Tathmini ya uchaguzi wa Urais katika majiji (Arusha, Dar, Mbeya, Mwanza)

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Wakuu!
Hii ni tathmini niliyoifanya kwa mikoa iliyokuwa na hamasa kubwa katika kipindi hiki cha uchaguzi. Karibuni muangalie hizi takwimu na mtoe maoni yenu, maoni yangu yatafuatia baadae.

Katika mikoa minne yani Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza

kura zilizopigwa ni 4,141,574 sawa na 26.56% ya kura zote

Arusha UKAWA imeizidi CCM kwa kura 308,209
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 5 CCM 1 (1 bado, AR Mjini)

Dar es Salaam UKAWA imeizidi CCM kwa kura 100,640
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa moja la Ilala na kushinda viti vya ubunge 6 CCM 4

Mbeya CCM imeizidi UKAWA kwa kura 69,189

ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa Tunduma na Mbeya Mjini na kushinda viti vya ubunge 9 UKAWA 4

Mwanza CCM imeizidi UKAWA kwa kura 306,222
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 8 UKAWA 1

Hali hii inatoa picha gani katika matokeo ya jumla?
 
Nadhani ndiyo sababu kuu iliyofanya kuwa ingawa jiji la Dar ndipo ambapo kituo cha kutangazia matokeo cha Mwalimu Nyerere, lakini jiji hilo ndilo lilikuwa la mwisho kutangaziwa kura zake hizo za Urais.

Hata hivyo nimefuatilia matokeo hayo yalipokuwa yanatangazwa, nilichoshangazwa nacho kupita kiasi ni asilimia zilizofanana katika majimbo matatu ya Dar.

Katika matokeo yaliyotolewa na NEC ilitangazwa kuwa jimbo la Mbagala Magufuli amepata 88,023 sawa na ssilimia 47, na Lowassa kapata 94,775 sawa na asilimia 51 ya kura zote zilizopigwa jimboni humo.

Katika jimbo la Ukonga ilitangazwa kuwa Magufuli kapata kura 86,288 sawa na asilimia 47 na Lowassa kapata kura 92,145 sawa na asilimia 51 ya kura zilizopigwa.

Katika jimbo la Kawe nalo ikatangazwa kuwa Magufuli kapata kura 84,870 sawa na asilimia 47 na Lowassa kapata kura 90,665 sawa na asilimia 51 ya kura zote zilizopigwa jimboni humo.
 
Nadhani ndiyo sababu kuu iliyofanya kuwa ingawa jiji la Dar ndipo ambapo kituo cha kutangazia matokeo cha Mwalimu Nyerere, lakini jiji hilo ndilo lilikuwa la mwisho kutangaziwa kura zake hizo za Urais.

Hata hivyo nimefuatilia matokeo hayo yalipokuwa yanatangazwa, nilichoshangazwa nacho kupota kiasi ni asilimia zilizofanana katika majimbo matatu ya Dar.

Katika matokeo yaliyotolewa na NEC ilitangazwa kuwa jimbo la Mbagala Magufuli amepata 88,023 sawa na ssilimia 47, na Lowassa kapata 94,775 sawa na asilimia 51.

Katika jimbo la Ukpnga ilitangazwa kuwa Magufuli kapata kura 86,288 sawa na asilimia 47 na Lowassa kapata kura 92,145 sawa na asilimia 51.

Katika jimbo la Kawe nalo ikatangazwa kuwa Magufuli kapata kura 88,023 sawa na asilimia 47 na Lowassa kapata kura 90,665 sawa na asilimia 51.

Hiyo 51 kwa 47 inatia mashaka.

Mi nilitegemea kwa kura za Dar kila chama kitakuwa na majumuisho yake mapema iwezekanavyo kwasababu matokeo yalibandikwa moja kwa moja kwenye vituo.
Cha ajabu Kibamba wanatangaza matokeo kabla ya mbagala wakati baadhi ya vituo vilipiga kura siku ya pili kwa kibamba
 
Wakuu!
Hii ni tathmini niliyoifanya kwa mikoa iliyokuwa na hamasa kubwa katika kipindi hiki cha uchaguzi. Karibuni muangalie hizi takwimu na mtoe maoni yenu, maoni yangu yatafuatia baadae.

