MNYISANZU
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 7,048
- 1,102
Wakuu, nadhani tuanze kupima upepo wa kisiasa wa CHADEMA ukoje majimboni mwetu.
Je kama uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda jimboni kwako leo?.
Kwa kuanzia jimboni kwangu Iramba mashariki dalili zinaonesha dhahiri ya kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda katika nafasi ya ubunge kutokana na kupwaya sana kwa mbunge aliyepo madarakani, Salome D Mwambu [ CCM ].
Mbunge wa sasa ameshindwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kama tatizo sugu la maji, barabara mbovu, huduma mbovu za afya, ukosefu wa walimu na vitabu mashuleni, nk. Mbunge wa sasa haongei na wananchi, ni mbaguzi wa kimaeneo na pia ni mgonjwa. Hajatimiza ahadi zake hata moja.
Katika nafasi ya udiwani na urais bado shughuli ni pevu kwani tathimini inaonyesha CCM na CHADEMA watagawana kura kwa usawa.
Je hali ikoje jimboni kwako kama uchaguzi ungefanyika leo?