Tathmini ya kisiasa: Hali ya CHADEMA ikoje jimboni kwako?

Mimi huwa nasikitika sana kuona Watanzania wenzangu hawaelewi kabisa viongozi wao wanatakiwa kuwajibika kwa lipi. Kama mtu bado haelewi kwamba ubovu wa barabara ni kushindwa kwa mbunge, tumekwisha. Kama barabara ni mbovu mbunge anawajibika moja kwa moja maana ameshindwa kuisimamia serikali kujenga hiyo barabara. Huyo anafikiri kazi ya mbunge ni kugawa kanga, kofia na Tsh 5000. TUBADILIKE JAMANI
Hata mimi mkuu watu wa aina hiyo huwa wananiacha hoi sana. Sijui ni ufinyu wa mawazo au wamezoeshwa vibaya na CCM?
 
JIMBO LA MOROGORO KUSINI:- Nimetembelea kata kadhaa na Vijiji vyake. Hali ya CHADEMA kiuongozi ni mbovu sana ila Wananchi wanataka mabadiliko makubwa 2015 kwakuwa Mbunge wao Bw.INNOCENT KALOGERIES(ccm) kauza mbuga yao ya GONABISI kwa MWARABU wa Oman chini ya jumuiya ya kifisadi ya JUKUM. Sasa wanavijiji wa Magogoni, Dutumi na kwingineko wanauawa kwa risasi na mwekezaji kila wanapoingia mbugani kutafuta kitoweo.
 
Ahsante mkuu kwa correction. Nilikuwa namaanisha Hawa Ng'umbi. Mshindani wa Mnyika 2010. Kero ya maji Ubungo Mnyika ameitatua kwa kiasi gani?
Kwa watu wa mabondeni, maji yanapatikana kwa mgao, ila kwenye miinuko, mradi ule wa world bank hakusimamiwa vizuri. Maana njia za mabomba nyngine zinatoka mabondeni kwenda milimani. Kuna marekebisho makubwa yanahitajika. Haya yalitokea kabla ya Mnyika. Lakini mradi wenyewe haujaisha, ndio maana Myika aliwaka sana Bungeni. sasa kazi iko katika utekelezaji, maana kuna pesa imetengwa. Mnyika anajitahidi sana ukilinganisha na wabunge waliopita. Hatuna shida ya mbunge mwingine kwa sasa, na hata 2015.
 
Taarifa fupi kwa njia ya simu Dr. Slaa amefanya mkutano kijijini Kagenyi, jimbo la Kyerwa. Nimeambiwa watu wanahamasika sana na vuvugu la mabadiliko. Kyerwa ni jimbo liliko mikononi mwa uwakilshi wa magamba lakini watu wameonesha mwelekeo mkubwa wa mabadiliko 2015.
 
JIMBO LA MOROGORO KUSINI:- Nimetembelea kata kadhaa na Vijiji vyake. Hali ya CHADEMA kiuongozi ni mbovu sana ila Wananchi wanataka mabadiliko makubwa 2015 kwakuwa Mbunge wao Bw.INNOCENT KALOGERIES(ccm) kauza mbuga yao ya GONABISI kwa MWARABU wa Oman chini ya jumuiya ya kifisadi ya JUKUM. Sasa wanavijiji wa Magogoni, Dutumi na kwingineko wanauawa kwa risasi na mwekezaji kila wanapoingia mbugani kutafuta kitoweo.
Ahsante sana kwa taarifa. Naamini viongozi wa CHADEMA watalifanyia kazi hili.
 
Kwa watu wa mabondeni, maji yanapatikana kwa mgao, ila kwenye miinuko, mradi ule wa world bank hakusimamiwa vizuri. Maana njia za mabomba nyngine zinatoka mabondeni kwenda milimani. Kuna marekebisho makubwa yanahitajika. Haya yalitokea kabla ya Mnyika. Lakini mradi wenyewe haujaisha, ndio maana Myika aliwaka sana Bungeni. sasa kazi iko katika utekelezaji, maana kuna pesa imetengwa. Mnyika anajitahidi sana ukilinganisha na wabunge waliopita. Hatuna shida ya mbunge mwingine kwa sasa, na hata 2015.
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Wabunge wengine waige mfano wa Mnyika. Long live CDM
 
