Tate nane!!: Hata Sierral Leone?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
BBC

Sierra Leone's new president has asked the country's anti-corruption body to probe ex-government ministers and other senior officials for alleged graft.
Ernest Bai Koroma said this would set an example by making all accountable.

He made the announcement after being presented with a an audit into the state of corruption in Sierra Leone.

The report has not been published but a copy seen by the BBC reveals widespread mismanagement in key areas such as health, tax and security.

Mr Koroma won elections in September on an anti-corruption ticket.

The BBC's Umaru Fofana in the capital, Freetown, says some Sierra Leoneans have welcomed Mr Koroma's announcement as a step in the right direction.

Others think it will further polarise the country, which remains politically divided since the presidential election.

Sierra Leone, one of the poorest countries in the world, is very slowly recovering from a decade of brutal war that ended in 2001.
 
Ipo siku, ipo siku, ipo siku nasi tutawafanyizia wahujumu uchumi wetu... wewe acha wafikirie kuwa hivi sasa wana ubavu, wanarithisha mali za umma kwa watoto wao wakifikiri tutasahau... wewe subiri..

SteveD.
 
Hiyo haitatokea chini ya utawala wa CCM! Kamwe hata kidogo.
 
Ipo siku, ipo siku, ipo siku nasi tutawafanyizia wahujumu uchumi wetu... wewe acha wafikirie kuwa hivi sasa wana ubavu, wanarithisha mali za umma kwa watoto wao wakifikiri tutasahau... wewe subiri..

SteveD.

Steve,
Hiyo siku sidhani kama iko mbali, Tanzania siyo kisiwa, mawasiliano yameongezeka na habari zinapatikana kirahisi sana, huu mwendo wa kumkoma nyani soon utazaa matunda, mafisadi wote lazima wawajibike kwa walivo tutenda, Naam kikubwa zaidi, lazima warudishe kilicho chetu!
 
Hapa tunashangaa nini wajamaa, hawa wamefanya vile kwa kuwa wameingia kwa tiketi ya chama kingine. Sisi tunafikiri kubadilisha sura ndiyo jibu badala ya mfumo, kalagha bao!
 
Hapa tunashangaa nini wajamaa, hawa wamefanya vile kwa kuwa wameingia kwa tiketi ya chama kingine. Sisi tunafikiri kubadilisha sura ndiyo jibu badala ya mfumo, kalagha bao!

Ekzaktli! Zaidi tutaendelea kuona mazingaombwe yale yale ya kina Ndumba Nangai.....ni tume ngapi zimeundwa? Mikwara mingapi imechimbwa? Wangapi wameadhibiwa? Tusipobadili watawala tusitegemee mapya....tutegemee more of the same
 
Wakati mwingine nasikia kichinachina, kwa nchi ambayo imetawala kwa amani miaka 46 labda ndiyo sumu iliyotutia ganzi! Maana nchi zote ambazo zimepitia misuko suko zimekuwa na ujasiri wa kuangalia nyuma yake. Amefanya hivyo mama wa Liberia, Sierra Leone, na kwingine.

Halafu siyo kama vile sisi hatuna pa kuanzia; tunapo - Mkapa & Yona Deal. Kwanini tusianzie hapo tu?

Upande mwingine sidhani siri ni kubadili chama, naamini siri kubwa ni kuwa na mambo mawili makubwa ya kubadilisha:

a. Kuondoa ulazima wa Mbunge kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa na kuhakikisha kuwa mbunge akihama au kujitoa chama hapotezi Ubunge wake (anaweza kupoteza seniority kwenye kamati n.k)

b. Kuhakikisha kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inakuwa huru kweli na kumuondoa Mwanasheria Mkuu kuwa Mbunge na pia asiwe Mshauri wa Ikulu bali msimamizi wa Sheria zote (Chief Law Enforcer). Hivyo Ikulu wawe na Mwanasheria wao.

c. Jeshi la Magereza kutoka Mikononi mwa Waziri wa Mambo ya Ndani au yeyote wa Mawaziri na kuwekwa chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu au chini ya Mahakama. Na Magereza badala ya kusimamia wafungwa n.k wanakuwa ni chombo cha Mahakama ambacho wanawajibika kwa mahakama tu na ndio chombo pekee ambacho kinahakikisha maamuzi ya mahakama yanatekelezwa pale ambapo Polisi au chombo kingine hakiwezi kufanya kazi. Nina maana wanakuwa kama US Marshalls.
 
Hapa tunashangaa nini wajamaa, hawa wamefanya vile kwa kuwa wameingia kwa tiketi ya chama kingine. Sisi tunafikiri kubadilisha sura ndiyo jibu badala ya mfumo, kalagha bao!

Well, not really a reliable formular, Zambia with Chiluba did the opposite.
 
Well, not real a reliable formular Zambia with Chiluba did the opposite.

