Taswira ya Mbagala

Taswira ya Mbagala

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,436
Wiki hii nilipata fursa ya kupita mbagala na kuzungukia mitaa michache na hiki ndio nilichokiona;

1.Kwa wenyeji Mbagala hujulikana zaid kama "Mbajala"
2.Mbagala ina watu wengi sana na pilikapilika ni nyingi sana.
3.Nyumba nyingi zimetenganishwa na njia na vipenyo finyu sana lakini ndani kuna sofa! sijui hata hizo sofa zinapitaje
4.Kuna ujamaa sana watu bado wanachangia matumiz ya vitu mbalimbali nimekuta jamaa watano wamejipanga kwa kinyozi wanahudumiwa kwa wembe mmoja!
5.Kuna ukaribu baina ya watu kiasi kwamba watu wanafahamiana, kama ni mgeni utajulikana tu.
6.Kuna biashara kubwa ya vitu feki / pirated hasa cd, tv n.k
7.Ofisi ya imamu ni moja ya ofisi muhimu sana pengine kuliko hata ya mjumbe wa mtaa
8.Kuna uwingi wa ofisi za wataalam wa tiba asili pengine kuliko hata maduka ya madawa.
9.Wakazi wa huko hupendelea sana sherehe zinazokwenda kwa majina mbalimbali kama kumtoa mwali, maulidi n.k, sherehe husherekewa kwa shangwe na vigelegele na akina dada na akina mama ambao wengi wao huvalia nguo nyepesi za kuangaza almuradi kila kitu burudani!

Jaman hii ndio Mbagala niliyoiona mimi, Je Mbagala yako ikoje?
 
Masulupwete

Hizo sifa mbona zipo maeneo mengi ya Dar?Mwananyamala, Mwenge Mlalakua kwa mama chambo, Msasani maeneo ya maandazi road, Mikocheni A, Buguruni, Keko Marumbasi, Keko Mwanga, Keko Machungwa, kurasini shimo la udongo n.k.
 
Last edited by a moderator:
Masulupwete

Teh teh tehe unaweza kuifata njia ukakuta inaishia maliwatoni!
 
Last edited by a moderator:
Namba nne niache wembe shilling mia watu hawachangii wanajua ngoma inaambukizwa kwa wembe
ila sifa zote ni sifa za mitaa yetu
 
Kwa mujibubwa Meck Sadick 70% ya makaazi ya Dar es Salaam ni slums na hizo ulizotaja no sifa mojawapo ya slums kwa hiyo hayo ya mbagala yasikushangaze hali iko hivyo karibu jiji zima la Dae
 
Masulupwete

Hizo sifa mbona zipo maeneo mengi ya Dar?Mwananyamala, Mwenge Mlalakua kwa mama chambo, Msasani maeneo ya maandazi road, Mikocheni A, Buguruni, Keko Marumbasi, Keko Mwanga, Keko Machungwa, kurasini shimo la udongo n.k.

kwa tathimini yako inaonyesha kigogo tunatoka kuitwa uswahilini maana hamjatutaja popote,nachukua fursa hii kumpongeza mbunge wangu iddy azan walau kwa barabara zilizochongwa hadi vichochoroni,na taa zilizowekwa kila kichochoro japo nyengine kutokana na umaskini wa watu wako tunashindwa kuchangia zikawaka ila wasiliana na walochukua mabilioni wakusaidie kuziwasha pia itawasaidia hata wao kuzirudisha hela hizi kihaina ndani ya jamiI
 
Last edited by a moderator:
Masulupwete

Hizo sifa mbona zipo maeneo mengi ya Dar?Mwananyamala, Mwenge Mlalakua kwa mama chambo, Msasani maeneo ya maandazi road, Mikocheni A, Buguruni, Keko Marumbasi, Keko Mwanga, Keko Machungwa, kurasini shimo la udongo n.k.

tena bora umwambie afadhali mbagala kuzuri ushafika vingunguti wewe mtoa hoja?
buguruni,manzese,mikocheni,manzese mbagala hamna ht mafuriko kwa kias km huko kungine
 
Last edited by a moderator:
10.napia ndo waasisi wa vigodoro , mchiriku .

sio kweli vimeanzia vingunguti kwa wazaramo wengi
vingunguti mpaka kesho kuna mdundiko na vigoma vya shalogwai au cha uruguai
 
Kwa mujibubwa Meck Sadick 70% ya makaazi ya Dar es Salaam ni slums na hizo ulizotaja no sifa mojawapo ya slums kwa hiyo hayo ya mbagala yasikushangaze hali iko hivyo karibu jiji zima la Dae

haijui dar angeijua dar asingeisema mbagala
 
Unaposema Mbagala unaamanisha eneo gani?.......maana kuna Kijichi, chamazi, mbande, Mbagala Kuu, Mbagala Rangi Tatu Mzinga etc. , Mbagala ni jina la Tarafa
 
Unaposema Mbagala unaamanisha eneo gani?.......maana kuna Kijichi, chamazi, mbande, Mbagala Kuu, Mbagala Rangi Tatu Mzinga etc. , Mbagala ni jina la Tarafa

Swali zuri sana. Ngoja alete majibu. Ni sawa na kusema Kimara. Kimara ipi?
Dar asilimia 70 haijapimwa. Maeneo hayo yana vitongoji vyenye sifa alizotaja huyo mheshimiwa ambaye nahisi anashangaa Masaki
 
Niliwahi kupita mbagala rangi tatu, chakula cha 1500 unaridhika vizuri tu
 
Niliwahi kupita mbagala rangi tatu, chakula cha 1500 unaridhika vizuri tu

Kama cha kula ni 1500 basi maisha ya huko mbagala ni ghali sana...
Maana huku kwetu 1000 unapata wali ndondo, mchicha,nyama vipande viwili yani unakula hadi unaomba mfuko ubebee mwingine utaobakiza..
 
11.Bila kuwa baunsa hupandi daladala za mbagala!
 
Kuna vitu vingine umetia ushabiki usio na maana eti watu wanachangia wembe! Husituingize kwenye umburula wako hapa.....hivi mbagala utalinganisha na vingunguti, buguruni kwa mnyamani, msasani bonde la mpunga, kinondoni mkwajuni nk,,,,unapewa story za kijiweni unaleta jf...sijui unaaishi wapi lkn kama ni sinza sipati tabu kwani ndiyo wale mnaohamka asubuhi na kutafuta poda kwanza kabla ya pesa na kwenda vijiweni kuzungumzia mbagala.....hawa ndiyo wale wanalala buguruni anashinda masaki
 
Back
Top Bottom