Tatizo kubwa la CHADEMA ni nongwa kwa wabunge 19 waliowafukuza kwenye chama bila kufuata taratibu na kanuni za chama

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Napenda kusema kwamba viongozi wa CHADEMA na kundi linaowaunga mkono waache nongwa kwa wabunge 19 walioapishwa na Spika Job Ndugai mwaka 2020 kwani kuwafukuza kwao kwenye chama bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kanuni za chama chao haimanishi ni rahisi kuchukua na ubunge wao mojakwamoja acheni u vasco dagama ambao hauna tija mmeshawafukuza mnajadili ubunge wao wa nini.

Kama mlikosea taratibu za kuwafukuza kwenye chama mnataka iwe rahisi na kufukuzwa ubunge? Nyie ni watu wa aina gani mbona mnapiga miluzi mingi ambayo haina tija kwa taifa.

Muangalie vizuri katiba yenu mmekurupuka kufanya maamuzi kumbukeni ndani ya hao wabunge 19 kulikuwa na kiongozi wa BAWACHA na mnajuwa vyema kabisa taratibu na kanuni za kuweza kumfukuza kwenye chama sasa kwa vile mmeshazoea kuburuza wanachama wenu naona hili nalo mmekurupuka.

Nawatakia kila la heri katika mapambano ambayo sion kama yanatija. Narudia kama mmeshawafukuza msiwafuatefuate barua mlipeleka kwa spika mmeshamaliza mambo mengine achieni ofisi ya spika yenyewe.
 
Mimi nasema kama sahihi ya katibu mkuu wa chama ilighushiwa sahivi ningeona shauri lipo kwenye vyombo vya sheria na angesema aliyekughushi sahihi hiyo ni nani hadi ikapelekea kuapishwa kwao.
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi
Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
 
1. Hawakwenda kihalali bungeni, wamegushi.

2. Halima hakufukuzwa kwa makosa aliyofanya kama mwenyekiti wa Bawacha, hivyo adhabu yake ni halali.
 
Mimi nasema kama sahihi ya katibu mkuu wa chama ilighushiwa sahivi ningeona shauri lipo kwenye vyombo vya sheria na angesema aliyekughushi sahihi hiyo ni nani hadi ikapelekea kuapishwa kwao.
Msajiri wa vyama vya siasa atuambie barua ya wabunge hao 19 alipokea kutoka kwa nani? simple & clear tutampata aliyeghushi sahihi tusitumie nguvu kubwa.
 
Back
Top Bottom