Sawa...inawezekana hakuna formula lakini hawa CCM wameunda tume baada ya tume. Tuna hadi kitengo maalumu cha kuzuia rushwa. Nini kimetendeka? Wapi tume ya Warioba? Kwetu sisi, inawezekana ikawa ndiyo formula itakayofanya kazi. Mi nimechoka na maneno, nataka matendo bana. Kama maneno tu tumeyasikia mengi na matamu. Wapi matendo?
 
Tatizo letu huwa tunachagua viongozi "wanaoishi kwenye nyumba za vioo" tukitegemea wawapige mawe wabaya wetu.
 
Wakati mwingine nasikia kichinachina, kwa nchi ambayo imetawala kwa amani miaka 46 labda ndiyo sumu iliyotutia ganzi! Maana nchi zote ambazo zimepitia misuko suko zimekuwa na ujasiri wa kuangalia nyuma yake. Amefanya hivyo mama wa Liberia, Sierra Leone, na kwingine.

Halafu siyo kama vile sisi hatuna pa kuanzia; tunapo - Mkapa & Yona Deal. Kwanini tusianzie hapo tu?

Upande mwingine sidhani siri ni kubadili chama, naamini siri kubwa ni kuwa na mambo mawili makubwa ya kubadilisha:

a. Kuondoa ulazima wa Mbunge kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa na kuhakikisha kuwa mbunge akihama au kujitoa chama hapotezi Ubunge wake (anaweza kupoteza seniority kwenye kamati n.k)

b. Kuhakikisha kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inakuwa huru kweli na kumuondoa Mwanasheria Mkuu kuwa Mbunge na pia asiwe Mshauri wa Ikulu bali msimamizi wa Sheria zote (Chief Law Enforcer). Hivyo Ikulu wawe na Mwanasheria wao.

c. Jeshi la Magereza kutoka Mikononi mwa Waziri wa Mambo ya Ndani au yeyote wa Mawaziri na kuwekwa chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu au chini ya Mahakama. Na Magereza badala ya kusimamia wafungwa n.k wanakuwa ni chombo cha Mahakama ambacho wanawajibika kwa mahakama tu na ndio chombo pekee ambacho kinahakikisha maamuzi ya mahakama yanatekelezwa pale ambapo Polisi au chombo kingine hakiwezi kufanya kazi. Nina maana wanakuwa kama US Marshalls.

Sasa hayo mambo yako makubwa mawili unafikiri yanawezekana kubadilishwa chini ya CCM? Kama ndiyo, kwa nini hawajayabadilisha hadi hivi sasa kama yanaweza kutuletea manufaa?
 
good question, let me read my book again... I missed something. I think I skipped the page that has CCM written over it.. LOL
 
Good to know!

Well, tuwe na matumaini, kwani our peers, Sierra Leone, (one of the poorest.....) wenzetu kila listi hizi zinapotajwa; wameanza, labda na sisi Tanzania tumo njiani. Mambo haya huja kwa vipindi kama upepo wa kusi.
 
Kwanza jambo dogo tu kama ripoti ya BoT imeshafunikwa kombe ili mwanaharamu apite. Hayo mambo makubwa tutaweza vipi ndani ya mfumo huu wa CCM? natamani tuweze lakini naumia kuona hatuwezi. Tufanyaje jamani? Tuendelee kupiga kelele tu? We need to do something with our hands now, we have been doing too much with our mouths, it's enough now!
 
Well, not really a reliable formular, Zambia with Chiluba did the opposite.

Lakini hata huko Zambia mwanzo haikuwa Chiluba, ilikuwa kwanza kuiondoa UNIP na Kaunda na hayo mengine yakaja baadaye, wewe unaanzia katikati, nenda nyuma kidogo yaani kwenye mzizi.
 
Upande mwingine sidhani siri ni kubadili chama, naamini siri kubwa ni kuwa na mambo mawili makubwa ya kubadilisha:

Well, inawezekana TZ tukaandika historia mpya, lakini so far kote walipochukua hatua kali kama hizo unazotaka walianza kwanza kwa kubadilisha chama kinachotawala, hii ni kote katika nchi masikini na tajiri, zilizoendelea na zisizoendelea na zinazoendelea na zilizodumaa. Sijui ni kwa nini waTZ tunapenda kukwepa option ya kuwafukuza CCM madarakani, why lakini?
 
Tanzania tunatakiwa tufanye mabadiliko makubwa kadhaa ili tujinasue:

(a) Tufupishe kipindi cha serikali kutoka miaka mitano hadi miaka mitatu (Kama Australia).

(b) Tuunde tume huru ya utumishi (Civil Service Comission) yenye kukaa madarakani miaka mitatu tu. Kazi yake iiwe ni kusimamia ajira za kitaalamu serikalini.

(c) Tumpunguzie madaraka rais wetu; asiteue watu wengi sana

(d) Tutenganishe kabisa vitengo vye serikali: utendaji, bunge na mahakama.

(e) Tuwe na utaratibu wa wazi kabisa wa kuwavua madaraka wabunge na rais anayeonyesha kushindwa kutimiza majukumu yake hata kabla ya kipindi chake kuisha.

....... na mengineyo mengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom