Wakati mwingine nasikia kichinachina, kwa nchi ambayo imetawala kwa amani miaka 46 labda ndiyo sumu iliyotutia ganzi! Maana nchi zote ambazo zimepitia misuko suko zimekuwa na ujasiri wa kuangalia nyuma yake. Amefanya hivyo mama wa Liberia, Sierra Leone, na kwingine.
Halafu siyo kama vile sisi hatuna pa kuanzia; tunapo - Mkapa & Yona Deal. Kwanini tusianzie hapo tu?
Upande mwingine sidhani siri ni kubadili chama, naamini siri kubwa ni kuwa na mambo mawili makubwa ya kubadilisha:
a. Kuondoa ulazima wa Mbunge kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa na kuhakikisha kuwa mbunge akihama au kujitoa chama hapotezi Ubunge wake (anaweza kupoteza seniority kwenye kamati n.k)
b. Kuhakikisha kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inakuwa huru kweli na kumuondoa Mwanasheria Mkuu kuwa Mbunge na pia asiwe Mshauri wa Ikulu bali msimamizi wa Sheria zote (Chief Law Enforcer). Hivyo Ikulu wawe na Mwanasheria wao.
c. Jeshi la Magereza kutoka Mikononi mwa Waziri wa Mambo ya Ndani au yeyote wa Mawaziri na kuwekwa chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu au chini ya Mahakama. Na Magereza badala ya kusimamia wafungwa n.k wanakuwa ni chombo cha Mahakama ambacho wanawajibika kwa mahakama tu na ndio chombo pekee ambacho kinahakikisha maamuzi ya mahakama yanatekelezwa pale ambapo Polisi au chombo kingine hakiwezi kufanya kazi. Nina maana wanakuwa kama US Marshalls.