Kwanza kaa ukitambua kwamba kama ni ugonjwa kila mmoja anaweza kuugua ukiwemo na wewe,kwa hiyo usimnyanyapae kwa hili lake la ugonjwa,pili suala la ujenzi wa barabara na hayo mengine meengi uliyoyaleta sio kazi ya Mbunge,ni kazi ya serikali,nambie mbunge ambaye ameweza kuwajengea wananchi barabara hata kilomita tano tu kwa pesa zake,kwa hiyo huwezi kufanya tathmini kubwa kama hiyo kwa hivi vigezo ulivyovitoa,nenda kajipange urudi humu ndani vizuri.

Hizo ndio sera zenu zilipotufikisha, kiktwana kondo ubungE na uenyekiti bodi ya korosho mpaka anakaribia kufa, kingunge mbungeni na waziri mpaka anakaribia kufa, huyu mwingine mmeunda mpaka wizara anakula tu kodi zetu.
Yani kwa mwendo huo lazima mende na maji, 2015 hamna chenu.
 
Taarifa fupi kwa njia ya simu Dr. Slaa amefanya mkutano kijijini Kagenyi, jimbo la Kyerwa. Nimeambiwa watu wanahamasika sana na vuvugu la mabadiliko. Kyerwa ni jimbo liliko mikononi mwa uwakilshi wa magamba lakini watu wameonesha mwelekeo mkubwa wa mabadiliko 2015.
This is a good news. Kinachotakiwa ni ufuatiliaje baada ya mkutano kwisha. Viongozi wa eneo husika wawajibike katika ufuatiliaje wa wanachama.
 
Hizo ndio sera zenu zilipotufikisha, kiktwana kondo ubungE na uenyekiti bodi ya korosho mpaka anakaribia kufa, kingunge mbungeni na waziri mpaka anakaribia kufa, huyu mwingine mmeunda mpaka wizara anakula tu kodi zetu.
Yani kwa mwendo huo lazima mende na maji, 2015 hamna chenu.
Ni kweli kabisa mkuu mfumo wa namna hii wa uongozi ndio uliotufikisha hapa. Umetuletea umaskini, ombwe la uongozi na ufisadi. Hata hivyo kikomo chao ni 2015.
 
Laiti kama tungepata nusu ya bunge wawe chadema hata kama raisi awe ccm tungeendelea aiseee
 
Kwanza kaa ukitambua kwamba kama ni ugonjwa kila mmoja anaweza kuugua ukiwemo na wewe,kwa hiyo usimnyanyapae kwa hili lake la ugonjwa,pili suala la ujenzi wa barabara na hayo mengine meengi uliyoyaleta sio kazi ya Mbunge,ni kazi ya serikali,nambie mbunge ambaye ameweza kuwajengea wananchi barabara hata kilomita tano tu kwa pesa zake,kwa hiyo huwezi kufanya tathmini kubwa kama hiyo kwa hivi vigezo ulivyovitoa,nenda kajipange urudi humu ndani vizuri.
Toa uongo hapa wewe!! Serikali ni ya chama gani! Ni nini kazi za mbunge!?
 
Hapa, ludewa mkuu kwahakika Ludewa ilikuwa ngome kuu ya CCM na CDM haikuwa na Diwani hata moja, lakini kwa uchaguzi wa madiwani uliopita CDM wameshinda kata moja, hivyo kuanzisha CDM ludewa, kwa hiyo hali nzuri, Japo kwa mbunge Deo, INAHAITAJI KAZI YA ZIADA, kwa uraisi kama uchaguzi ufanyike kesho Dr waukeli anapita.
 
Mkuu,

Uchambuzi wako ni mzuri. Kuna magamba hapa jf upita yakiuliza inakuwaje Dr. Slaa anasadikika alipata kura nyingi wakati CDM ilipata wabunge wachache?
 
JIMBO LA MAGU ni wazi kwa CHADEMA Mbunge wake bwana Festus Limbu alishabakia kununua tu pamba ya wakulima wa Magu kwa bei ya dharau huku yeye ndo mwenyekiti wa Board yapamba Taifa, hafanyi tena kazi zake za kibunge kwa maana ya kushiriki katika harakati za kimaendeleo na jamii yake. Wanainchi wanahasira naye ikikumbukwa kwamba jamaa alilazimisha ushindi uchaguzi uliopita. Hapa Chadema waje tu na mgombea makini na mwenye vission ya ukweli, nafasi ni yao.
 
