimekuwa ninapata matatizo kwenye ndoa yangu mara kwa mara mimi na mume wangu, kiukweli naweza sijakaa kufurahia raha ya ndoa ni machungu tu mara nyingi. nina elimu ya kutosha nina kazi ya uhakika na mume wangu pia as well amenizidi kipato. Toka nimeanza maisha ya ndoa mimi ni kugombana na wasichana wake kwenye simu tu anatoka Asha, anaingia Hadija, akitoka anaingia ashura mpaka sasa hawahesabiki, kipindi chote hiko nimemvumilia nikijua ni utoto unamsumbua. inafika mahali mpaka anakuwa down mpaka kipato kinakuwa tabu kwake anakua amelost anakuwa na mapenzi sana na mimi tunajitahidi pamoja tunainuka.

Sasa hivi karibuni amehama kazi kimkoa nilipo mimi ameenda mkoa mwingine kabla ya kuhama kulikuwa na ugomvi juu ya msichana fulani alikuwa anatembea nae, kiukweli sijawahi kufika kwake cause nilikuwa pregnant kwa wakati huo na hata baada ya kujifungua nikawa nalea mtoto pia job na niliona si vizuri kusumbua watoto kusafiri safiri especially mtoto mchanga na pia sababu alikuwa anakuja kuja mara kwa mara. Ikapita muda kidogo almost miezi miwili hajakuja nyumbani ila pesa akawa anatuma kama kawaida. juzi juzi kaja home akadai simu yake imezima chaji sikushtuka cause namjua tabia yake. asubuhi naenda job nikatumiwa sms na yule msichana anaetembea nae tht nimwambie mume wangu awashe simu anataka pesa ya cliniki dizaini ana mimba yake. nilikuwa namjibu kistaarabu yule dada amenitukana saaaana. ok nikamwambia mwenzangu akaleta visingizio vya hapa na pale, nilikuwa kazini niliporudi home sijamkuta mume wangu akawa amesafiri mkoa anaofanya kazi, siku iliyofuatia nilienda ule mkoa anaofanya kazi cause hajaacha hata pesa ya kutumia home namimi naishi na mama mkwe wangu na watoto wawili home.

Nilipofika huko mkoani kwake nilikuta dalili zote za mtu kuishi na hawala mule ndani, nilikuta mafuta, na vikolokolo vyote vya wanawake. alikiri mbele ya ndugu yangu kuwa huyo mtu anakujaga mara moja moja kiukweli niliumia saana. tukalala asubuhi akaanza kuniambia maneno ya kijeuri tht huyo mwanamke hata nikimkuta pale kwake tutakaa wote na anaweza kuja huku home nilipo yaani popote atapoenda atakuwepo yule hawala cause ana mimba yake. nikamwacha nimerudi huku nilipo nikijua tatizo limeshakua kubwa na nahitaji kulitatua. NIKO NJIA PANDA SIJUI NITATUEJE NISAIDIENI WADAU. Maana nahisi watoto wangu mwisho wao siuoni na sijapanga watoto wangu waishi bila baba. sina la kufanya.

Pole sana dadaangu na Hongera sana kwa uvumilivu. Kati ya haya yafuatayo yanaweza kuwa dawa au suluhisho kwa tatizo lako;
1. Kuivunja hiyo ndowa na ukaamuwa kuishi peke yako. Hili ni suluhisho kubwa kwani litaweza kukuepusha na maumivu ya moyo na kujilinda na maradhi ambayo lazima itayapata kwa kuendelea kuishi na huyo mumeo. Ni mtu asietosheka na wala haendi nje kwa bahati mbaya bali kwa makusudi, hajikingi na ndio maana anatia mimba, na usifikiri kuwa hata huyo alinaye hamfanyiikama anavyokufanyia wewe.
2.Kuasiana nae kabisa bila ya kudai talaka ili hao watoto wako waendelee kuwa na baba ndani ya ndowa ya kuasiana. Hapo baba yao atakapopata maradhi atarejea na watoto watamtunza mpaka kifo chake.
3. Kuuchuna tu na kuendelea kuishi nae kama tabia zenu mlivyoziamuwa ndani ya ndowa yenu. Tabia yako ya kumvumilia na kumsamehe kila anapokutenda ni matokeo ya haya ya sasa hivi. Kwa vile ulivumilia na maisha yakaendelea eti unampenda na hutaki watoto wako wasiwe na baba. Vumilia tu hela itakwisha atarejea tena ili umtunze tena, lakini la uhakika ni kuwa kama ulivyokula kiapo kuwa nae kwa raha na tabu basi na la tatu ni kuwa nae katika kuchangia maradhi.

Hili ndio tatizo la pingu za maisha!
 
Back
Top Bottom