Katika mikoa minne yani Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza

kura zilizopigwa ni 4,141,574 sawa na 26.56% ya kura zote

Arusha UKAWA imeizidi CCM kwa kura 308,209
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 5 CCM 1 (1 bado, AR Mjini)

Dar es Salaam UKAWA imeizidi CCM kwa kura 100,640
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa moja la Ilala na kushinda viti vya ubunge 6 CCM 4

Mbeya CCM imeizidi UKAWA kwa kura 69,189

ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa Tunduma na Mbeya Mjini na kushinda viti vya ubunge 9 UKAWA 4

Mwanza CCM imeizidi UKAWA kwa kura 306,222
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 8 UKAWA 1

Hali hii inatoa picha gani katika matokeo ya jumla?

Hii ni data nzuri ya kuchambulia si mwenedo tu wa kura bali pia mwenendo wa ajenda ya mabadiliko. Mimi ningesema kwamba hii mikoa ndio imejibainisha kuwa NGOMe ya ajenda ya MABADILIKO. Hadi mchakato wa kuteua wagombea wa urais katika vyama vikuu vya siasa, hawa watu walikuwa kitu kimoja - wote walikuwa wanaongoza harakati za mabadiliko. Upepo ulibadilika mara tu baada ya CCM kumteua ndugu Magufuli ambapo ukanda, lakini zaidi zaidi ukabila ulijitokeza kuwa mzito kuliko mabadiliko na hivyo kufanya ngome ya mabadiliko ipwaye - hence hayo matokeo ya Mwanza. Si kweli kwa wale wanaosema kuwa watu wa Arusha na Kilimanjaro ndio wanaendekeza ukanda. La hasha, hawa walindelea na msimamo uliokuwa umeishakubaliwa na wote wa kuvunjilia mbali mfumo kandamaizi na fisadi wa ccm. Ni watu wa Mwanza ambao walijitoa katika safari ya mabadiliko. Hili ni jambo la kawaida kwa binadamu na katika jamii mbalimbali. Hata Marekani ambaye ni mwalimu wa demokrasia katika chaguzi mbili zilizomweka Obama madarakani haikuwa siri kuwa asilimia zaidi ya 90 ya Wamarekani weusi walikuwa wanampigia kura simply because ni mweusi mwenzao. Lakini hii hakuzuia wengine ambao si weusi kumpigia kura kwa kuangalia vigezo vingine. Mswahili hunena 'damu ni nzito kuliko maji'. Katika hali ya uchaguzi huu, kwa Mwanza (ngome ya mabadiliko iliyobomoka) 'mabadiliko' yalionekana kama maji mbele ya 'Msukuma mwenzetu' ambayo ni damu.
Hii ina maana gani katika siasa za kesho za Tanzania? Pamoja na sifa nyingine za msingi, ukanda, ukabila, umkoa, u-whatever havitakuwa tena vitu vya kubeza au kuwekwa upenuni katika mikakati ya michakato ya kuteua wagombea na kuendesha kampeni za urais. Na visichukiliwe kwa mtazamo hasi, bali ni jinsi gani ya kuvi-manage for positive outcomes. Vipo na vitaendelea kuwepo.
 
Mystery hiyo kali. Hizo namba zinaendanaendana sana.
That is reality, fuatilia hizo figure na hata NEC hawawezi kuzikanusha, kwa kuwa walikuwa wanazitangaza moja kwa moja na sisi wananchi tulikuwa tunazinakili.

Ndiyo maana sishangazwi sana na juhudi kubwa sana inayofanywa na vyombo vya dola kuvamia taasisi mbalimbali wanazozihisi zinafanya shughuli ya kufanya majumuisho ya kura hizo kama walivyofanya kwa wale vijana wa Ukawa na Tume ya haki za binadamu.

