Tatizo kwenye ndoa yangu naomba msaada

Daaah
Mwanamke ana safari ndefu kwa kweli. Hivi inapotokea mwanamke anaamua kutembea na mume wa mtu mpaka anapachikwa mimba, ni kwamba anakuwa amezidiwa vishawishi na mwanaume (yaan ule msemo usemao "mwanamke ni kiumbe dhaifu") au ni kwamba anafanya makusudi ili kubomoa ndoa ya mwenzie?
 
Mimi ni binti wa miaka kama 30 hivi nina watoto wawili niko kwny ndoa ya kikristo kwa miaka mitano kwa sasa, Nimekuwa ninapata matatizo kwenye ndoa yangu mara kwa mara mimi na mume wangu, kiukweli naweza sijakaa kufurahia raha ya ndoa ni machungu tu mara nyingi. nina elimu ya kutosha nina kazi ya uhakika na mume wangu pia as well amenizidi kipato. Toka nimeanza maisha ya ndoa mimi ni kugombana na wasichana wake kwenye simu tu anatoka Asha, anaingia Hadija, akitoka anaingia ashura mpaka sasa hawahesabiki, kipindi chote hiko nimemvumilia nikijua ni utoto unamsumbua. inafika mahali mpaka anakuwa down mpaka kipato kinakuwa tabu kwake anakua amelost anakuwa na mapenzi sana na mimi tunajitahidi pamoja tunainuka.

Sasa hivi karibuni amehama kazi kimkoa nilipo mimi ameenda mkoa mwingine kabla ya kuhama kulikuwa na ugomvi juu ya msichana fulani alikuwa anatembea nae, kiukweli sijawahi kufika kwake cause nilikuwa pregnant kwa wakati huo na hata baada ya kujifungua nikawa nalea mtoto pia job na niliona si vizuri kusumbua watoto kusafiri safiri especially mtoto mchanga na pia sababu alikuwa anakuja kuja mara kwa mara. Ikapita muda kidogo almost miezi miwili hajakuja nyumbani ila pesa akawa anatuma kama kawaida. juzi juzi kaja home akadai simu yake imezima chaji sikushtuka cause namjua tabia yake. asubuhi naenda job nikatumiwa sms na yule msichana anaetembea nae tht nimwambie mume wangu awashe simu anataka pesa ya cliniki dizaini ana mimba yake. nilikuwa namjibu kistaarabu yule dada amenitukana saaaana. ok nikamwambia mwenzangu akaleta visingizio vya hapa na pale, nilikuwa kazini niliporudi home sijamkuta mume wangu akawa amesafiri mkoa anaofanya kazi, siku iliyofuatia nilienda ule mkoa anaofanya kazi cause hajaacha hata pesa ya kutumia home namimi naishi na mama mkwe wangu na watoto wawili home.

Nilipofika huko mkoani kwake nilikuta dalili zote za mtu kuishi na hawala mule ndani, nilikuta mafuta, na vikolokolo vyote vya wanawake. alikiri mbele ya ndugu yangu kuwa huyo mtu anakujaga mara moja moja kiukweli niliumia saana. tukalala asubuhi akaanza kuniambia maneno ya kijeuri tht huyo mwanamke hata nikimkuta pale kwake tutakaa wote na anaweza kuja huku home nilipo yaani popote atapoenda atakuwepo yule hawala cause ana mimba yake. nikamwacha nimerudi huku nilipo nikijua tatizo limeshakua kubwa na nahitaji kulitatua. NIKO NJIA PANDA SIJUI NITATUEJE NISAIDIENI WADAU. Maana nahisi watoto wangu mwisho wao siuoni na sijapanga watoto wangu waishi bila baba. sina la kufanya.
Binti mmoja Ndoa inamajaribu mengi sana dada angu ambayo yanakupasa kupambana nayo mengine ni majaribu ukiyashinda ndoa itendelea na ukiyashindwa ndoa nayo imekwisha,Na kwa sababu we ni mkristo jaribu kausali sana kwani hakuna lisilowezeka kwa baba yetu. Na pia usifiche hayo matatizo ya mumeo jaribu kuwashirikisha hata wasimamizi wenu wa ndoa katia swala hili pamoja na ndugu wa karibu na mumeo.
Ila suluhisho si kuwaza kuachana na mumeo hilo ni jaribu lako na wewe tu ndiye wakumbadilisha mumeo.
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom