Tathmini: Bomoa Bomoa Maeneo Ya Mambondeni DAR Imezaa Matunda, Mvua Hazijaleta Mdhara

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Miaka iliyopita majira kama haya jijini Dar es Salaam watu walikuwa wanalia vilio tofauti tofauti kutokana na athari za mvua zilizonyesha. Wapo waliokosa mahali pa kuishi, wwngine kupoteza mali na hata wengine ndugu zao kupoteza Maisha.

Mwaka huu ni tofauti kabisa. Pamoja na mvua kuonekana kuwa nyingi kuliko hata miaka iliyopita, hakuna madhara makubwa yalioripotiwa kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mytake: Wale waliokuwa wanakaidi kuondoka maeneo ya mabondeni leo wanajisikiaje? Lakini pia Wale walioingiza siasa wakati wa zoezi la kuwaondoa wale waliokuwa wanaishi mabondeni leo wanajisikiaje?
Tujitafakari.
 
Madhara hayajatokea au hayakuwa riported?
Anzia hapo kujenga hoja yako
 
Miaka iliyopita majira kama haya jijini Dar es Salaam watu walikuwa wanalia vilio tofauti tofauti kutokana na athari za mvua zilizonyesha. Wapo waliokosa mahali pa kuishi, wwngine kupoteza mali na hata wengine ndugu zao kupoteza Maisha. Mwaka huu ni tofauti kabisa. Pamoja na mvua kuonekana kuwa nyingi kuliko hata miaka iliyopita, hakuna madhara makubwa yalioripotiwa kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mytake: wale waliokuwa wanakaidi kuondoka maeneo ya mabondeni leo wanajisikiaje? Lakini pia Wale walioingiza siasa wakati wa zoezi la kuwaondoa wale waliokuwa wanaishi mabondeni leo wanajisikiaje?
Tujitafakari.
Safi sana mleta mada, ila sidhani kama raia tuko hivyo, serikali inapofanya mengi kwa manufaa yetu ni wachache sana watayakubali, hasa kipindi hichi cha vyama vingi, kama simba na yanga, na ni kweli maafa yalikuwa ni machache mno, ila wakumbuka zile kelele za watu wa mabondeni na vyama vya upinzania kushikilia bango?!
Jiulize mbona hwajashika bango kuisifu serikali kwa hili?!
 
Hata kama yangetokea serikali hii sio ya kujali kabisa watu wanapokuwa na majanga..
Sana sana majanga yanatumika kama advantage ya kujinufaisha kama kule Bukoba.
 
Safi sana mleta mada, ila sidhani kama raia tuko hivyo, serikali inapofanya mengi kwa manufaa yetu ni wachache sana watayakubali, hasa kipindi hichi cha vyama vingi, kama simba na yanga, na ni kweli maafa yalikuwa ni machache mno, ila wakumbuka zile kelele za watu wa mabondeni na vyama vya upinzania kushikilia bango?!
Jiulize mbona hwajashika bango kuisifu serikali kwa hili?!
Ndiyo maana nimeileta hii mada ili wajiulize.
 
Hili ni fundisho kuwa upinzani wa Tanzania ni wa kupinga kila kitu na tunapaswa kutafakari kabla hatujaanza kufuata mkumbo
 
Safi sana mleta mada, ila sidhani kama raia tuko hivyo, serikali inapofanya mengi kwa manufaa yetu ni wachache sana watayakubali, hasa kipindi hichi cha vyama vingi, kama simba na yanga, na ni kweli maafa yalikuwa ni machache mno, ila wakumbuka zile kelele za watu wa mabondeni na vyama vya upinzania kushikilia bango?!
Jiulize mbona hwajashika bango kuisifu serikali kwa hili?!
Kiukweli hii mada huu ni wakati wake muafaka
 
Back
Top Bottom