Lakini cha kushangaza kupita kiasi wakati vyombo vya dola vikivamia taasisi hizo vijana wa Makamba walikuwa wakiendelea kufanya shughuli hizo hizo pale Mlimani City bila kubughuthiwa kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Hii ni data nzuri ya kuchambulia si mwenedo tu wa kura bali pia mwenendo wa ajenda ya mabadiliko. Mimi ningesema kwamba hii mikoa ndio imejibainisha kuwa NGOMe ya ajenda ya MABADILIKO. Hadi mchakato wa kuteua wagombea wa urais katika vyama vikuu vya siasa, hawa watu walikuwa kitu kimoja - wote walikuwa wanaongoza harakati za mabadiliko. Upepo ulibadilika mara tu baada ya CCM kumteua ndugu Magufuli ambapo ukanda, lakini zaidi zaidi ukabila ulijitokeza kuwa mzito kuliko mabadiliko na hivyo kufanya ngome ya mabadiliko ipwaye - hence hayo matokeo ya Mwanza. Si kweli kwa wale wanaosema kuwa watu wa Arusha na Kilimanjaro ndio wanaendekeza ukanda. La hasha, hawa walindelea na msimamo uliokuwa umeishakubaliwa na wote wa kuvunjilia mbali mfumo kandamaizi na fisadi wa ccm. Ni watu wa Mwanza ambao walijitoa katika safari ya mabadiliko. Hili ni jambo la kawaida kwa binadamu na katika jamii mbalimbali. Hata Marekani ambaye ni mwalimu wa demokrasia katika chaguzi mbili zilizomweka Obama madarakani haikuwa siri kuwa asilimia zaidi ya 90 ya Wamarekani weusi walikuwa wanampigia kura simply because ni mweusi mwenzao. Lakini hii hakuzuia wengine ambao si weusi kumpigia kura kwa kuangalia vigezo vingine. Mswahili hunena 'damu ni nzito kuliko maji'. Katika hali ya uchaguzi huu, kwa Mwanza (ngome ya mabadiliko iliyobomoka) 'mabadiliko' yalionekana kama maji mbele ya 'Msukuma mwenzetu' ambayo ni damu.
Hii ina maana gani katika siasa za kesho za Tanzania? Pamoja na sifa nyingine za msingi, ukanda, ukabila, umkoa, u-whatever havitakuwa tena vitu vya kubeza au kuwekwa upenuni katika mikakati ya michakato ya kuteua wagombea na kuendesha kampeni za urais. Na visichukiliwe kwa mtazamo hasi, bali ni jinsi gani ya kuvi-manage for positive outcomes. Vipo na vitaendelea kuwepo.

Well said...
 
Vile vile hii vamia vamia ya vyombo vya dola, kwa 'maagizo' ya watawala kwa wale wanaoonekana wanafanya shughuli halali kabisa ya kufanya tallying ya matokeo kutokana na form zinazobandikwa vituoni, inaonyesha wazi namna watawala wanavyoonyesha guilty consciousness.

Kwa kuwa haiingii akilini ni kwa vipi CCM waruhusiwe kufanya majumuisho yao kwenye vituo vyao vya Mlimani City na Double Tree Hotel, lakini wakati huo huo vijana wa Ukawa na wale wa Tume ya Haki za binadamu ambao pia walikuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi huo wavamiwe na vifaa vyao vya kazi kama computers nk. kuwa confiscated na watumishi wa taasisi hizo kurundikwa ndani na kufunguliwa mashitaka ya kubambikiwa ya Human trafficking!
 
Kuteuliwa kwa Magufuli hakutokani na kura. MKitaka kujustify hii biashara kwa kura, mtakuwa mnakosea. Linganisheni na jumba la maigizo la kaole au original komedi. Mkianza kulitafiti kisayansi mtazeeka hadi mfie maabara.
 
Shutup.Tumeishamaliza. Rais ni Dr John P Magufuli aliyechukia anywe sumu afe
Nyinyi magamba mnajifanya kama nchi hii mmepewa hati miliki na Mwenyezi Mungu ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia?!

Ndiyo maana kwa kutumia wingi wenu bungeni hamko tayari nchi hii kuwe na Katiba mpya yenye kuweka uwanja sawa kwa vyama vyote vya siasa.

Hivi inawezekanaje tuwe na Katiba ambayo Rais wa nchi ambaye ndiyo pia Mwenyekiti wa chama tawala apewe mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi pamoja na wajumbe wake wote na hapo hapo Katiba hiyo iwe na ibara inayosema Mwenyekiti wa Tume anapomtangaza mshindi wa Urais hakuna chombo chochote cha sheria kitakachokuwa na uwezo wa kusikiliza malalamiko yoyote yanayohusiana na uchaguzi huo?!