Ahsante kwa taarifa mkuu. Hebu tudokeze japo hali ya CDM kwa ujumla ikoje? Ina viongozi imara ngazi ya wilaya, kata na kwenye mashina? Uchaguzi wa mwaka 2010 CDM ilikuwa na mgombea?
 
Mkuu,

Uchambuzi wako ni mzuri. Kuna magamba hapa jf upita yakiuliza inakuwaje Dr. Slaa anasadikika alipata kura nyingi wakati CDM ilipata wabunge wachache?
Mkuu watu wa magamba huwa wananiacha hoi na akili zao mfu. Huwa nawaita 'brain dead ******'
 
Hapa, ludewa mkuu kwahakika Ludewa ilikuwa ngome kuu ya CCM na CDM haikuwa na Diwani hata moja, lakini kwa uchaguzi wa madiwani uliopita CDM wameshinda kata moja, hivyo kuanzisha CDM ludewa, kwa hiyo hali nzuri, Japo kwa mbunge Deo, INAHAITAJI KAZI YA ZIADA, kwa uraisi kama uchaguzi ufanyike kesho Dr waukeli anapita.
Nilifurahishwa sana na matokeo ya udiwani katika hiyo kata hasa ikizingatiwa ili kuwa chini ya CCM. Kwa kweli hiyo kata imefungua ukurasa mpya wa kisiasa wilayani Ludewa. Je kuna viongozi thabiti wa CDM huko Ludewa?
 
Kwa hapa Tunduma, naishukuru jf kwa kufanikiwa kumwamusha mbunge wetu mh.Silinde. Tokea zimeanza mada mfululizo hapa jf kuhusu hatma ya jimbo la Mbozi magharibi Silinde alikurupuka toka usingizini.. Sasa hivi kila kitu kinakwenda sawa, kuna barabara moja ya mtaa imejengwa kwa kiwango cha lami, bila kusahau barabara ya katikati ya mji ilikua na mahandaki badala ya mashimo sasa hivi imepigwa lami na mitaro kuzibuliwa vizuri sasa hivi mjini panapendeza..Funga kazi ni visima vya maji vinavyoendelea kuchimbwa maeneo ya shule za msingi japo upatikanaje wa maji umekua ni mgumu lakini tunashukuru kwa juhudi zake.kwa maeneo ya pembeni ya mji kama vijijini sina data za kutosha, lakini kwa hapa Tunduma mjini 2015 ni chadema tena.!
 
Nashukuru kwa taarifa hii mkuu. Pia nimefurahi kusikia kuwa JF imemwamsha kutoka usingizini Kamanda Silinde. Je hali ikoje kwa upande wa Mbozi mashariki kwa Zambi?
 
mkuu kwa upande wa mbozi mashariki naamini kule ni Chadema mwanzo mwisho,ikumbukwe kuwa wananchi wa kule walilalamika sana jimbo lile kudondokea kwenye mikono ya ccm katika mazingira tatanishi,hali iyofikia wananchi kuvamia nyumba ya Zambi kupiga mawe na kutaka kuchoma moto,ndio maana ilifikia mahali wananchi wakatangaza kuwa mbunge wao ni Silinde wa chadema badala Zambi wa ccm...inaamiinika chadema ilishinda majimbo yote mawili Mbozi magharibi na mashari,Kitu ambacho ccm hawakua tayari kuachia majimbo yote mawili. Hivyo waliaziamia lazima jimbo moja wabaki nalo hasa jimbo la Silinde ambalo lipo mpakani na lina vyanzo vingi vya mapato,lakini kulina na msimamo wa vijana wa Tunduma ilikua ngumu sana kuchakachua naamini yangetokea maafa makubwa sana ukizingatia Silinde alikuja na nauli tu toka chuoni hivyo hawakua tayari kuzulumiwa. Wakaangalia wapi walipo wanyonge wakaamua kuchukua mbozi mashariki..!
 
Back
Top Bottom