Wiki hii nilipata fursa ya kupita mbagala na kuzungukia mitaa michache na hiki ndio nilichokiona;
1.Kwa wenyeji Mbagala hujulikana zaid kama "Mbajala"
2.Mbagala ina watu wengi sana na pilikapilika ni nyingi sana.
3.Nyumba nyingi zimetenganishwa na njia na vipenyo finyu sana lakini ndani kuna sofa! sijui hata hizo sofa zinapitaje
4.Kuna ujamaa sana watu bado wanachangia matumiz ya vitu mbalimbali nimekuta jamaa watano wamejipanga kwa kinyozi wanahudumiwa kwa wembe mmoja!
5.Kuna ukaribu baina ya watu kiasi kwamba watu wanafahamiana, kama ni mgeni utajulikana tu.
6.Kuna biashara kubwa ya vitu feki / pirated hasa cd, tv n.k
7.Ofisi ya imamu ni moja ya ofisi muhimu sana pengine kuliko hata ya mjumbe wa mtaa
8.Kuna uwingi wa ofisi za wataalam wa tiba asili pengine kuliko hata maduka ya madawa.
9.Wakazi wa huko hupendelea sana sherehe zinazokwenda kwa majina mbalimbali kama kumtoa mwali, maulidi n.k, sherehe husherekewa kwa shangwe na vigelegele na akina dada na akina mama ambao wengi wao huvalia nguo nyepesi za kuangaza almuradi kila kitu burudani!
Jaman hii ndio Mbagala niliyoiona mimi, Je Mbagala yako ikoje?