Katika mazingira hayo ninaona nchi yetu theoritically yaweza kujiita nchi yenye mfumo wa vyama vingi lakini practically ni nchi yenye mfumo wa chama kimoja.
 
Mystery, kuhusu hao vijana kukamatwa, Mallya na/au Yericko walisema kuna maeneo kama hayo 50. Kwanini hiyo ya Dar lawama zimekua nyingi?

Nadhani tulidanganywa au hiyo ndo pekee ina raw data hivi kwamba ikifutwa hiyo ndo basi tena. Zingine zilikua hazitunzi au zilitupiwa virusi kama JF. Na backup huenda ilikua 'neutral' kituo cha sheria.

Isije kuwa kuna syndicate au zaidi ya moja zipo kazini. Rostam ashaanzishiwa uzi alivyotaka kuiba uchaguzi. Alikua gamba na mamvi. Kabla walikua maswahiba na mkwere. So gemu linakua nani atamzidi mwenzie kete.

Muda utatujuza lakini ukishaona FAMILIA inapambana nchi nzima kupata matokeo 'yao' jua ni zaidi ya tusikiayo.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu!
Hii ni tathmini niliyoifanya kwa mikoa iliyokuwa na hamasa kubwa katika kipindi hiki cha uchaguzi. Karibuni muangalie hizi takwimu na mtoe maoni yenu, maoni yangu yatafuatia baadae.

Katika mikoa minne yani Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza

kura zilizopigwa ni 4,141,574 sawa na 26.56% ya kura zote

Arusha UKAWA imeizidi CCM kwa kura 308,209
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 5 CCM 1 (1 bado, AR Mjini)

Dar es Salaam UKAWA imeizidi CCM kwa kura 100,640
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa moja la Ilala na kushinda viti vya ubunge 6 CCM 4

Mbeya CCM imeizidi UKAWA kwa kura 69,189

ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote isipokuwa Tunduma na Mbeya Mjini na kushinda viti vya ubunge 9 UKAWA 4

Mwanza CCM imeizidi UKAWA kwa kura 306,222
ikiwa imeongoza kwa kura katika majimbo yote na kushinda viti vya ubunge 8 UKAWA 1

Hali hii inatoa picha gani katika matokeo ya jumla?

Kuna jumla ya kura 784260.

Tuki toa ACT- wasiliti, Rungwe, Dovutwa, TLP, nk kama
2000 tu.

Zilizoharibika kama 50,0000 hivi make hizi mikoa watu wako na shule kichwani.

Je kura 3,357,314 zimeenda wapi? (Assume zibaki 3M).
 
Nyinyi magamba mnajifanya kama nchi hii mmepewa hati miliki na Mwenyezi Mungu ...

Wengi walio CCMscrow wanadhani upinzani unachotaka ni kutawala tu. Ila kidogo kidogo wanaelewa.

Lowassa ni juzi tu hakufanya jitihada yoyote kubadili katiba iwe ya wananchi. Sasa kimenuka kule kaja huku kakutana na hali ambayo tumekua nayo tangu 1995.

Na hao magamba wengine wakidhani ni sawa, siku yaja watapogundua CCMscrow imehodhiwa na kakikundi kadogo ambako kameamua kujitajirisha kwa namna yoyote ile, ndipo watakumbuka sana walivyobeza katiba ya Warioba.

Kuna kitu hakipo sawa kabisa kwenye namna CCMscrow wanavyofikiria/fikirishwa.
 
Kuna jumla ya kura 784260.

Tuki toa ACT- wasiliti, Rungwe, Dovutwa, TLP, nk kama
2000 tu.

Zilizoharibika kama 50,0000 hivi make hizi mikoa watu wako na shule kichwani.

Je kura 3,357,314 zimeenda wapi? (Assume zibaki 3M).

Nadhani ye kaonyesha tofauti ya (kuzidiana kwa) kura na sio idadi ya zote kwa kila chama.
 
Back
Top Bottom