BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Mnaochangia mmeoa au mnachangia tu kwa uzoefu wa kusoma kwenye vitabu vya udaku.? Kuanzia wadhamini nimewaeleza na walishachoka kumweleza na wakasema hatuwezi kuongea na sikio la kufa. wazazi wake walishamwambia na kumwonya na kumfunda mara ya pili na wakaniomba nirudi kukaa naye akileta shida niwaambie tena . Hii ndo ni mojawapo ya sababu kuwa hathubutu kabisa kwenda kwao nikimfukuza. NINGEKUWA MI NINA MATATIZO HAWA MASHAHIDI WOTE INCLUDING WAZAZI WAKE TENA WENYE UWEZO WASINGEMWONYA NA KUMWEKA KIKAO.
Dah! Kuwekwa kikao na Wazazi wake si ushahidi kama mkeo ndiye mwenye matatizo. Vitabu vya udaku ndiyo vipi hivyo? ni nani mtunzi wa hivyo vitabu? Badilika Kaka ili uishi vizuri na mkeo au utakuja kupata kimeo hapo ndio utajuta kuzaliwa na kumkumbuka mkeo huyu ambaye anajaribu kadri ya uwezo wake kukuridhisha lakini huridhiki. Hakuna binadamu ambaye yuko perfect lakini inaelekea matatizo ya mkeo si makubwa kiasi hicho na unaweza kabisa kuyasamehe lakini hutaki kufanya hivyo. Watu wanakupa ushauri wa bure ufanyie kazi na pia ubadilike vinginevyo utapoteza mke na kubaki na majuto mjukuu.