DOKEZO TARURA Moshi ni jipu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mchwa mpaka

Member
Nov 18, 2009
35
70
Miongoni mwa madereva tunaopata changamoto kubwa ni tunaotumia barabara inayoanzia Tembo Road hadi kiwanda cha Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia FM Foundation Pre and Primary School. Barabara imeharibika sana na kipindi cha mvua haipitiki na magari yanakwama.

Mwanzoni tulikuwa tunachepukia barabara ya Sembeti kuanzia kwenye lami, lakini nayo imeharibika kwa hata lori nazo ziliamua kutumia barabara hii baada ya ile ya Tembo Road hadi SBL kupitia FM Foundation kuharibika kabisa na kushindwa kupitika. Mathalan, karibu na mwana CCM aitwaye Kisunda, kuna bomba limepasuka chini ya ardhi wakati mteja akipitisha bomba la maji taka ili kuunga na mfumo wa MUWSA. Wapo vijana hujitokeza na kujaza mawe na kutoza kila gari linalopita kati ya Sh500-1,000 kama ujira wake kwa kazi hiyo ambayo ni wajibu wa TARURA.

Hatuelewi madiwani wa CCM wa kata za Pasua na Bomambuzi wanafanya kazi gani maana wao ndio walipaswa kusimama na wananchi. TARURA wanaleta sababu nyepesi kuwa hawaikarabati barabara hiyo kwa kuwa iko katika mpango wa kuwekwa lami, lakini barabara hii imeharibika ina mwaka wa pili sasa. Ina maana sisi watumiaji wa hiyo barabara hatuna haki kwa vile tu TARURA wana mpango wa kuiweka lami? Kama mwaka mzima huu umefika nusu mmeweka lami mita 100 karibu na SBL wananchi tutateseka hadi lini? Au ni mpaka tuandike malalamiko kwa RC Nurdin Babu?

Au tumlalamikie Rais au engineer Seif CEO wa TARURA? Hebu timizeni wajibu wenu maana barabara nyingine zote zinazoingilia na barabara hii zilikarabatiwa mwaka jana na kuwekwa moram, why hii ambayo watumiaji ni wengi haikuguswa? Hatuamini kama madiwani na watendaji hawapiti barabara hii.

Au kwa vile serikali inajenga shule jirani na FM Foundation basi ndio tutapata fadhila ya ukarabati wa barabara. Acheni ubaguzi hata ibara ya 13 ya Katiba inakataza kufanya kazi kwa upendeleo.
 
Back
Top Bottom